Tuesday 11 July 2017

ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA NA GARI BARABARANI.

Askari wa usalama barabarani “trafiki” mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akitekeleza majukumu yake. 
 
Askari huyo aliyefahamika kwa jina E.51 Koplo Aswile Ambwene amefariki dunia jana asubuhi ya saa 12:30 akiwa kazini eneo la barabara ya Sikonge, kijiji cha Kipalapala kwa Chief, kata ya Itetemia, mkoani Tabora.
 
Mauti ya askari huyo yalisababishwa na gari lenye namba za usajili 564 ALG aina ya Isuzu likiendeshwa na dereva Hasan Husein-Kiula mwenye umri wa miaka 36. Gari hilo lilikuwa likitokea Mpanda kwenda Kahama likiwa limepakia magunia ya mahindi.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo alieleza kuwa Bwana Hasan(dereva wa gari hilo) alisimamishwa barabarani na askari mwenye namba G.4246 Konstebo Abuu lakini dereva huyo aligoma kusimama na kusababisha kumgonga askari namba E.51 Koplo Aswile Ambwene ambaye alipoteza maisha papo hapo.
 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Milambo Jeshini mkoani Tabora.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hap

0 comments:

Post a Comment