Wednesday, 18 September 2019

Old Shule ya Sekondari Tanga inateketea kwa moto.

Shule ya Sekondari Old Tanga inateketea kwa moto ulioanza leo mchana Jumatano Sept. 18, 2019.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amesema chanzo cha moto huo ulioteketeza chumba cha mikutano na cha kuhifadhi vifaa bado hakijafahamika.

Kikosi cha Zimamoto tayari kiko eneo la tukio  kuuzima moto huo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 4 April 2018

Wabunge wa Upinzani Wasusia Bunge Viti Vyao Vyabaki Tupu.

Wabunge wa upinzani wakiwamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni kama wamesusia Mkutano wa 11 wa Bunge ulioanza vikao vyake mjini Dodoma jana huku viti vyao vikionekana vitupu.



Aidha, kutokana na kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), swali laki ilibidi liulizwe na Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF).



Wabunge hao wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ambapo jana wabunge waliokuwapo walikuwa wanne tu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) na wabunge wawili wa Chadema.



Hata hivyo, leo wabunge wa Chadema hawakuwapo kabisa ambapo baadaye walionekana wabunge wawili tu, akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili ambao walionekana kwa muda mfupi kwa nyakati tofauti na kupotea.



Kubenea aliingia bungeni asubuhi na kutoka kabla ya kikao kuanza huku Kamili akionekana nje ya ukumbi wa bunge bila kuingia ndani.



Wabunge wa CUF walikuwapo lakini idadi yao ikiwa haifiki 20 wakati wa kipindi cha maswali na majibu na kubaki tisa pekee baada ya kipindi hicho.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 3 April 2018

Breaking News: Mbowe na Viongozi wa Chadema Waachiwa Kwa Dhamana.

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 3, 2018. Mahakama hiyo imejiridhisha na nyaraka za udhamini zilizowasilishwa mahakamani hapo.



Masharti ya dhamana yalikuwa ni kila mshtakiwa kuwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS 20m, barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.



Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ili kusomewa mashtaka yanayomkabiri.



Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wenzake sita wa Chadema wanaokabiriwa na mashataka manane yakiwemo ya uchochezi, uasi na kuhamasihsa maandamano, hivyo wote kwa pamoja watasomewa mashtaka upya.



Mdee alikamatwa juzi Jumapili akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar wakati akiwasili kutokea nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Mahakama imempa dhamana baada ya kuridhika na sifa za wadhamini.



Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 27 March 2018

Breaking News: Freeman Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Wafikishwa Mahakamani.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Viongozi wa CHADEMA wengine waliofikishwa Mahakamani ni Katibu Mkuu Dr. Vincent Mashinji, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Ester Matiko Mbunge. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mwenyekiti UVCCM Amvaa Waziri Shonza "Mnawafungia Kina Roma, Daimond Mtaimba Nyie".

Kufuatia sakata la kufungiwa kwa baadhi ya wasanii na nyimbo zao, akiwemo Roma Mkatoliki, Diamond Platnumz, Snura na wengine, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James, amekerwa na maamuzi hayo yaliyofanywa na Basata na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kupitia kwa Naibu wake, Juliana Shonza.



Akizungumza jana Mjini Dodoma, Kheri James alieleza masikitiko yake na kusema kuwa wizara hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya wasanii ambao wengi wao ni vijana wanaojitafutia kipato kupitia tasnia hiyo.



“Mmemfungia Roma, mmemfungia Diamond na wengine, kila anaenyanyuka mamkata mguu, hivi mnavyowafungia mtaimba nyie?



“Kama wizara itendelea na tabia hiyo ya kuwafungia wasanii, na wao ndio viongozi wa sanaa je watamsimamia nani wakishawafungia wote?” alihoji Kheri. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Chamsimamisha Masomo Abdul Nondo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye, amemsimamisha masomo Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo hadi kesi yake ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa itakapomalizika.

Nondo alipewa dhamana na mahakama ya Iringa, jana Jumatatu,Machi 2018 baada ya kusota rumande kwa wiki kadhaa


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Monday, 26 March 2018

MAREKANI: Rais Trump ametoa amri ya kufukuzwa kwa wanadiplomasia 60 wa Kirusi.

MAREKANI: Rais Trump ametoa amri ya kufukuzwa kwa wanadiplomasia 60 wa Kirusi, kufuatia Urusi kuhusishwa na shambulio la sumu kwa Jasusi wa zamani raia wa Urusi nchini Uingereza

Tayari nchi za kadhaa za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Ukraine zimetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Kirusi katika nchi zao

Viongozi wa EU walikubaliana wiki iliyopita kuwa inawezekana sana Urusi ilihusika katika shambulio la sumu la Sergei Skripal(Jasusi) na binti yake kusini mwa Uingereza

Hata hivyo, Urusi imepinga kuhusika na shambulio hilo

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 21 March 2018

Mahakama Kuu Iimetoa Amri kwa Serikali Kupeleka Majibu Juu ya Abdul Nondo.

Mahakama Kuu leo imetoa amri kwa serikali kuweza kupeleka majibu ya maombi yaliyofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Abdul Nondo kujibu kesi ya kutompeleka Mahakamani kwa zaidi ya siku 10 tangu kukamatwa kwake.


Amri hiyo imetolewa leo Jumatano ya Machi 21 ambapo Mahakama kuu mbele ya Jaji Sameji  iliwataka DCI,IGP na AG kufika mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtka juu ya Nondo ambapo leo majibu ya maombi hayo wyametakiwa yapelekwe Machi  26 na walalamikaji  kupeleka majibu yao ya nyongeza yapelekwe Machi 27.

Aidha  mahakama inatarajiwa kusikiliza maombi ya pande zote mbili 04/08/18 kutoa hatma ya Abdu Nondo.

Kwa upande mwengine kesi ya mwanafunzi huyo (Nondo)  iliyosikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 26 March 2018 ambapo Hakimu atatoa uamuzi kwamba mshitakiwa apewe dhamana ama asipewe dhamana, mshitakiwa amerudishwa rumande.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Necta Yafanya Mabadiliko Mtihani Darasa la Saba.

Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji  wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi .

Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa  (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.

Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).

Amesema maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Kutokana na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 20 March 2018

Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma.

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika .
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Monday, 19 March 2018

Zitto Kabwe Alishitaki Jeshi La Polisi Mahakamani.

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo, Kabwe Ruyagwa Zitto amefunguka na kusema kuwa chama chake tayari kimefungua kesi ya Kikatiba katika mahakama Kuu Dar es Salaam kulishtaki jeshi la polisi.

Zitto Kabwe amesema hayo leo Machi 13, 2018 wakati akitoa tathmini ya ziara alizofanya kutembelea Madiwani katika kata mbalimbali nchini zinazoongozwa na ACT Wazalendo ambapo amedai katika ziara hiyo wamebaini mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya maisha kuwa ngumu sana, migogoro ya ardhi, kukosekana kwa huduma ya Maji safi na salama, ukosefu wa huduma bora za afya, tatizo la Miundombinu ya Usafirishaji.

Kiongozi huyo aliendelea kuweka wazi mambo mbalimbali ambayo wamefanikiwa kuyaona katika ziara hizo kuwa ni pamoja na  ukosefu wa pembejeo za Kilimo, ukosefu wa masoko ya mazao ya wavuvi, wakulima na wafugaji, kushuka kwa bei ya mazao yao, kupanda kwa gharama za maisha ya watu, kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi, upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, vyoo pamoja na walimu, na kuzorota kwa hali ya usalama wa wananchi pamoja na mali zao, hali mbaya ya ajira kwa vijana pamoja na uminywaji mkubwa wa demokrasia na uhuru wa watu kukusanyika na kujieleza.

"Tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli, ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza. Tunaamini Mahakama itatenda haki kwenye suala hili" alisema kiongozi huyo

Aidha Zitto Kabwe ametoa ushauri kwa serikali kuhusu suala la Demokrasia nchini na kusema kuwa mazungumzo ya kitaifa ndiyo yanaweza kuwa na jibu kuhusu masuala haya na kuleta utatuzi juu ya jambo hili.

"Demokrasia na Ustawi wa Taifa tunaendelea kusisitiza rai yetu kuhusu umuhimu wa kuitisha Mkutano wa Kitaifa wa maridhiano ya kisiasa kama jukwaa la kuzijadili changamoto za uendeshaji wa siasa nchini. Jambo hilo litaondoa uadui unaoendelea kukua sasa kati ya serikali na wananchi, viongozi wa dini, mashiriki yasiyo ya Kiserikali, taasisi za wanafunzi, pamoja na vyama vya Upinzani. Tunaamini mazungumzo ya Kitaifa ndio jambo sahihi la utatuzi wa suala hili" alisisitiza Zitto Kabwe

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 16 March 2018

Baada ya Magari ya Mwendokasi Kusitisha Huduma ya Usafiri Daladala, Bodaboda Zatumia Njia ya Mwendokasi.

Baada ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dart) kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, baadhi ya magari madogo, daladala na bodaboda wametumia fursa hiyo kupitisha magari yao katika barabara zinazotumika na magari hayo.

Mwananchi limeshuhudia daladala zikipita katika vituo hivyo huku zikishusha na kupakiza abiria katika kila kituo cha mwendokasi, huku trafiki wakielekeza baadhi ya magari kutoka kwenye barabara hizo.

Hata hivyo vituo vingi vya mwendokasi vimefungwa isipokuwa kituo cha Ubungo ambacho wahudumu wameonekana wamelala huku kukiwa hakuna abiria  wanaoingia katika kituo hicho.

Dereva wa daladala linalofanya safari zake Mbagala Rangitatu - Simu 2000 Jafari Himid amesema kutokana na foleni iliyopo katika barabara hiyo, wameamua kutumia barabara za mwendokasi ili kuokoa muda.

"Bila kufanya hivi hatuwezi kuwahisha abiria na hizi barabara leo hazina matumizi, hata trafiki wanatuachia hawajatukamata," amesema Jafari.

Hata hivyo barabara ya Morogoro Road ina foleni kubwa inayosababishwa na kipande cha barabara ya jangwani kujaa tope. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 14 March 2018

BREAKING: Goodnews Kwa Watanzania Watakaopenda Kufanya kazi Mradi wa Bomba la Mafuta.

Watanzania watakaopenda kufanya kazi katika Bomba la Mafuta, Bonyeza PLAY hapa chini kutazama. VIDEO: 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 6 March 2018

Gazeti Lililomuandika Mange Vibaya Lapewa Onyo Kali na Serikali.

Serikali imelionya Gazeti la Tanzanite kwa kuchapisha picha za utupu kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada msemaji wa serikali Dkt. Hassan Abbas kuahidi kulichukulia hatua gazeti hilo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na ukakasi wa habari zake pamoja na picha wanazochapisha.


Onyo hilo limetolewa hii leo mjini Dodoma na Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wametoa onyo kwa Gazeti hilo kwakua ni jipya pia ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo hivyo ni bora kujirekebisha.

Amesema kuwa Gazeti hilo halikuwa na kosa katika maudhui ya kuandika ila kosa kubwa ni kutumia picha za utupu, hivyo kwenda kinyume na maadili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Moto Mkubwa Waunguza Soko Mbagala.

Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii Machi 6, 2018.

Sehemu iliyoathirika zaidi ni ile ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika  kuzima moto huo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Picha: Hivi Ndivyo Polepole Alivyonusurika Kufa Baada ya Msafara Wake Kupata Ajali.

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba T150 EWE iliyokuwa ikiendehswa dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hosiptali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Poplepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wameandamana Afrika Kusini Kushinikiza Ukweli wa Kifo cha Mtanzania Alieuawa.

Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya maandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania mwezi February.

Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari la nje ya bweni la chuo kikuu.

Maafisa wa shirika hilo wameandamana kwa pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni linaloitwa Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo aligongwa na kufariki.



Maandamano hayo yalikuwa salama na watu walikusanyika kwenye uzio mahali gari lilipo mgonga marehemu Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.

Mtuhumiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana. Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday, 2 March 2018

Rufaa ya Kupinga Hukumu ya Kifungo ya Sugu, Masonga Yapelekwa Mahakama Kuu.

Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanaotumikia jela miezi mitano imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya jana Machi 1, 2018 na mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imepokelewa katika Mahakama Kuu (Mbeya), sasa tunasubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza. Tunawashukuru watu wa Mahakama hii wameshughulikia vizuri jambo hili,” alisema Mangula.

Mawakili hao wamekusudia kuomba dhamana kwa Sugu na Masonga ili wawe kuwa nje katika kipindi ambacho watakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambapo walitoa kauli hiyo Desemba 30, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 1 March 2018

TCRA Yawazipiga Marufuku Nyimbo za Diamond, Nay, Gigy na Roma.

Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) imepokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupiga marufuku nyimbo hizo kuendelea kurushwa katika vyombo vya habari huku ikisema hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watakaokiuka.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tanzania Yazikataa Meli za Korea Kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga amewafahamisha  mabalozi wa nchi tano ambazo ni wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba meli mbili zilizoonekana zikielekea Korea ya Kaskazini zikipeperusha bendera ya Tanzania;


Inadaiwa kuwa Meli hizo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Tanzania zilionekana kwa njia ya satelaiti, moja ikielekea Korea ya Kaskani moja kwa moja na nyingine ilinaswa ikihamisha mizigo ambayo haikutambulika kwenye meli nyingine ambayo baada ya zoezi hilo la uhamishaji ilielekea Korea ya Kaskazini baada ya kupakia mizigo hiyo.

Balozi Mahiga amewaomba Mabalozi hao kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa Urusi na China kuisadia Tanzania kuweza kuzibaini meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania na kwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa wa usafirishaji baharini.

Januari mwaka huu Tanzania ilizifutia usajili meli zote 450 zilizokuwa zinapeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji ya kimataifa baada ya kupatikana kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na dawa za kulevya huku ikipeperusha bendera ya Tanzania.

Wiki moja iliyopita Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuyawekea vikwazo vya Kiuchumi Kidplomasia Kisiasa na kibiashara mataifa yote yatakayokiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Marekani dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa