Tuesday 31 January 2017

Yeleuwiii..Eti Gigy Money Anataka Kuokoka Ila Sio Sasa..!!!..Fahamu zaidi hapa.

MUUZA sura kwenye video za Bongo Fleva ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Choice FM, Gift Stanfod ‘Gigy Money’ hivi karibuni amefunguka kuwa, katika maisha yake, ipo siku ataachana na mambo yote yasiyompendaza Mungu kisha kumtumikia muumba wake.
Akipiga stori mbili tatu na Global Publishers, Gigy aliweka wazi kuwa, katika maisha ya mwanadamu, hasa kijana hukumbana na changamoto nyingi za kimaisha ambazo wakati mwingine humfanya kumkosea muumba wake, lakini inafikia hatua anaamua kuacha kila kitu na kufanya yanayompendeza Mungu.
“Unajua sometimes tunadondoka dhambini, lakini si kwa mapenzi yetu, binafsi ipo siku tu, nitaachana na mambo ya kidunia na kusimama kwa Mungu,” alisema Gigy asiyeishiwa vibwanga.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mzee Mwenye Wake 86 Afariki Dunia..!!.Fahamu zaidi hapa.

NIGERIA: Mzee mmoja(93) aliyekuwa na wake 86 na watoto zaidi ya 170 amefariki dunia kwa maradhi ambayo hayajawekwa wazi.
Mzee huyo ambaye ni Mhubiri wa zamani wa dini ya Kiislamu nchini Nigeria alikuwa akiwaambia Wanawake hao kuwa Mungu alimuagiza kuwaoa.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Hatimaye Serikali Yakiri Bungeni Kuwa Baadhi ya Maeneo Nchini Kuna Njaa.Fahamu zaidi hapa.

Jumla ya tani 35,491 za chakula zinahitajika ili kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula na lishe kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili mwaka huu unaowakabili watu 1,186,028.
Taarifa hiyo ya serikali imetolewa bungeni leo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini huku akisisitiza kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini bado ni wa kuridhisha pamoja na kuwa baadhi ya maeneo yenye upungufu wa chakula.
Tizeba amesema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tathmini ya serikali iliyobaini kupungufu huo katika halmashauri 55 nchi nzima. 
Aidha amesema kuwa jumla ya watu 118,603 wasio na uwezo wa kupata chakula watahitaji tani 3,549 za chakula cha bei nafuu kwa haraka na tayari serikali imeanza kuchukua hatua za kushusha bei ili wananchi waweze kumudu bei zake.
Amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua na mtawanyiko usioridhisha katika maeneo mengi nchini athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na matarajio ya malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula huenda yasifikiwe, uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo utapungua, uwezekano wa kuongezeka kwa bei za baadhi ya mazao ya chakula upo, kupungua kwa mapato yatokanayo na ushuru wa mazao kwa baadhi ya halmashauri.
Athari nyingine ni pamoja na kuongezeka kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kutokana na uhaba wa malisho na maji na uwezekano wa kupungua kwa mapato yatokanayo na mazao ya kilimo yanayouzwa nje ya nchi, uwezekano wa kuwa na maeneo mengi yenye upungufu wa chakula na hivyo kuongezeka kwa kiwango cha utapia mlo.
Dkt.Tizeba amesema kuwa ili kukabiliana na athari za ukame tathmini imebainisha kuwa halmashauri za wilaya hizo 55 zinahitaji jumla ya tani 1,969 za mbegu bora za mahindi, mtama na mizizi inayokomaa kwa muda mfupi na kustahimili ukame na mbegu hizo zinahitajika ziwafikie mwezi Februari mwaka huu ili ziweze kupandwa katika msimu wa mwaka 2016 /2017 katika maeneo yanayoendelea kupata mvua wakati huu wa mwaka.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MwanaHalisi Lamuomba Radhi Rais Magufuli. Lakiri Habari ilikuwa na Makosa.Fahamu zaidi hapa.

MwanaHalisi Lamuomba Radhi Rais Magufuli. Lakiri Habari ilikuwa na Makosa


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

KUONDOKA KWA MJAMAICA PACHA WA SAMATTA, NI NAFASI KWAKE KUJITANGAZA ZAIDI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kama unakumbuka Bailey amekuwa ni pacha wa Mtanzania Mbwana Samatta.

Leverkusen imemwaga dola milioni 21 kumpata mshambuliaji huyo kinda matata wa Genk.
Samatta na Bailey mara kadhaa wamekuwa wakiisaidia Genk kupaa kwa kufunga au kutengeneza mabao muhimu. Kuondoka kwake kunakuwa na faida mbili kwa Samatta.

Kwanza atapata nafasi pana zaidi ya kucheza lakini kwa kuwa Bailey ametokea Genk maana yake timu nyingine za Ujerumani au nje ya Ujerumani, yaani sehemu nyingine barani Ulaya zitatupa jicho katika klabu hiyo.


Samatta ana uwezo mkubwa lakini hakuwa amepata nafasi ya kutosha akiwa Genk. Sasa anaweza kupata nafasi zaidi ili kuonyesha alichonacho na huenda ananukia kwenda mbali zaidi.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Baba Amgeuza Bintiye Mwenye Ulemavu Kuwa Mke, Aanza Kumtesa Baada ya Kumtumia na Kumchoka.Fahamu zaidi hapa.

Habari ya simanzi na kusikitisha wilayani Chunya Mbeya, Baba amemgeuza bintie wa kumzaa mwenye ulemavu kuwa mke. Baada ya kumtumia kwa namna awezavyo, ameanza kumfanyia vitimbi ikiwa ni pamoja na kuanza kumnyanyasa kuashiria kuwa amemchoka.
VIDEO:



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Jamaa Aliyenyang'anywa Demu na Harmo Rapa Ajitokeza na Kulalamika Kupitia Redio.Fahamu zaidi hapa.

Harmo Rapper yule msanii anayejifananisha na Harmonize yadaiwa alimnyanganya Demu presenta na DJ aitwae Msabato na jamaa huyo ameenda studio za EA radio kulalamika na kusema alimnunulia kila kitu na kumpangishia chumba lakini demu huyo ameondoka kwa dharau
Demu mwenyewe jamaa anadai alimtoa Arusha na kumleta Dar kisha kumpangishia chumba na kumpa fedha za saluni na mahitaji mengine
VIDEO:


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Noma Sana..Hili Ndio povu Alilotoa Lulu Baada ya Video Inayomuonyesha Akivunja Amri ya Sita Kusambaa Mitandaoni..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Video ya mtu anayesemekana kuwa ni msanii maarufu wa maigizo nchini, lulu michael, ikimuonyesha msanii huyo akivunja amri ya sita imezagaa mitandaoni. 
Video hyo inasemekana kuwa ya muda, hata hivyo mwenyewe kupitia ukurasa wake wa instagram amekanusha vikali kuwa hyo video sio yake bali ni lulu rappe

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Simu yawagombanisha Vanessa na Jux.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa mara nyingi huwa wanagombana na mpenzi wake huyo Jux kutokana na tabia yake ya kuchelewa kujibu jumbe fupi au hata kupokea simu zake.
 Jux na Vanessa
Vanessa Mdee alisema haya kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai kuwa Jux kwenye suala la simu amekuwa mvivu sana na ndiyo jambo linaloleta tofauti kati yao.

"Mvivu wa simu amefarakanishwa na simu yake huyu jamaa, hata kwenye kujibu txt au kupokea simu hana ushirikiano na simu kabisaa kwa hiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na communication" alisema Vanessa Mdee.

 Chanzo
               eatv


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Sholo Mwamba & Baba Levo unaoitwa "Noma".

Download wimbo wa Sholo Mwamba & Baba Levo-Noma.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Hugo City unaoitwa "Kwako Mama (Wolowolo)".

Download wimbo wa Hugo City-Kwako Mama (Wolowolo).

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Monday 30 January 2017

Download wimbo mpya wa Joslin & Laquisher unaoitwa "Tell Me".

Download wimbo wa Joslin & Laquisher-Tell Me.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#Breaking News>>>Kocha wa Simba Afunguka Mazito Juu ya Hali ya Timu Yake,Awatolea Povu Mashabiki ..!!! .Fahamu zaidi hapa.

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameshusha presha ya mashabiki wa timu hiyo kwa kuwataka kuwa watulivu kwa kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha makosa yao na kutimiza lengo ambalo ni ubingwa.
Simba inashika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Yanga, baada ya Jumamosi kufungwa bao 1-0, na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu, ya Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga imekamata usukani baada ya kuifunga Mwadui ya Shinyanga juzi kwa mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 na kuiondoa Simba kileleni ambayo ina pointi 45 baada ya kipigo cha Jumamosi.
Akizungumza  Omog, ambaye amekuwa katika wakati mgumu kufuatia kipigo hicho alisema hata yeye pamoja na wachezaji wameumizwa na matokeo hayo, lakini mpira ni mchezo wa makosa na kilichobaki kwa sasa ni kujipanga upya ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyokusudia mwishoni mwa msimu huu.
“Hakuna anayependa kufungwa au kutolewa kwenye nafasi nzuri , lakini mashabiki wanapaswa kujua Simba siyo lazima kila siku ishinde ingawa malengo yetu ni ushindi, hivyo inapotokea tumepoteza mchezo kama ilivyotokea Jumamosi tunatakiwa tukubaliane na matokeo alafu tujipange kwa mechi nyingine,” alisema Omog.
Mcameroon huyo alisema, kipindi hiki walichokuwa nacho siyo cha kutupiana lawama bali ni muda wa kuongeza mshikamano na kuisapoti timu yao kwa kuja kwa wingi uwanjani ili kuweza kushinda mechi zao na kuitoa

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Trump Amtimua Kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali Baada ya Kupinga agizo lake la Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekanii.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
 
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
 
Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
 
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.
 
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kwa Faida Yako:Kutafuna Bigijii kwa Muda Mrefu Kunaweza Kukusababishia Vidonda vya Tumbo..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Kuna athari kubwa sana zinazotokana na utafunaji wa bigijii (chewing gums) kwa muda mrefu
Utafunaji huo husababisha tumbo kuzalisha acid ya kutosha likifikiri kuna chakula ambacho kinatafunwa tayari kumezwa. Kitendo cha kutafuna bigijii husisimua seli linazozunguka ukuta wa ndani wa tumbo kutengeneza juisi (digestive juice) ambayo husaidia kwenye mmeng’enyo wa chakula.
Hii ni njia asilia ambayo husababisha chakula ambacho kimetafunwa kuanza kumeng’enywa punde tu kinapofika tumboni. Kwahiyo utafunaji wa bigijii (chewing gums) husababisha uzalishaji wa aside isiyo na ulazima. Hii ni habari nmbaya kwa walaji wa bigijii kwani aside hii huongeza athari za kupata vidonda vya tumbo.
Lakini risk ni ndogo sana labda uwe unatafuna bigijii (chewing gums) nyingi sana kwa siku, kwahiyo ondoa hofu labda uwe kocha wa mpira wa miguu (football coach).

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

DIMITRI PAYET JEURI SANA, AKAMILISHA DILI LA UHAMISHO, AWATOLEA KAULI WEST HAM.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Dimitri Payet ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Marseille ya Ufaransa akitokea West Ham United ya England kwa ada ya pauni 25m lakini kuna neno ametoa kuhusu timu yake ya zamani.
Payet ambaye alitolewa lugha nyingi kali na mashabiki wa West Ham walimuona kama msaliti kwa kugoma kucheza akitaka auzwe amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu yake hiyo ya nyumbani na kuamua kuzungumzia kilichotokea.

 Akizungumzia kuhusu tabia yake iliyojitokea mpaka dili hilo linakamilika, Payet amesema: "Sina haja ya kuthibitisha au kufafanua kuhusu tabia yangu. Slaven Bilic (kocha wa West Ham) tulizungumza na tunajua kilichotokea.

“Sina cha ziada kuzungumzia kuhusu suala hilo, naona bora nitahifadhi hayo, nitayazungumza siku nyingine lakini siyo sasa, kwa ufupi nilihitaji sana kurejea Ufaransa hasa Marseille."



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Rais wa Guinea achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika (AU).Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais Conde anapokea uongozi kwa Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ni kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the Union). Mwenyekiti huyu huchaguliwa  na Marais wa Nchi wanachama wa AU ambaye hushika wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa zamu katika Kanda tano za bara la Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, na Afrika ya Kati).
Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002 ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza.
Rais wa Chad,  Idriss Deby (kushoto) akikabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Alpha Conde wa Guinea (kulia).

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Njaa na Deni la Tiafa Kutikisa Bunge Kesho..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.
Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.
Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-

KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-
    Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
    Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
    Mhe. Anne Kilango Malecela
    Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)
MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi. 

KAULI ZA MAWAZIRI
Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa  kama ifuatavyo:-
Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
MISWADA YA SHERIA
Katika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...
Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Picha: Meli kubwa ya kisasa ya Azam yatia nanga Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza.Fahamu zaidi hapa.

Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga
Bandari ya Tanga leo.

Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

SIMU INAWEZA KUMTIA PAUL POGBA MATATANI, USHAHIDI HUU HAPA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kiungo wa bei kubwa wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kuingia matatani baada ya kuonekana akiendesha gari huku akitumia simu kitu ambacho ni kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini England.

Pogba ameonekana akiendesha gari lake aina ya ua Audi RS6-R lenye thamani ya pauni 85,000 alipokuwa akiwasili mazoezini kwenye Uwanja wa Carrington, Ijumaa iliyopita.

Picha zimemuonyesha akiwa ameishika simu yake hiyo huku akiendesha gari na kama mamlaka husika za usalama barabarani zitaamua kutumia picha hiyo zinaweza kumuingiza matatizoni.
 
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mangwea Awatokea Cpwaa na Noorah,Wafunguka Alichowaambia ..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Ikiwa sasa ni miaka minne na miezi kadhaa imepita tangu Rapa Albert Mangwea kufariki dunia, wasanii Noorah pamoja na Cpwaa kwa pamoja wamejikuta wakifanya mpango wa kuingia studio na kurudi na nguvu mpya wakidai kuwa ni maagizo aliyowapa ndotoni.
Hatua hiyo ni baada ya wakali hao kwa muda tofauti kumuota rappa huyo na kuamini kuwa huenda alikuwa anawakumbusha kuwa wanapaswa kurudi kwenye muziki na kumuenzi kwa kufanya kazi ya pamoja.
Alianza rapa Noorah kwa kupost picha ya Albert Mangwea na kusema alimuota na jinsi alivyokuwa wakizungumza ni kama alikuwa hai na kitendo kilichomfanya Noorah atamani kuona ile ndoto kama ingekuwa ndiyo uhalisia lakini haikuweza kuwa kwa kuwa ni ndoto tu.
"Nimekuota usiku wa leo (jana) mshkaji wangu. Ilikuwa 'too realistic' kama vile bado upo hai. R.I.P ndugu yangu" aliandika Noorah 
Baada ya hapo aliibuka Cpwaa na kudai hata yeye amemuota Albert Mangwea juzi hivyo ni kama rapa huyo anaongea nao, hivyo Cpwaa alimuomba Noorah warudi kwenye muziki kwani game ni kama imemiss sana ladha zao, hivyo Noorah alisema haina tatizo japo kwa muda huu bado anafanya matibabu kutokana na tatizo lake la kichwa, ila aliahidi kuwa atapita kwa Cpwaa ili wamalize kesi hiyo. 
"Bro huwezi amini I did as well jana! Daah bro is talking to us. Come back my brother game ime miss ladha zetu Babastylz jana nime request sana ngoma za Ngwea kiwanja flani" alisema Cpwaa.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Hatimaye Njia Ya Reli Kati Ya Dar Es Salaam Na Ruvu Yafunguliwa.Fahamu zaidi hapa.

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9 alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli.

Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali  kutoka relini na pia kuikarabati sehemu iliyoharibika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.

Aidha treni ya abiria iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara..

Wakati huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi. Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo.

Taarifa kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefahamika kuwa ni Nd. Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa tumbo.

Mgonjwa wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi.

Kuhusu idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya 1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480.

Aidha imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa. Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 30, 2017
DAR ES SALAAM

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Sunday 29 January 2017

#Breaking News>>>>Treni ya abiria inayofanya safari zake kutoka Dar-Kigoma lapata ajali hivi punde.Fahamu zaidi hapa.

Inaelezwa kuwa Treni ya abiria inayofanya safari zake kutoka Dar-Kigoma almaarufu DElux.


imepata ajali hivi punde maeneo ya Ruvu mkoa wa Pwani, ikitokea Kigoma kuja Dar,Hivyo kama una ndugu,jamaa au rafiki aliekuwa akisafiri leo.

Poleni sana kwa mliopata ajali. 

Kwa habari zaidi endelea kufatilia hii blog"www.hebronmalele.blogspot.com"


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

DARASSA AACHA GUMZO KIGOMA,WANA KIGOMA WAFUNGUKA JINSI WANAVYOMKUBALI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Darasa got a Bless from an old Women Fancy from Kigoma.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

LWANDAMINA ASHITUKIA PRESHA YA KUKAA KILELENI, AWAPA SOMO WACHEZAJI KABLA YA MWADUI LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kocha George Lwandamina amewata wachezaji wake kuondoa presha ya kuwaza kurejea kileleni na badala yake wacheze kwa lengo la kuishinda Mwadui FC, leo.


Yanga inakutana na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Iwapo Yanga itashinda, basi itapaa hadi kileleni ikiwa na pointi 46 na kuiacha Simba yenye 45 kileleni hadi sasa.
“Kocha kasisitiza suala la pointi tatu na si kuwenda kileleni. Ametuambia tunachotakiwa kufanya ni ushindi  kwa lengo la kupata pointi tatu.

“Ametukataza suala la kufikiria kukaa kileleni kwa kuwa linaweza kutupa presha na kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Mwadui FC,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga ambaye sasa ni tegemeo.


Imeelezwa Lwandamina anayesifika kwa uwezo mkubwa wa masuala ya saikolojia kwa wachezaji amegundua kuna presha kubwa ya wachezaji kuhusiana na kukaa kileleni na kuipita Simba.


Simba imebaki pengo la pointi mbili tu kati yake na Yanga baada ya jana kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC. 


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

HAKIKA VIDEO YA MADEE NI MBAYA…HATIMAYE YAFUTWA YOUTUBE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

HAKIKA VIDEO YA HELA ALIYO TOA MADEE NI MBAYA SANA KULINGANA NA HADHI YAKE KWA SASA NA VIDEO KALI ZINAZO TENGENEZWA KWA KIPINDI HIKI

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MANE AIMWAGA SENEGAL NJE YA AFCON, AKOSA PENALTI YA MWISHO, CAMEROON YASONGA NUSU FAINALI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Senegal iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Afcon, imetolewa katika hatua ya robo fainali na Simba Wasioshindika, Cameroon wamesonga mbele.

Cameroon wamesonga mbele baada ya ushindi wa penalti 5-4, penalti ya mwisho ya Senegal ilipotelea kwa nyota wake Sadio Mane anayekipiga katika kikosi cha Liverpool nchini England.

Kwa Liverpool itakuwa furaha kuu maana bila Sane mambo yalionekana yanakwenda kombo. Lakini kwa Wasenegali ni majonzi makubwa wakiwa wanaenda nyumbani.

Katika mechi hiyo, dakika 90 halafu 120 ziliisha kwa sare ya bila mabao huku Senegal ikiwa imepoteza nafasi nyingi za kufunga.

 PENALTI ZILIVYOKUWA
SENEGAL
Koulibaly - FUNGA
Kara - FUNGA
Sow -FUNGA
Saivet - FUNGA
Mane - KOSA 


CAMEROON
Moukandjo - FUNGA
Oyongo - FUNGA
Teikeu - FUNGA
Zoua - FUNGA
Aboubakar - FUNGA
Senegal (4-3-3): Diallo; Gassama, Kara, Koulibaly, M'Bengue (Ciss 86mins); Gueye, Saivet, Kouyate (Ndiaye 109); Mane, Diouf (Sow 64), Keita.
Booked: Diouf, Kouyate.


Cameroon (4-3-3): Ondoa; Fai, Teikeu, Ngadeu-Ngadjui, Oyongo; Siani, Moukandjo, Djoum (Mandjeck 102); Bassogog, Tambe (Aboubakar 102), Ekambi (Zoua 46).

Booked: Oynogo, Fai, Djoum.
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa