Kueleka mchezo wa kirafiki baina ya Everton FC dhidi ya mabingwa wa
SportPesa Super Cup, Gor Mahia, Nguli na balozi wa klabu hiyo ya nchini
Uingereza, Leon Osman ameendelea kutembelea vivutio mbalimbali hapa
nchini kabla ya mchezo wao wa Julai 13 utakao chezwa katika dimba la
Taifa jijini Dar es salaam.
Leon alipata nafasi ya kutembea juu ya daraja linaloshikiliwa na kamba ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Manyara.
Osman ambaye aliwasili wikiendi iliyopita kutoka nchini Uingireza alipata nafasi pia ya kumbelea makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyopo eneo la makumbusho kwa kuweka mashada ya maua.
Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa zaidi huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaona nyota mbalimbali wa Everton kama vile Wayne Rooney, Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.
Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment