Saturday 30 January 2016

#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli Amuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange...Afanya Uteuzi wa Makamanda Wengine wa JWTZ.Fahamu zadi hapa.

RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .
 
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Sanajari na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia Rais Magufuli  amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo  kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
 
Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais  ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.

Jeneral Mwamunyange alimtaja pia  kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.

Mwingine  aliyeteuliwa  na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali George William Ingram kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga ambaye anachukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph  Pwani aliyestaafu leo kisheria  baada ya kufikisha umri wa kustaafu. Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.

Pia Rais Magufuli amemteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo  kuwa  Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo,baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.

Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu  kuwa   mkuu wa shirika la mizinga  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umri .Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.

Pia Rais Magufuli  amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS) kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria .Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
 
Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo  kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo  kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,.Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa Afisa Mnadhimu makao makuu ya Jeshii.
 
Rais Magufulia pia amemteua  Bregedia Jenerali Sylevesta M.Minja kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kazi  leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo kabla ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC

#YALIYOJIRI>>>Taarifa Ya Kukanusha Uvumi Wa Kuwepo Ajira Za Madaktari JWTZ.Fahamu zaidi hapa.

Hivi karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti Makao Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.

Habari hizo si za kweli,JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali lina mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Aidha JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za jeshi bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi kinyume na utaratibu huu,unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano Makao Makuu JWTZ.

#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli Awaapisha Balozi Na Makatibu Tawala Wawili,Amtuea Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu JWTZ.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Januari, 2016 amewaapisha Balozi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania na Makatibu Tawala wawili, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Walioapishwa ni:
Balozi Mahadhi Juma Maalim, ambaye anakuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait.

Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ambaye anakuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, ambaye amestaafu. Kabla ya Uteuzi huu Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa Mkuu wa Usalama na Utambuzi wa Jeshi la wananchi Tanzania.

Kamishna Paul Moses Chagonja, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, akijaza nafasi iliyoachwa wazi Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kamishna Clodwig Mathew Mtweve, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kuwait Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim, ameahidi kuiwakilisha vyema Tanzania nchini Kuwait hususani katika uchumi ili Tanzania iweze kunufaika na ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili.

Nae Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa wananchi Tanzania Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ameahidi kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na Mtangulizi wake Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Albert Ndomba ya kuhakikisha anamshauri vizuri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na hivyo kuliwezesha Jeshi hilo kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Kwa upande wao, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna Clodwig Mathew Mtweve na Katibu wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Moses Chagonja, wameahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye mikoa waliyopangiwa, ikiwemo kusimamia nidhamu kwa watumishi wa umma.

Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
                                                                30 Januari, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016

#YALIYOJIRI>>>Balozi Amina Salum Ali Amuomba Seif Sharif Hamad Kufikiria Upya Uamuzi Wa Kususia Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar.Fahamu zaidi hapa.

Kada aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM, Amina Salum Ali amesema mgogoro wa kisiasa Zanzibar hautakwisha hata baada ya Uchaguzi wa marudio kwa kuwa ni wa kihistoria na baadhi ya viongozi hawana nia ya dhati ya kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani humo.

Balozi Amina pia amesema uamuzi wa CUF kususia uchaguzi wa marudio visiwani humo utasababisha mpasuko mkubwa zaidi na kumtaka katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kufikiria upya na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

Zanzibar imekuwa ikikumbwa na mgogoro wa kisiasa kila inapoingia kwenye Uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka 1995 baada ya vyama vya upinzani kuruhusiwa, na vurugu za mwaka 2005 zililazimisha CUF na CCM kuingia kwenye mazungumzo yaliyozaa SUK.

Lakini dalili za SUK kuendelea sasa zinaonekana kufifia baada ya CUF kupinga uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa, wawakilishi na madiwani visiwani humo Oktoba 28, mwaka jana na kutangaza uchaguzi mpya Machi 20, ambao chama hicho kikuu cha upinzani kimesema hakitashiriki.

Balozi Amina anaona kuyumba kwa Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kunatokana na Maalim Seif kutotambua kuwa maridhiano hutokana na kupata kitu fulani na wakati huohuo kukubali kupoteza kingine.

“Mimi namshauri Seif kujua kuwa katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, afahamu kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania na kwa upande wa Zanzibar, Wazanzibari wanataka maendeleo,” alisema.

“Seif analalamika wakati yuko serikalini, anakutana na mwenzake (Dk Shein) wanakula haluwa na kufurahi pamoja, lakini akitoka nje, anageuka. Tutafika wapi kwa siasa za namna hii?”

Amina alisema Zanzibar ilikuwa na bahati kumpata Dk Shein ambaye Maalim Seif angeweza kumtumia kufanya mambo anayotaka, lakini ameshindwa kugundua fursa hiyo na kuanza kujivuruga.

“Chini ya Dk Shein, Zanzibar imepata fursa nzuri ya kufikia maelewano. Shein anawawakilisha Wazanzibari wote na anajua siasa za Zanzibar ni mstahamilivu, ni mwenye busara, msomi na mpenda maendeleo,” alisema Balozi Amina na kuongeza kuwa:

“Hivyo huu ulikuwa wakati mzuri kwa Seif kushirikiana wafanye anachotaka kwa ajili ya maendeleo ya Wazanzibari.”

Alisema kitendo cha CUF kususia uchaguzi wa marudio kitaongeza mpasuko wa kisiasa badala ya kuupunguza, hivyo ni vyema Seif akaliangalia hilo vizuri na kubadili msimamo huo kwa faida ya Wazanzibari wote.

“Uchaguzi huu wa marudio ndio utakuwa kipimo cha kuonyesha nani anakubalika Zanzibar sasa Seif akisusa maana yake nini?” alihoji.

#YALIYOJIRI>>>Mahakama yamfutia kesi mtuhumiwa wa kupokea fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko, ameachiwa huru katika shtaka la kutuhumiwa kuwa alipokea rushwa ya Sh milioni 40.4 kutoka kwa Mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Saliboko aliachiwa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumuona hana hatia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliyesema mahakama imemuona mshtakiwa hana hatia kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasi na kuacha shaka yoyote.

“Mahakama inaona upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi bila ya shaka. Mshtakiwa (Saliboko) hana hatia, anaachiliwa huru na mna haki ya kukata rufani kwa upande ambao haujaridhika,” alisema Simba.

Alisema mshtakiwa huyo aliposomewa shtaka kwa mara ya kwanza alikana na kwamba wakati wa usikilizwaji upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Dennis Lekayo, ulileta mashahidi watatu ambao ni mpelelezi mkuu na maofisa wawili wa Benki ya Mkombozi iliyoko Ilala, Dar es Salaam.

Pia alisema mshtakiwa anatetewa na Wakili Jamhuri Johnson, alijitetea mwenyewe baada ya mahakama kumuona ana kesi ya kujibu.

Hakimu Simba alisema shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri alikuwa Mpelelezi Mkuu, Emmanuel Koroso, aliyeeleza kuwa alikabidhiwa jalada afanye upelelezi juu ya tuhuma hizo za Saliboko Oktoba 9, mwaka juzi na Mkurugenzi wa Takukuru.

Akichambua ushahidi wake, Hakimu Simba, alisema shahidi huyo alieleza alikusanya hati mbalimbali na kuhoji watu na alijitosheleza fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko na mshtakiwa huyo hakuwa na maelezo mazuri kuonyesha namna gani alipokea fedha hizo.

Alisema mashahidi wawili kutoka Mkombozi, walithibitisha Saliboko alienda kufungua akaunti kama mteja wao na fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya mshtakiwa huyo na alizitoa mara tatu.

Kwa upande wa utetezi wa mshtakiwa Saliboko, alikubali kufungua akaunti ya Mkombozi na kuingiziwa fedha hizo na Rugemalira aliyekuwa na makubaliano naye ya kumtafutia shamba katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam ili aendeleze biashara zake.

Baada ya kuchambua ushahidi huo, Hakimu Simba alisema utaratibu wa sheria ni kwamba upande wa Jamhuri ndio wenye wajibu wa kuthibitisha mashtaka pasi kuacha shaka yoyote na sio jukumu la mshtakiwa kuthibitisha kwamba hajafanya kosa.

“Katika kesi hii, hakuna ubishi kwa upande wa Jamhuri na ule wa utetezi kwamba fedha ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko, hivyo hakukuwa na ulazima wa kuwaleta wale mashahidi wawili kutoka Benki ya Mkombozi.

“Shahidi muhimu aliyebaki ni mpelelezi mkuu ambaye alipohojiwa na wakili wa utetezi alidai hakuna siku hata moja alienda kumuuliza Rugemalira fedha ziliingia katika akaunti ya Saliboko kwa kazi gani. 

"Kwa mujibu wa sheria za Takukuru, mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wakosaji, kama kweli ilikuwa rushwa kwanini Rugemalira hakuletwa mahakamani kushtakiwa maana ni mtoaji,” alisema Hakimu Simba.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Saliboko alikuwa anadaiwa Februari 5, mwaka juzi katika Benki ya Mkombozi, iliyoko wilayani Ilala, Dar es Salaam, akiwa mkuu wa Rita alipokea Sh milioni 40.4 kupitia akaunti ya VIP Engineering ya Rugemalira ambaye alikuwa Mkurugenzi wa IPTL. 

Ilidaiwa alipokea fedha hizo kutokana na kazi yake kama bosi wa Rita wakati IPTL ilikuwa mfilisi na yeye alishughulikia hilo.

#YALIYOJIRI>>>Nchi 12 Za Ulaya na Marekani Zalaani Tume Ya Uchaguzi Zanzibar Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Wakati Mazungumzo Yakiendelea.Fahamu zaidi hapa.

Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza tarehe ya marudui ya Uchaguzi wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro yakiendelea na kumtaka Rais John Magufuli kutumia nafasi yake ya uongozi kutatua mtanziko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Taarifa ya pamoja iliyotumwa kwa vyombo vya habari na mabalozi hao jana, pia inamtaka Rais Magufuli kuendeleza wito wake wa kuzitaka pande zote zitafute suluhu kwa amani.

Tamko hilo limetolewa siku saba baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza kuwa uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani utarudiwa Jumapili ya Machi 20, lakini siku tano baadaye CUF ilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.

Kutokana na sakata hilo, mabalozi hao wamelaani kitendo hicho wakisema kurudia uchaguzi kwa kigezo kuwa utaratibu ulikiuka, kinawatia wasiwasi kwa kuwa tume hiyo haikutoa ushahidi wa ukiukwaji huo.

Mabalozi hao wamesema katika tamko lao kuwa ZEC imerudia kauli yake ya kuwa uchaguzi ulikiuka taratibu licha ya waangalizi kutoka EU, Jumuiya za Afrika Mashariki, Sadc Marekani na Jumuiya ya Madola kufanya tathmini na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru na haki.

“Tunasikitika kuwa ZEC imetangaza tena kuwa uchaguzi utarudiwa Zanzibar, wakati mazungumzo baina ya pande mbili yanaendelea. Kwa manufaa ya Watanzania wote, tunasisitiza kuwa hali ya kisiasa ya visiwani humo ni bora ikatatuliwa kwa pande mbili kukubaliana,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa ushirikiano wa mabalozi wa Uholanzi, Norway, Hispania, Italia, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Sweden, Uswisi, Uingereza, Ireland na Marekani inasisitiza kuwa kitendo cha upande mmoja kuamua kurudia uchaguzi, kinaweza kuzidisha hofu na taharuki miongoni mwa Wazanzibari.

“Tunawaomba Wazanzibari kuwa watulivu na wavumilivu nyakati hizi na tunazitaka pande zote mbili na washirika wao kuendelea kufanya kazi pamoja ili wapate suluhisho la amani,” ilisema taarifa hiyo.

Pia inasema ili uchaguzi uwe wa kuaminika, mchakato wake hauna budi kuziwakilisha pande zote na kuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, mabalozi hao wamesema kulingana na mazingira ya Zanzibar kwa sasa, itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kutegemewa kushiriki kwa namna yoyote katika uchaguzi huo. 

Friday 29 January 2016

#MICHEZO>>>Mbia ajiunga na Gervinho ya huko nchini Uchina.Fahamu zaidi hapa.

 Akiweka record ya Mbia ameichezea timu yake ya taifa ya Cameroon mara 67

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina.

Mbia amekuwa akichezea Trabzonspor ya Uturuki.
Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina.

Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.
Stephane Mbia wakati wa Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 
 
"Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.

Mbia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi."

#YALIYOJIRI>>>CCM Yaipongeza ZEC Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar,Yawataka Wananchi Kujitokeza Kwa Wingi Kupiga Kura.Fahamu zaidi hapa.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.

Kimesema  maamuzi  ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.

Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoshiriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza  kwa wingi wa kura halali.

“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura  Machi 20 mwaka huu.

"Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.

Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango  ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.

“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao,  lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia."

Aidha alisema  chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.

Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika  Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.

Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein

Habari Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 30 iko hapa.


#MICHEZO>>>Alexandre Pato atia wino Chelsea.Fahamu zaidi hapa.

 Chelsea Football Club ni furaha kutangaza mkopo kusainiwa kwa Alexandre Pato kutoka Wakorintho hadi mwisho wa msimu.

Pato, ambaye jina lake kamili ni Alexandre Rodrigues da Silva, ni hodari mbele mchezaji na kugusa bora na kuvutia upande wa kasi.

Pato alisema 'mimi hivyo furaha kutia saini kwa Chelsea. Ni ndoto kwa ajili yangu.
Mimi ni kuangalia mbele kwa mkutano na kupata kujua mpya wachezaji wenzake wangu na hawezi kusubiri kwa kucheza.

'Namshukuru Chelsea kwa msaada wao na matumaini naweza kulipa imani hii kwa klabu na mashabiki wake.'

 Kujitokeza kama moja ya soka duniani hottest mali na wakati Internacional ya Brazil asili yake, Pato chuma hoja kwa mabingwa wa wakati huo wa Ulaya AC Milan katika majira ya 2007.

Yeye flourished katika msimu wake wa kwanza katika Serie A chini ya uongozi wa Carlo Ancelotti na kuendelea kumvutia na maono yake, harakati, na kumaliza kliniki, alifunga mabao 14 katika Rossoneri ya kampeni ya taji la 2010/11.

Pato kushoto Milan katika Januari 2013 baada ya kufunga mabao 63 katika mechi 150.
Alirudi Brazil kucheza kwa Wakorintho na hatimaye starehe na mafanikio kwa mkopo katika mji wao wapinzani Sao Paulo kabla ya kuwa mchezaji wa Chelsea.

Pato imefanya mechi 27 kwa timu yake ya taifa, na kufunga mabao 10, na kuwakilishwa nchi yake katika ngazi ya mwaka 2008 na 2012 Michezo ya Olimpiki.

#MICHEZO>>>Mbwana Samatta akamilisha usajili katika timu mpya.Fahamu zaidi hapa.

 Mbwana Samatta atimae kapata timu mpya baada ya kutoka katika timu ya TP MAZEMBE,akiwa ametoka kwa mafanikio baada ya kuchukua Tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya Afrika.

Haya ni maneno ya Mbwana Samatta ambayo aliyoyaandika katika page yake ya facebook baada kufanyika kwa usajili."Leo nimeingia mkataba rasmi na Club yangu mpya ya FC Genk, mkataba wa miaka minne kucheza katika Ligi kuu ya Ubelgiji. Kama mnavyojua Ubelgiji ndio imekuwa chanzo kikubwa cha wachezaji wengi wakubwa na kikosi chao cha timu ya Taifa ni moja kati ya timu bora duniani. Namshukuru Mungu kwa fursa hii na nitaitumia ipasavyo".

#YALIYOJIRI>>>Umoja wa Vijana Chadema Wampa siku Tatu Rais Magufuli.Fahamu zaidi hapa.

BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

“Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi."

Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima itakuwa na mapungufu yake, tunachohitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii.

TRA Yasitisha Upokeaji Wa Maombi Ya Nafasi Za Kazi.Fahamu zaidi hapa.

ISO 9001:2008 CERTIFIED
KUSITISHWA KWA MUDA UWASILISHWAJI WA MAOMBI YA KAZI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
 
Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
 
Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
 
Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
 
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
 
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
kituo cha huduma kwa wateja- 
08000780078, 0800750075, 0713800333

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu

#YALIYOJIRI>>>>Rais Magufuli Amteua Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
29 Januari, 2016