Home »
Habari Moto
» Wakulima wakutwa na kilo 5,000 za bangi.Fahamu zaidi hapa.
POLISI mkoani
Morogoro wakishirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na dawa
za kulevya wamekamata tani tano za bangi, mbegu zake zaidi ya kilo 300
na nyara za serikali yakiwemo magamba 42 ya mnyama adimu kakakuona.
Watu
wawili wamekamatwa kuhusu sakata hilo. Watuhumiwa hao wamekamatwa
katika operesheni maalumu kuanzia Desemba 16 hadi 19, mwaka huu katika
wilaya ya Kilosa na Mvomero.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo,
(SACP), Ulrich Matei, amesema jana kuwa, Polisi wa mkoa, na timu maalumu
ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya kitaifa ikiongozwa na SACP,
Mihayo Msikhela wamewakamata watuhumiwa Ally Rashid Abdallah Manji (36)
na Julius Keneth (40). Amesema, Manji alikamatwa Desemba 19, mwaka huu
majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Kipara, kijiji cha Msengele, Kata
ya Doma, Tarafa ya Mlali, wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na kikosi
cha kudhibiti dawa za kulevya taifa.
Walipompekua mtuhumiwa huyo
mbaye ni mkulima na mkazi wa Doma alikutwa akiwa na bangi viroba 11
vyenye uzito wa kilo 800 ambapo vitano vilikuwa na mbegu na vingine sita
vikiwa na bangi yenyewe.
Kamanda Matei alisema katika upekuzi wa
kibanda hicho mtuhumiwa huyo pia alikutwa na nyara za serikali bila
kuwa na vibali vyovyote.
Nyara hizo ni ngozi ya fungo na magamba 42 ya kakakuona.
Mtuhumiwa huyo alikutwa akimiliki shamba la bangi lenye ukubwa wa ekari 20 na walilitekeleza na moto.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment