Kama wewe ni mfuatiliaji na msomaji wa habari mitandaoni basi bila shaka huenda ulishawahi kukumbana na hali ya kusoma habari ambayo baada ya kumaliza ukaanza kukumbuka kama ulishawahi kusoma habari hiyo sehemu fulani lakini umesahau, basi utakuwa upo sahihi kabisa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na muandishi wa habari mkongwe wa Gazeti la Financial Times, Michael Skapinker amebaini kuwa wasomaji wa habari mitandaoni wengi wao hupoteza kumbukumbu ya kuhifadhi habari walizosoma kwa muda mfupi sana ukilinganisha na wale wanaosoma habari kupitia Magazeti.
Mwandishi huyo amesema asilimia kubwa ya wasomaji wa habari mitandaoni hufikiria zaidi kutoa maoni na kushare habari walizozipenda na sio kutilia maanani kwenye usomaji wa habari.
Utafiti huo uliofanyika kwenye nchi 60 tu umeonesha kuwa wasomaji wengi wa habari mitandaoni wanasoma habari nyingi kwa muda mfupi huku wakifanya shughuli nyingine kitu ambacho kinawafanya wakose umakini wa kuzingatia kile wanachokisoma tofauti kabisa na wale wanaosoma habari kwenye magazeti ambao hupaswa kupumzika kabisa ili kuweza kusoma gazeti.
Kwenye nchi 60 alizofanya utafiti huo, Michael Skapinker amesema kuwa asilimia 85 ya vijana chini ya miaka 40 ndiyo wanaopendelea zaidi kusoma habari za mitandaoni huku 15% wakisoma habari kupitia Majarida na Magazeti.
Hata hivyo utafiti huo umeonesha ingawaje vijana wengi wanasoma habari mitandaoni ila ni wepesi sana kusahau habari walizoma yaani kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi ukilinganisha na wale wanaosoma habari kwenye Magazeti.
Utafiti huo pia umeonesha kuwa ingawaje kuna ongezeko kubwa la wasomaji wengi wa habari mitandaoni lakini bado kuna kundi la wasomaji hawaamini habari hizo mpaka wazikute kwenye magazeti.
Bwana Skapinker amesema ingawaje wasomaji wa mtandaoni hupoteza kumbukumbu haraka lakini bado watu wengi huvutiwa na habari za mitandaoni kutokana na uharaka wa kuzipata, kuokoa muda, kupunguza gharama na urahisi wa kutoa maoni ya walichokisoma.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment