Timu ya Yanga SC ambayo ni mabingwa
wa Tanzania bara, wataanza na Cercle de Joachim ya Mauritius katika
Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati Azam FC
itaanzia Raundi ya Kwanza.
Azam FC itakutana na mshindi kati Bidvest Wits ya Afrika Kusini na wawakilishi wa Shelisheli amabo hawajapatikana.
Yanga
itaanzia nyumbani kati Februari 12, 13 na 14 mwakani huku ikimalizia
ugenini kati ya Februari 26, 27 na 28 na ikivuka hatua hiyo,
itakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Huku kama ikivuka tena hatua hiyo, itakutana na Al Ahly ya Misri, au mshindi
kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Racing Micomiseng ya
Equatorial Guinea.
Azam FC itaanzia kucheza ugenini kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18, 19 na 20 na ikivuka mtihani huo, itakutana na ama Esperance ya Tunisia, wawakilishi wa Chad au News Stars de Douala ya Cameroon.
Mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo wataanzia Raundi ya awali na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati JKU itacheza na Gaborone ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.
0 comments:
Post a Comment