Thursday, 3 December 2015

#Hivi Punde>>Waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim afanya Ziara nyingine ya kushtukiza ya katika bandari ya DSM na TRA.Fahamu zaidi hapa.


Ziara nyingine ya kushtukiza ya waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim katika bandari ya DSM na TRA yabaini upotevu wa makontena 2431.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.
 
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. 
 
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
 
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni.
 
Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).

 
Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners.
 
 Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

 
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.
 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.
 
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. 
 
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.

 
“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.
 
Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba 2014.
 
Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.
 
“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.
 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.

#Hivi Punde>>>>Rais Dkt. Magufuli atoa siku saba kwa wafanyabiashara wakwepa kodi.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John  Pombe  Magufuli amewapa siku saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria
 
Hayo  yamesemwa leo Ikulu  jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika mkutano wake na wadau wa sekta binafsi  alipoamua kufanya mazungumzo nao pamoja na kuwasikiliza maoni  yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Rais  aliendelea kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.

“Tutaangalia namna ya kupunguza utitiri wa ushuru katika bidhaa mbalimbali,mfano katika kipindi cha kampeni niligundua katika Mkoa wa Kagera na Kilimanjaro wanakolima zao la Kahawa,wamekuwa wakitozwa tozo  26 kwa zao hilo na hiyo imechangia kusababisha wafanyabiashara wa zao hilo kufanya biashara haramu ya kupeleka zao hilo kwa magendo kuuza  katika nchi jirani”,alisema Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Dkt.Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli  ameendelea kusema kuwa kama kutakuwa na mfayabiashara yeyote  atakayetaka kuwekeza  na akakwamishwa na  mtu aliyechini ya uteuzi wake  basi mtu huyo ataondoka kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyo toa ajira.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka kwenye machimbo ya madini,kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo  na mazao ya misitu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw.Regnald Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa  Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha uchumi watanzania unakuwa kwa haraka na pia amemuomba mheshimiwa rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa  pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Reginald Mengi akiongea katika mkutano huo na kumuahidi Rais Dkt. Magufuli ushirikiano katika kutekeleza yale anayodhamiria kwenye serikali yake ikiwemo kusimamia ulipaji kodi kwa dhumuni la kuiinua Tanzania kiuchumi
 Baadhi ya Wadau wa Sekta Binafsi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano huo Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Reginald Mengi akimpongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipomaliza kutoa hotuba kwa wajumbe wa Sekta Binafsi nchini Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza Jambo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Reginald Mengi wakati wa Mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi nchini Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.

#Bad News>>Kituo cha redio cha Hits FM, Zanzibar chavamiwa na kuchomwa moto.Fahamu zaidi hapa.

Studeo ya Hits kabla ya kuungua na baada ya kuungua kama inavyoonekana pichani. 
Naibu kamishina wa pilisi Visiwani humo Salim Msangi ameiyambia Redio One kuwa tukio hilo lilitokea saa 7 na dakika 40 Usiku.
Watu hao waliofika kwenye Studio izo walimdhibiti mtangazaji huyo na kumziba mdomo na macho kisha na kutumia mito na makochi yaliyokuwepo hapa kukichoma.
Mtangazaji aliyekuwa pekeyake alisema watu hao walikuwa wamevaa nguo nyeusi na kujifunika sura mtangazaji huyo akujeluhiwa japokuwa walichukua simu yake.

Download nyimbo ya Banana_Zorro_Ft-_Jay_Dee-Peke_yake.Hapa hapa.


#YALIYOJIRI>>>Watu wawili akiwemo mwanasheria na mwalimu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kula njama za kumuua Mwenyekiti wa NEC Jaji Lubuva.Fahamu zaidi hapa.

WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake.

Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.

Wakili wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia yake.

Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yana dhamana.

Wakili Moshi alidai Jamhuri inatambua mashitaka hayo yana dhamana kisheria, lakini inaomba dhamana izuiliwe kwa muda hadi watakapoona inafaa kwa sababu ya asili ya kosa, washitakiwa hawawezi kuwa nje wakati upelelezi unaendelea.

Hata hivyo, Wakili Kaluwa alidai sababu zilizotolewa na upande wa jamhuri hazina msingi kisheria, suala la msingi ni mashitaka yanayowakabili kuwa na dhamana na washitakiwa wapo tayari kutimiza masharti yatakayotolewa na mahakama.

Hakimu Simba alisema pamoja na mashitaka hayo kuwa na dhamana kisheria, kutokana na kosa pamoja na hatua ya upelelezi, mahakama imekubali hoja za upande wa jamhuri hivyo washitakiwa watakuwa rumande. Kesi itatajwa tena Desemba 15, mwaka huu.

#YALIYOJIRI>>>Mahakama ya Kisutu Leo imefuta kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa M/kiti wa CUF Prof.Lipumba na wenzake 30.Fahamu zaidi hapa.

Professor Ibrahim Lipumba alikuwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi.
Kesi hiyo imefutwa rasmi leo  baada  ya DPP kuileleza mahakama kuwa hana nia tena ya kuendelea na kesi hiyo.

#YALIYOJIRI>>>CHADEMA Wasema Magufuli Anatekeleza Sera za Wapinzani.Fahamu zaidi hapa.

Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia  hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, amesema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na  ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku zijazo.

 “Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema Mwalimu.

Mikakati ya Dk Magufuli
Tangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati kadhaa ya kubana matumizi ya Serikali, ili kuimarisha huduma za jamii, sambamba na kufichua na kuminya mianya ya rushwa na ufisadi.

Miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusitisha safari za nje, kupiga marufuku michango ya aina yoyote kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kufuta sherehe za Uhuru zilizotajwa kufanyika Desemba 9 na kuagiza fedha za sherehe hizo zitumike kujenga barabara pamoja na kuibua madudu ya ukwepaji wa kodi la rushwa katika Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mwalimu alisema mambo hayo ni kati ya mengi yaliyokuwa yakipigiwa kelele na Chadema pamoja na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.

“Mambo haya (yanayotekelezwa na Dk Magufuli) tulikuwa tumeyapeleka mbele ya Watanzania ili watuamini na tuwafanyie. Wananchi wanajua nini kilichotokea na si ajabu kuona wao (Serikali iliyopo madarakani) wanachukua ya kwetu na kuyafanyia kazi, maana Watanzania ndiyo walioyachagua na ndiyo waliyokuwa wakiyataka,” alisema.

Huku akitolea mfano hoja za Chadema za ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom) na kuandikwa kwa Katiba Mpya zilivyotekelezwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Mwalimu alisema: “Uungwana ni vitendo (Dk Magufuli) atakapokuwa anayafanya si vibaya akasema jamani haya yalikuwa si ya kwangu bali nimeyakopa kutoka kwa wenzangu.”

Alisema si vibaya kwa kiongozi au chama kuiga mambo mazuri ya chama kingine na kusisitiza kuwa lengo la upinzani ni kuona mambo ya msingi yanafanyika ili nchi iwe na maendeleo.

“Suala atafanikiwa kwa kiwango gani hilo ni suala jingine, kama  anayafanya kwa utashi au kwa kuwahadaa Watanzania hilo ni suala jingine.

Mwishowe kama si lako linakuwa na changamoto katika kulitekeleza,” alieleza.

Alisema wapinzani hawawezi kuishiwa hoja za kuikosoa Serikali ambazo nyingi zinalalamikiwa na wananchi, “Mambo yetu mengi wameyachukua ila swali linakuja je, wanaweza kuyatekeleza? Chadema ni chama chenye ubunifu wa hali ya juu katika kutafuta suluhu ya kero za wananchi.”

Alisema chama hicho sambamba na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  wataendelea kuumiza vichwa ili kutafuta jinsi ya kuzitatua kero zinazowakabili wananchi.

“Tunachokitaka kukiona ni Watanzania wakipata haki zao na maendeleo, waishi  katika nchi yenye demokrasia, utawala bora na misingi mizuri ya sheria,” alisema Mwalimu.

#YALIYOJIRI>>>Mawaziri wa JK watajwa kuhusika Ufisadi wa Mabilioni.Fahamu zaidi hapa.

Watu tisa wakiwamo mawaziri wawili wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete wametajwa kushiriki kwenye kashfa ya rushwa ya Sh13 bilioni wakati Serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Kimarekani 600 milioni (Sh1.3 trilioni) kutoka benki ya Standard ya Uingereza.

Ripoti ya Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi (SFO) ya Uingereza iliyokuwa inafuatilia kashfa hiyo imewataja maofisa hao kuwa ni Waziri wa Fedha ambaye alifukuzwa kazi Mei 2012, na Waziri wa Fedha aliyefariki dunia Januari 2014.

Waziri wa Fedha aliyefukuzwa kazi Mei 2012 alikuwa Mustafa Mkulo wakati aliyerithi nafasi hiyo na baadaye akafariki akipatiwa matibabu Afrika Kusini Januari 2014 alikuwa Dk William Mgimwa.

Wakati ilipowasilisha barua ya pendekezo la mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani 600 milioni (Sh12 trilioni) wizarani, Februari 2012, wizara ilikuwa chini ya Waziri Mkulo na mazungumzo ni kama yalififia kwa muda kabla hayajaanza upya Septemba chini ya Dk Mgimwa.

Kipindi cha uhai wake na kudumu kwake wizarani hapo, ripoti ya SFO iliyowasilishwa katika mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza inasema Dk Mgimwa ndiye aliyeidhinisha kuzinduliwa kwa hati fungani hiyo pamoja na nyaraka nyinginezo.

Mbali ya mawaziri hao, wengine waliokuwamo kwenye timu ya Serikali ya majadiliano ni Ofisa mwandamizi wa Hazina ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Madeni ya Serikali (NDMC). Huyo ndiye aliidhinisha barua ya ada ya mkataba na ile ya mamlaka.

Pia, alikuwamo msaidizi wa ofisa mwandamizi (Msajili wa Hazina) ambaye alipokea barua ya mapendekezo ya mkataba na waraka wa mamlaka kutoka Stanbic. Alihusika pia katika mapendekezo yaliyopitiwa na Waziri Mkulo.

Kamishna Msaidizi na Mshauri wa Sera wa wizara, alipokea barua ya mapendekezo ya mkataba na barua ya mamlaka kutoka Stanbic. Mwenyekiti wa Ufundi wa Kamati ya Madeni ya Serikali (TDMC) alipokea mapendekezo ya barua ya mamlaka na ile ya ada ya mkataba.

Hao ndio walikuwa wanakutana na timu ya maofisa wanne kutoka benki ya Stanbic. Kiongozi wa timu ya Stanbic alikuwa Bashir Awale, ambaye kwa wakati huo alikuwa mkurugenzi mtendaji wa Stanbic. Ingawa ripoti inamtaja kama alifukuzwa kazi Agosti 19, 2013 baada ya kushindwa kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi wa kesi hii, lakini inafahamika kuwa aliacha kazi mwenyewe.

Mwingine alikuwa Shose Sinare, ambaye alikuwa kaimu mkuu wa uwekezaji wa benki hiyo. Alikuwa anawajibika moja kwa moja kwa Bashir na alikuwa kiungo muhimu katika mkataba huu akimjuza mkuu wake kila lililojiri. Alijiuzulu Juni 3, 2013 na hivyo akawa amekwepa uchunguzi.

Ofisa wa  tatu ametajwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha (Mgimwa) aliyefariki dunia 2014. Mtoto huyo, kwa mujibu wa ripoti ya SFO ni mhitimu aliyekuwa kwenye mafunzo ya kazi.

Mtoto wa waziri huyo, Godfrey Mgimwa, ambaye sasa ni mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa alipoulizwa jana kama amewahi kufanya kazi katika benki ya Stanbic alikiri kuwa kwa wakati huo alikuwa akifanya kazi katika benki hiyo, lakini hajui chochote kuhusu mchakato huo.

“Nimesikia habari hizo lakini sifahamu lolote. Kuwa mtumishi wa Stanbic wakati tukio hilo linatokea haimaanishi kuwa watumishi wote walihusika. Nadhani ni uhusiano uliopo kati yangu na waziri ndio unafanya nihusishwe…ni vile tu hatupo naye hivyo hakuna wa kuelezea zaidi. Kwa kuwa mzee amefariki naona inatafutwa namna ya kutengeneza uhusiano uliokuwepo kati ya taasisi zilizohusika,” alisema Godfrey.

Mtu wa nne kwa upande wa Stanbic alikuwa mkuu wa huduma za sheria na usuluhishi wa benki hiyo. Ingawa hakuwa sehemu ya mpango huo lakini alishirikishwa na alifukuzwa kazi Oktoba 31, 2013 baada ya kushindwa kufuata maagizo ya bodi ya wakurugenzi ya kutoa taarifa juu ya ushiriki wa kampuni ya Egma.

Tukio la kwanza kuwakutanisha wahusika wengi waliotajwa ni mkutano kati ya wawakilishi wa benki ya Standard, Stanbic na Waziri Mgimwa Mei 28, 2012 kujadili pendekezo la mkopo wa Dola za Kimarekani 550 milioni na siyo Dola 600 milioni. Bashir na Sinare waliiwakilisha Stanbic.

Siku chache kabla ya mkutano huu, Bashir alikuwa ametuma barua wizarani hapo akifafanua na kubadili baadhi ya vipengele vya pendekezo la mkataba wa Februari 2012. Katika barua hiyo, alieleza kuwa endapo wizara ingeendelea na mpango huo basi mkataba wa mkopo na nyaraka nyingine za kisheria ziwe kati ya wizara na serikali na si mamlaka nyingineyo.

Siku chache baada ya mkutano huo, Dk Mgimwa alimtuma mwanaye na kumpatia barua ya utambulisho kwa mkurugenzi wa Stanbic. Bashir aliahidi kuwa angemsaili yeye mwenyewe. Alikutana naye Julai na akaidhinisha kuajiriwa kwake chini ya mpango wa wahitimu walio kwenye mafunzo ya kazi na kukabidhiwa kwa vijana walioongozwa na Shose Sinare. Kwenye mchakato huo, inaelezwa kuwa mtoto huyo wa waziri alikuwa na ushiriki fulani mdogo uliofanikisha mkataba huo.

Waziri Mgimwa, Msajili wa Hazina pamoja na msaidizi wake wakiwa na aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Bodi ya Egma, Harry Kitillya walisafiri kama ujumbe wa Tanzania ulioshiriki mkutano wa wawekezaji kwa lengo la kunadi pendekezo la kuuza hati fungani hiyo ambao uliandaliwa Benki ya Standard. Mkutano huo ulifanyika Februari 2013 na akihudhuriwa pia na Bashir na mwakilishi wa Standard.

Haya yamewekwa wazi na ripoti hiyo ya SFO yenye kurasa 55 ambayo ni matokeo ya uchunguzi wa ndani uliofanywa na mwanasheria wa benki ya Standard ya Uingereza, Jones Day. Baada ya uchunguzi huo Day aliwasilisha SFO ushahidi wote wa kimaandishi, baruapepe, simu na mazungumzo mengine aliyokusanya ya wote waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za kibenki. Ripoti hiyo iliyotolewa Novemba 25, ndiyo imetumiwa na SFO katika shauri lililoendeshwa kwa mfumo wa mtindo wa makubaliano ya kumlipa fidia mlalamikaji (DPA) kwenye mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi Februari 2012 mapendekezo yalikuwa riba ya mkopo huo iwe asilimia 1.4. Baada ya Mukulo kuondolewa Sinare aliwahakikishia maofisa wa benki ya Standard ya Uingereza kwamba japokuwa hati ya uthibitisho ilikuwa haijatiwa saini “dili letu liko salama kwa sababu Serikali inahitaji fedha na dili letu linaungwa mkono na timu ya ufundi pamoja na maofisa waandamizi serikalini.”

Dk Mgimwa alipoiingia Mei 2012 mazungumzo yalizorota lakini yalipofufuliwa Septemba 2012 riba ilipandishwa hadi asilimia 2.4 kwa maelezo kuwa asilimia moja ni kwa ajili ya wakala wa Tanzania kampuni ya Egma (Enterprise Growth Markets Advisors Limited).

Benki zote mbili yaani Standard ya Uingereza na Stanbic zilijulishwa na Serikali ilifahamishwa.

Waliosimamia kidete ongezeko la asilimia hiyo moja ni Awale na Sinare. Novemba 2012 yaani miezi miwili baada ya kuipenyeza Egma katika mpango huo na kuilipa asilimia moja, ndipo Serikali iliwasilisha rasmi barua yake kwenye benki ya Standard na Stanbic ya mkopo wa Dola 550 milioni. Hadi mkataba huo unakamilishwa Machi 2013 kiwango cha mkopo kiliongezeka hadi Dola 600 milioni.

Stanbic ndiyo iliilipa Egma Dola 6 milioni (Sh12 bilioni) ambapo Mkurugenzi mtendaji wake Dk Fratern Mboya alizichota katika mikupuo minne kati ya Machi 18 na 27, 2013.

Ufisadi huu umeishtua Serikali ambapo juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema Serikali imeanza kuzichunguza benki ya Stanbic na Egma kutokana na kuhusika katika udanganyifu wa riba ya mkopo huo. Tayari Stanbic imekubali kurejesha fedha hizo.

Download nyimbo ya Tunda_Man-Mama_kijacho.Hapa hapa.


Download nyimbo ya KECHU Ft. Barnaba-Migogoro.Hapa hapa.


Wednesday, 2 December 2015

Tuesday, 1 December 2015

#Breakiking News>>>Basi la Takbir ajali likitokea Dar kwenda Mwanza lasababisha vifo vingi huko Shelui, Singida usiku huu.Fahamu zaidi hapa.

Kuna ajali imetokea muda si mrefu, ikihusisha basi la Takbir likitoka Dar kwenda Mwanza.

Ffuatilieni kama nduguyo au jamaa yako alikuwepo humo. Waliokufa ni wengi balaaa..upande wa dereva wamebaki wawili tu mana kwa haraka maiti nyingi zimeripotiwa kupatikana.
 Poleni Majeruhi na Poleni Wafiwa.

Kaa tayari kwa ujio wa Producer-Yona endelea kufatilia hii page.

Producer-Yona ni kijana anae kuja kwa kasi Jiji Dar-es-salaam kwa kufanya mixing za hatari unaitaji kuwa msanii nyimbo yako iwe nzuri wala usiangaike jibu lako liko kwa Producer-Yona ambae anapatikana Ubungo Liverside kalibu na bango la Mzee wa Upako karibuni sana wasanii kwa mawasiliano yako juu.

#YALIYOJIRI>>>Taarifa Rasmi ya IKULU Kuhusu Sakata la Ufisadi wa Mabilioni katika Serikali ya JK Lililoibuliwa Jana.Fahamu zaidi hapa.

1.0  Utangulizi
1.1 Jana, tarehe 30 Novemba, 2015, mahakama jijini London ilitoza Standard Bank $ 32.2 milioni. Kati ya hizo $ 16.8 milioni ni faini inayolipwa kwa Serious Fraud Office (SFO), $8.4 milioni ni “disgorgement of profits”; na $ 7 milioni zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania. Fedha hizo ni $ 6 milioni ambazo tulitozwa isivyostahili na $ 1 milioni ni riba ya fedha hizo. Fedha tunazorejeshewa zililipwa isivyostahili kwa kampuni ya Kitanzania iitwayo EGMA. Kesi inayohusika ilifunguliwa na SFO dhidi ya Standard Bank.

1.2 Mwaka 2012/13, Serikali ya Tanzania iliamua kukopa fedha ($600 milioni) kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Huu ni utaratibu wa kawaida, ambapo Serikali inaingia mkataba na Benki moja (Lead arranger) ambayo inatafuta fedha kutoka kwenye benki na taasisi nyingine za fedha. Ni utaratibu wa kawaida pia kuwa Lead Arranger analipwa ada kwa kazi hiyo.

1.3 Serikali ya Tanzania ilitoa kazi hiyo kwa Standard Bank, kupitia Stanbic (T) Ltd. Fedha tulizohitaji, $600 milioni ambazo wakati huo zilikuwa sawa na Sh.947,673,240,000.00 zilipatikana na zikatumika kama ilivyokusudiwa. Standard Bank ililipwa asilimia 2.4 ya fedha hizo kama ada yao. Mkopo ulikuwa na masharti ya grace period ya miaka miwili na nusu na kulipwa kwa miaka 7 (2019).

2.0  Uchunguzi Nchini Tanzania
2.1 Mwaka 2013 kulikuwa na matatizo kwenye Stanbic Bank (T) Ltd, wakati huo ikiongozwa na Bwana Bashir AWALE. Kwa kutumia mamlaka yake chini ya Kifungu 47 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 na Kifungu 31 cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ilifanya ukaguzi wa kulenga (Targeted Examination) benki hiyo.

2.2 Wakaguzi wa Benki Kuu, pamoja na mambo mengine, walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya Kitanzania inayoitwa EGMA. Malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki, na baadhi ya watumishi wa Stanbic Bank (T) walishindwa kuvumilia hali hiyo. Wakaguzi wa Benki Kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa Stanbic Bank (T) ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki. Fedha kiasi cha $ 6 milioni kiliingizwa kwenye akaunti ya EGMA na siku chache baadaye zilitolewa zote kwa fedha taslimu na wala benki haikukusanya kodi ya zuio (withholding tax) kwa mujibu wa sheria ya mapato ya kodi ya mwaka 2004 kutokana na mapato ya Standard Bank kwa kazi ya ushauri iliyoifanya.

2.3 Kama ulivyo utaratibu, Benki Kuu ilitoa taarifa ya ukaguzi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Stanbic Bank (T) Ltd na kuitaka Bodi hiyo kuchukua hatua za kurekebisha kasoro ndani ya benki, pamoja na kutoa taarifa kwa Financial Intelligence Unit kuhusiana na miamala yenye mashaka kwenye akaunti ya EGMA kwa mujibu wa Sheria ya Anti-Money Laundering Act 2006.

2.4 Taarifa tulizopewa ni kuwa bodi ilikutana na kuchukua hatua zinazostahili, ikiwemo kutoa taarifa FIU kuhusiana na miamala kwenye akaunti ya EGMA, na kwa Wizara ya Fedha kuhusiana na kodi ya zuio.

2.5 Vile vile tumesikia kuwa bodi ya Standard Bank iliona kuwa makosa yaliyobainishwa na wakaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania yalistahili kutolewa taarifa kwa SFO nchini Uingereza ambao walianzisha uchunguzi ambao hatimaye ulipelekea kesi kufunguliwa.

3.0 Udanganyifu ulivyofanyika
3.1 Kwa taarifa zilizopo, inaelekea kuwa Standard Bank ilipanga kututoza ada ya asilimia 1.4 tu, yaani $ 8,400,000. Hata hivyo ukafanyika ujanja wa kudai kuwa ati anahitajika local agent wa benki hiyo, ambaye naye alipwe asilimia 1 nyingine, na kufikisha ada yote kuwa asilimia 2.4 ($14,400,000).

3.2 Local agent huyo alikuwa kampuni ya EGMA, ambayo miamala yao kuhusiana na hizo $6,000,000 walizochukua ndiyo ilishtua wakaguzi wa Benki Kuu na taarifa kutolewa kwa Bodi ya Stanbic (T) Ltd na hatimaye Standard Bank, SFO na Mahakama Uingereza.

4.0 Uchunguzi Uingereza
4.1 Tarehe 29 Septemba, 2015, Mkuu wa Idara ya Rushwa kwenye SFO aliiandikia Benki Kuu, akiomba ushirikiano wa Benki Kuu kwenye uchunguzi na uendeshaji wa kesi dhidi ya Standard Bank Plc (ambayo sasa inajulikana kama ICBC Standard Bank Plc).

4.2 Tarehe 29 Oktoba, 2015, Benki Kuu, iliiandikia SFO kutoa taarifa kuhusu ukaguzi-lengwa ambao Benki Kuu iliufanya tarehe 15 – 19 Julai, 2013 kwenye Benki ya Stanbic Bank (T) Ltd. Ushahidi huo kutoka Benki Kuu ulikuwa sehemu ya ushahidi uliosaidia SFO kushinda kesi. Katika kipindi chote ambacho SFO ilikuwa inafanya uchunguzi, ilishirikiana na taasisi zetu ikiwamo TAKUKURU, Benki Kuu, FIU na wengine. Mafanikio haya yaliyopelekea kwenye uamuzi wa Tanzania kurejeshewa $ 7 milioni (Sh.15 bilioni/=) yametokana na dhamira  ya kweli ya Serikali ya  Uingereza na Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa.

5.0 Hitimisho

5.1 Tunaishukuru Serikali ya Uingereza, pamoja na SFO, kwa kuonesha njia katika kusaidia nchi maskini zinazodhulumiwa na wapokea rushwa na watoa rushwa. Maana zipo nchi nyingine tajiri ambazo wanapigia kelele rushwa kwa kuangalia upande wa mpokeaji tu, na kusahau makampuni makubwa kutoka kwao yanayopenda kuhonga watu wetu. Natoa wito kwa nchi nyingine tajiri kutoa ushirikiano kama huu wa Serikali ya Uingereza. Nazishukuru taasisi zetu, Benki Kuu, na TAKUKURU, FIU na wengine kwa kutimiza wajibu wao na kutoa ushirikiano kwa SFO uliowezesha SFO kushinda kesi hii, na sisi kurejeshewa fedha ambazo zitatumika kutatua matatizo yetu ya maendeleo na kero za wananchi.

5.2 Baada ya ushindi huo uchunguzi unaendelea ndani ya nchi ili tujue hizo $ 6 milioni zimekwenda wapi, na kama zilitumika kumhonga mtu tujue ni nani. Katika hili tutaomba ushirikiano wa wenye kampuni hiyo ya EGMA ambao kwa taarifa za vyombo vya habari vya Uingereza ni Bwana Harry KITILLYA, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana MBOYA ambaye ni marehemu na Bwana Gasper NJUU.  

#YALIYOJIRI>>>Kashfa Nzito ya Ufisadi Wa Trioni 1.2/- Katika Serikali ya JK Yaibuliwa na Zitto Kabwe.Fahamu zaidi hapa.

Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la kuchunguza makosa ya jinai (AFO), imeibua kashfa ya rushwa katika ununuzi wa dhamana (hati fungani) ya serikali katika kipindi cha uongozi wa aliyekuwa Rais Jakaya Kikwete.

Madai hayo yametolewa jijini Dar es Salaam jana na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, katika taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari jana.

Katika taarifa yake hiyo, Zitto alidai kuwa biashara hiyo iliyofanyika kati mwaka 2011 na 2012, iliyohusisha serikali na benki ya Standard Group ya Afrika Kusini kupitia Stanbic ya Tanzania ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 600 (sawa Sh. Tanzania trioni 1.2).

Benki ya Standard Group ambayo ni benki mama ya Stanbic Tanzania, imekiri makosa hayo na kukubali kulipa faini ya Dola milioni 25.2 (sawa na Sh. bilioni 54 ) kwa kosa hilo.

Ilikubali kulipa faini hiyo mbele ya Jaji Lord Justice Leveson, wakati shauri hilo liliposikilizwa jana kwenye Mahakama ya Southwark nchini Uingereza.

Benki hiyo ilikubali shauri hilo limalizwe kwa njia ya muafaka baada ya kukiri ilitoa kiasi cha fedha ili kuwahonga maofisa wa Tanzania kinyume na Sheria ya Rushwa ya Uingereza ya mwaka 2010 kufanikisha mpango wao.

Pia benki hiyo imekubali kulipa kiasi cha Dola milioni saba (sawa na Sh. bilioni 15.1) kwa Serikali ya Tanzania kama fidia ya shauri hilo baada ya kubainika walihonga baadhi ya maofisa wa Tanzania kufanikisha mpango huo.

Hata hivyo, fedha hizo hazitakabidhiwa moja kwa moja kwa Serikali ya Tanzania bali zitapitishwa kwenye Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza ili kupangiwa kazi ya kufanya.

Pia benki hiyo inatakiwa kulipa kiasi cha pauni 300,000(sawa na Sh. milioni 974) ikiwa ni gharama za shauri hilo kusikilizwa nje ya mahakama.

Katika taarifa yake, Zitto alitaka mamlaka zenye kuchunguza sakata hilo ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kudhibiti Biashara Haramu ya Fedha (FIU) Tanzania na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru) waungane na SFO kutoa  taarifa za chunguzi huo na sababu ya kutoziweka hadharani mapema.

Aliomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua wote waliohusika na upotevu fedha hizo za Watanzania.

Alisema hati fungani hiyo ya serikali iliuzwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa benki hiyo ya kigeni ambayo ni miongoni mwa kundi la mabenki ya Afrika ya Kusini, yenye makao makuu yake London, Uingereza.

Alisema ni jambo la kawaida duniani serikali kuuza dhamana zake za hati fungani, lakini kwa Tanzania uligubikwa na harufu ya rushwa na kuisababishia nchi hasara.

Alidai kuwa kwa mujibu wa uchunguzi huo, sehemu ya fedha hizo hazikuingia kwenye akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za hati fungani hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati.

Kutokana na upaishaji wa gharama hizo, takriban Dola milioni 60 zilitolewa kwa maofisa waliothibitisha biashara hiyo.

Zitto alimuomba Rais Dk. John Magufuli, kuingilia kati suala hilo akisema jambo hilo lina maslahi mapana ya nchi, hasa ikizingatiwa na uzoefu katika masakata kama hayo yanayohusisha nchi za kigeni, kama ununuzi wa rada, vyombo vya uchunguzi vya hapa nchini, vilitoa majibu ya kutokuwapo kwa rushwa na kisha kuja kuthibitishwa na Serikali ya Uingereza.

“Baada ya kuthibitishwa na Uingereza, serikali yetu ilirudishiwa sehemu ya fedha zilizozidi kwenye manunuzi ya rada, ni vyema Rais Magufuli akaliingilia kati,” alisema Zitto.

Alisema ACT-Wazalendo inasubiri taarifa ya makubaliano kati ya SFO na benki mama ya iliyonunua hati fungani hiyo ili ashauri zaidi hatua za kuchukua.

“Ikumbukwe kuwa Benki ya…(anaitaja jina), ilihusika na kashfa ya Tegeta Escrow na mpaka sasa haijachukuliwa hatua zozote kama ilivyoagizwa na Bunge. Benki hiyo imewaficha waliochota fedha za Escrow mpaka leo,” alisema Zitto.

Alisema kashfa hiyo iliwafanya washauri uongozi wa benki hiyo hapa nchini kuondolewa na kurejeshwa nchini Uingereza kwa hatua zaidi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Hazina, Ramadhani Kijja, alisema kuwa halifahamu suala hilo na kwamba kwa sasa hana maelezo yoyote juu ya jambo hilo.

“Kama Zitto ndiye katoa hiyo taarifa, mimi sina na wala siwezi kuizungumzia kwa sasa,” alisema Kijja.

#YALIYOJIRI>>Rais John Magufuli Atangaza Kupunguza Wafanyakazi Katika Mshirika Ya Umma Ambayo ni Mzigo kwa Serikali.Fahamu zaidi hapa.

Mamia ya wafanyakazi katika mashirika na taasisi mbalimbali za umma zinazoendeshwa kwa hasara likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wako hatarini kufutwa kazi kufuatia amri ya serikali  ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kupunguza mzigo wa gharama za uendeshaji katika taasisi hizo.

Mashirika hayo yameelezwa licha ya kuwa na watumishi wengi, lakini bado uzalishaji na utendaji wake umekuwa hauna tija kwa taifa.



Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Msajili wa  Hazina,  Laurence Mafuru,  katika kikao na wenyeviti wa bodi na wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya umma.

“Kuna kampuni ambazo zimepewa mtaji na serikali, lakini zinashindwa kuzalisha. Zinaandika barua kuomba msaada Serikali Kuu. Kama unaona (mkuu wa taasisi) una wafanyakazi wengi na huzalishi kwa namna inayotarajiwa, ni vyema upunguze watu,” alisema Mafuru.

Kadhalika, licha ya kutoa maelekezo hayo, Mafuru alizitaja taasisi kadhaa zinazoendeshwa kwa hasara au kuzalisha chini ya kiwango kinachotarajiwa kuwa ni Tanesco, Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Shirika la Ndege (ATCL), Kampuni ya Simu Tanzania ( TTCL) na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Maafuru alizitaja taasisi na mashirika mengine yasiyofanya vizuri kuwa ni Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mamlaka ya Bandari (TPA), Kampuni ya Miliki ya Rasilimai za Reli (Rahco) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Mafuru alisema Serikali haihitaji kuvuna fedha katika taasisi hizo, bali jambo kubwa ni kuona kuwa zinajiendesha na kutimiza malengo yanayotarajiwa na umma wa Watanzania.

“Serikali haihitaji kuchukua fedha katika taasisi hizi. Isipokuwa tunataka (taasisi za umma) zifanye kazi na ziwe nguzo za uchumi wa nchi. Tuache bajeti inayotengwa (na serikali) ifanye kazi nyingine ya maendeleo kwa Watanzania,” alisema, huku akiyataja Tazara na TRL kuwa ni vinara wa kuomba fedha kwa Serikali Kuu ili kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.

“Kwa mfano Tanesco, kwa kipindi chote ilichoanza kufanya kazi mpaka sasa tulitarajia iwe imefanya kazi nzuri ya uzalishaji, lakini badala yake tunaona kinyume chake na hapo isitegemee kwamba endapo itaendelea kufanya hivyo serikali itakuwa inaangalia tu,” alisema.

“Ni vema kama kuna shirika au taasisi ya umma ambayo inaona haizalishi na ina wafanyakazi wengi iwapunguze wafanyakazi hao. Kama tunaona tunashindwa, ni vyema tupunguze watu au turudi nyumbani tukapumzike,” alifafanua Mafuru.

Mafuru aliongeza kuwa baadhi ya sababu za kufanya vibaya kwa taasisi na mashirika ya umma ni uzembe wa baadhi ya watumishi ambao hawafanyi kazi kwa kiwango kinachotarajiwa na wala kuwajibika ipasavyo katika kutimiza majukumu yao.

Alisema tatizo jingine ni viongozi wa baadhi ya taasisi na mashirika hayo ya umma kuchukulia nafasi za uteuzi wanazopewa kuwa ni zawadi, fikra ambazo hivi sasa wanapaswa kuzifuta mara moja na kutanguliza zaidi uwajibikaji hasa kwa kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano inaangalia zaidi utendaji wenye matokeo chanya kwa umma na siyo kinyume chake.

“Msifikiri kwamba nyie ndiyo wapishi (wajuzi) pekee… wapo watu wengine wanaojua zaidi, kwa hiyo mjiandae kufanya kazi. Kila mtu atawajibika kwa nafasi yake,” alisema.

Alisema  pamoja na kwamba serikali imezipa mali  taasisi hizo kujiendesha, lakini zimendelea kuwa mzigo kwa serikali kwani baadhi hushindwa kuzalisha na kuwa vinara wa ‘kutembeza bakuli’ kwa maana ya kuomba msaada kwa Serikali Kuu mara kwa mara.

Mafuru alikitaja Chuo cha IFM kuwa ni mojawapo ya taasisi za serikali zinazoshangaza kwani licha ya kuwa na fursa ya kuzalisha, bado kimekuwa kikiendeshwa kwa hasara na kuwa miongoni mwa vinara wa kuomba msaada kwa Serikali Kuu.

“Kwa mfano Chuo Kikuu binafsi cha Tumaini, kinajiendesha kutokana na ada za wanafunzi pekee. Kwa nini IFM inashindwa kufanya hivyo?” alihoji.

Alisema taasisi zinazojiendesha kwa hasara zimekuwa mzigo mzito kwa serikali, hivyo ni lazima sasa kwa wakuu wa taasisi husika kuhakikisha kuwa wanaongeza ufanisi ili kujikwamua kutoka katika hali mbaya kiuchumi waliyonayo.

“Hivi sasa serikali ina taasisi 220 kutoka 600 zilizokuwapo awali. Pamoja na kwamba taasisi za serikali zimepewa assets (mali) za kuzalisha, bado (baadhi) zimeshindwa kufanya hivyo, badala yake nyingine kila siku zinaandika barua kuomba fedha katika Mfuko Mkuu wa Serikali kuongezewa mtaji,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mafuru alisema inasikitisha kuona kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ni miongoni mwa taasisi zisizozalisha kwa kiwango kinachotarajiwa na kwamba hadi sasa, hakuna faida yoyote ambayo imekuwa ikirudisha serikalini.

Alisema kama TPA inafanya vizuri, ilitakiwa kufanya maendeleo mengine ikiwamo kujenga bandari nyingine.
 
Aliitaka taasisi hiyo na nyinginezo kama TPDC kujifunza kutoka kwa taasisi binafsi juu ya namna ya kuongeza uzalishaji.

Alisema kutokana na uendeshaji wa hasara kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma, matokeo yake mashirika na taasisi hizo, kwa pamoja huchangia asilimia 22 tu ya pato la Taifa kwa mwaka, hali ambayo haipaswi kuendelea.

Wakati huo huo, Mafuru alitoa agizo kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa taasisi za umma ifikapo Desemba 15, zikiwamo zote zilizobainika kuwa hazikuwa zikifanyiwa ukaguzi hapo kabla.

#YALIYOJIRI>>>TRA Yakomaa na Mabasi Ya UDA Kwa Kukwepa Kulipa Kodi.Fahamu zaidi hapa.

Agizo  la Rais Dk. John Magufuli kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kodi nchini, limeanza kuwa mwiba baada ya mabasi ya Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), kukamatwa kutokana na kukwepa kodi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, jana alisema mabasi tisa ya UDA yalikamatwa kutokana na kukiuka sheria za mlipakodi.

Mbali na UDA, Kayombo alisema TRA pia iliyakamata mabasi ya kampuni nyingine kutokana na kushindwa kulipa kodi ambapo walitumia kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart.

Kayombo alisema operesheni ya TRA kuwakamata wafanyabiashara wanaokwepa kodi ni endelevu nchi nzima na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa wanaokaidi kutekeleza sheria.

Hata hivyo, Kayombo hakutaka kuzungumzia kwa undani kuhusu kiwango cha kodi ambacho hakikulipwa na UDA, akidai kuwa hiyo ni siri ya mlipakodi na mamlaka yenyewe. 
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDA, Robert Kisena, alithibitisha kukamatwa kwa mabasi yake ambayo alisema uzembe huo ulifanywa na idara yake ya uhasibu.

Kisena alisema muda wa kulipia kodi ulikuwa umefika, lakini idara yake ya uhasibu haikuweza kulipa viwango vinavyotakiwa.

“Ni kweli kuna magari yetu matatu au manne yamekamatwa na tatizo kubwa ni kodi ya magari, ambayo tulijua mtu wetu wa uhasibu amelipa, lakini kumbe alikuwa hajalipa,” alisema Kisena huku akisisitiza kuwa taratibu za kuyakomboa magari hayo zimefanyika ambapo wamekwishalipia gharama zilizokuwa zinahitajika.

#Breaking Nwes>>Polisi Kwa Kushirikiana na TRA Wakamata Makontena 9.Fahamu zaidi hapa.

Maofisa wa Jeshi la Polisi  Dar es Salaam kwa kushirikiana na TRA, wanayashikilia makontena 9   Mbezi Tanki Bovu baada  ya  kuyatilia shaka kuwa yalikuwa yanasafirishwa kinyememela usiku wa kumakia leo.