Ziara nyingine ya kushtukiza ya waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim katika bandari ya DSM na TRA yabaini upotevu wa makontena 2431.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara
nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo
na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431
yametolewa bila kulipiwa ushuru.
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya
ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita
bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM
na AZAM.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10
tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo.
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa
Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika
na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni.
Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3,
2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona
ukaguzi
wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners.
Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo
inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili
kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.
Katika
hatua nyingine,
Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la
Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi
waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya
mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi
Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza
utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi
cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya
hivyo.
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa
sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala
ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui
mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila
kupata majibu.
Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani
hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya
makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo
ya kuanzia Julai – Novemba 2014.
Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka
Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la
Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa
na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.
“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu
wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja
mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es
Salaam,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA
WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410
DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.
0 comments:
Post a Comment