Thursday, 29 December 2016

MITANDAO ya Kijamii Hatari zaidi Kuongeza Ugaidi.Fahamu zaidi hapa.

Vikundi vya kigaidi vinatumia aina zote mpya za mitandao ya kijamii na teknolojia ya mawasiliano ili kupanua wigo wa mitandao yao sambamba na kufadhili shughuli zao.

Hiyo ni kwa mujibu mwakilishi wa kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi, Delphine Schantz ambapo amesema tovuti na majukwaa mbali mbali kwenye mitandao hiyo inatumika kuchangisha fedha na kununua silaha kupitia kwenye mitandao.

Aidha ameongeza kuwa juhudi za pamoja zahitajika kufuatilia mifumo hiyo kwa kuwa Hakuna nchi mwanachama ambayo ni salama dhidi ya ugaidi au salama dhidi ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ugaidi.

Bi. Schantz amesema kamati yao hivi sasa inafuatilia tovuti zinazohusika na uandikishaji magaidi na uchangishaji fedha lakini jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wana uelewa wa kutosha kuwa mitandao hiyo inaweza kutumika vibaya kueneza ujumbe mbaya wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ugaidi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment