Mkurugenzi
wa Clouds Media Group ambao ni waandaaji wa tamasha la Fiesta, Ruge
Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo halitakuwepo mwaka huu.
Amesema
wameamua kuahirisha kufanya tamasha hilo mwaka huu kutokana na ufinyu
wa muda uliobaki hasa baada ya kupisha kipindi cha uchaguzi.
“Tulijua
tukimaliza kampeni tutafanya kwa mikoa michache lakini tumeona kwamba
hakuna kitu kizuri kama kumsupport mheshimiwa Magufuli , hebu sasa hivi
turudi kwanza tutulie tuache hii amsha amsha aliyoanza nayo ianze
kufanya kazi tujipange kwaajili ya Fiesta 15 ambayo itafanyika mwaka
kesho,” Ruge aliiambia XXL ya Clouds Fm.
“Tutakuwa
tunafikisha miaka 15 ya Fiesta na nina uhakika itakuwa na ukubwa
inayostahili kuliko kufanya kitu kidogo mwaka huu. Tumeona tuache mwaka
kesho mikoa 15, miaka 15 ya Fiesta itakuwa kubwa zaidi. Hapa Kazi imebidi iivae Fiesta pia,” alisema.
0 comments:
Post a Comment