Monday 23 January 2017

Tobaah..!! Nay wa Mitego Afunguka Juu ya Bifu na Mama Yake Mzazi,Adai Kuwa Hajaongea Naye kwa Miaka Mitano..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Rapa Nay wa Mitego ambaye anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi' amefunguka na kusema kuwa ni kweli alikuwa amezinguana na mama yake mzazi na walikaa miaka mitano bila kupiga stori yoyote ile. 
Nay wa Mitego alisema haya kupitia kipindi cha Planet bongo na kusema kwa sasa wameshamaliza tofauti zao na anaishi na mama yake mzazi ingawa anakiri kuwa ni kweli ameishi zaidi ya miaka mitano bila kuongea na mama yake mzazi.

"Mimi na mama mzazi tuko poa sana na nina kaa naye this time, ni kweli kabisa tumekaa miaka mitano bila kuzungumza jambo lolote lile ila ni mazingira ya maisha ya mtaa niliyokuwa naishi lakini mpka muda huu tunaongea mimi naishi na mama yangu nyumbani kwangu, hivyo niko naye nyumbani" alisema Nay wa Mitego 

Mbali na hilo Nay wa Mitego anasema yeye haamini katika dini kwani anaona dini nyingi saizi zimekuwa biashara, hivyo yeye anamini Mungu na anajua Mungu yuko kila sehemu si lazima iwe kanisani.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment