Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema
Barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga imegharimu Sh 190 bilioni.
Waziri Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu ambao wamehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.
Akizindua
ujenzi wa barabara hiyo leo Rais John Magufuli amesema kwamba
Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umasikini na wananchi wanafanya
ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.
Kwa
upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono
msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na
masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli
yake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment