Wednesday 31 January 2018

TCRA Yafafanua Matuzi ya Alama za Vidole Kwenye Usajili wa Laini.

“Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,” ni ujumbe ambao watumiaji mbalimbali wa mitandao ya simu nchi wametumiwa kuanzia juzi kutoka katika mitandao yao.

Kuhusu ujumbe huo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa imetoa kibali kwa makampuni ya simy nchini upya kadi za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala na kuwatoa hofu wananchi kwamba tayari walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.

Alisema kuwa, mfumo huo unatumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.

“Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi.”

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mzee Majuto Baada ya Kutembelewa Hospitalini na Rais Magufuli.

Jumatano ya January 31 2018 Rais John Pombe Magufuli alimtembelea hospitalini muigizaji mzee Majuto, ambaye amelazwa hospitali ya Tumaini Up

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Rosa ree Afunguka "Sina Mahusiano ya Kimapenzi na Young Dee".

Rosa ree Amkana Young Dee Amchana Kweupe "Sina mahusiano ya kimapenzi na Young Dee" Tazama Video Hapa chini:
 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hii Ndio Gharama ya Passport za Kielektroniki.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000.

Dk Nchemba amesema hayo leo  wakati wa uzinduzi wa Hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam ambapo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha Dkt. Miwgulu Nchemba amesema kuwa Pasipoti hizo zitakuwa na ukurasa zaidi ya mmoja  na mwonekano mpya.

“kiasi cha gharama hiyo  ni sawa na Sh15,000 kwa mwaka kwa sababu itatumika kwa miaka 10. Gharama za kupata pasipoti sasa ni TSh.50,000 na hutumika kwa miaka 10 tangu zilipotolewa,“ amesema Dkt. Mwigulu.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa gharama ya laki moja na nusu bei hiyo ni ya juu kidogo kuliko bei ya sasa . huku kieleza kuwa bei hiyo imezingatia ubora wa utenngenezaji wa Pasipoti hiyo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Aunt Ezekieli, Tunda na Iyobo Kimenuka Wamwagiana Mvua ya Matusi Mitandaoni.

Moja kati ya stories zinazotrend katika mitandao ya kijamii leo Jumanne ya January 30 2018 ni post ya Tunda ambapo alipost picha yake katika ukurasa wake wa instagram na baadae Aunt Ezekiel kumjibu kwa kucomment.
“Afu na wewe Mose kweli unakaa chini unaandika upuuzi kama huo kama kweli ni wewe umeandika basi huna uso wa haya!….inawezekana pia Aunt ndo umejiandikilisha🤣ivi wewe Moze huna haya NAKUULIZA SWALI MOJA TU KWANINI ULINIBLOCK KUPIGA KIPINDI ANT AMEANZA KUNIULIZA KUHUSU HELA KWANINI YANI UNIBLOCK”-Tunda

“KWANINI HUKUTAKA NIKUULIZE IMEKUAJE HELA HAIJAFIKA DUKANI SIKIENI NYIE NITOLEENI UJINGA WENU HAPA WATU WAZIMA MLIOKOSA BUSARA NA AKILI YANI KABISA MIMI NIGOMBANE NA WEWE KISA LAKI KWELI HATA KAMA NINGEKUA SINA HELA SIWEZI KOSA LAKI YA KULIPA KWA HIYO MSITAFUTE STORY”-Tunda

“MMEMISI KUWEKWA FRONTPAGE KWENYE MAGAZETI MSINILETEE WAZIMU WENU AFU NINA SWALI KWANINI VIBENTEN VINAKUAGA NA MKONO MREFU YANI KABISA MOZE UMEONA NI BORA WATU WAGOMBANE KULIKO KUSEMA HELA ULICHUKUA KWA MATUMIZI MENGINE SHOGA WEWE !..Unantaka sio bure sina desturi ya kutembea na madancer🤪”-Tunda

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa.

DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hizi Ndivyo Wema, Mobetto na Tunda Wanavyozungukana kwenye Penzi la Diamond.

Mambo ni moto! Habari ya mjini inayotrendi ni kitendo cha staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kuonekana akioneshana mahaba shatashata na zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambacho kimeamsha ‘vilivyolala’.

Wema na Diamond ‘walifanya yao’ wikiendi iliyopita kwenye ‘iventi’ ya Wasafi Classic Baby (WCB) kumsaini msanii mpya katika lebo yao, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Marombosso au ‘Mbosso’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nyota Tano ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar kisha kujiachia kwenda kwenye Klabu ya Maisha Basement, Kijitonyama, usiku huohuo.

Kufuatia tukio hilo, wakali wa ubuyu walilidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na skendo ya mastaa wa kike, Wema, Video Queens, Tunda Sebastian na Hamisa Mobeto kudaiwa kuzungukana kwa jamaa huyo.

Chanzo makini kilimwaga ubuyu kuwa, kabla ya Mobeto kutangaza kubeba ujauzito wa Diamond kisha kujifungua mtoto wa kiume, Prince Dully kulikuwa na ‘unyunyuz’ kuwa, Wema alikuwa akionekana nyumbani kwa jamaa huyo, Madale-Tegeta, Dar.


Mobeto.



Hata hivyo, Wema na Diamond ambao walikuwa wapenzi wa kukata na shoka kabla ya kumwagana, walikanusha kwa nguvu zote kuwa hawakuwa wamerudiana.

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, jambo hilo lilisababisha kuwepo kwa msuguano mkali kati ya Wema na mzazi mwenza wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

MOBETO

Msuguano huo ulimalizwa na skendo ya Diamond kuzaa na Mobeto ambapo sasa Zari na timu yake waliachana na Wema na kuhamishia mashambulizi kwa Mobeto.

Katika maelezo yake, Diamond alikiri kumsaliti Zari na kuzaa na Mobeto.

TUNDA

Ilisemekana kuwa, wakati mambo yakiwa ni moto kati ya Mobeto na Zari, ghafla upepo ulibadilika baada ya kuibuka kwa skendo mpya kuwa, Tunda naye anatoka na Diamond.


Tunda



Ilidaiwa kuwa, kwa nyakati tofauti, Tunda alionekana nyumbani kwa Diamond, Madale-Tegeta, Dar na kujiachia na jamaa huyo kwenye klabu mbalimbali za usiku ikiwepo Elements iliyopo Masaki, Dar.

“Kama hiyo haitoshi, mambo yalipamba moto zaidi baada ya kuwepo kwa ubuyu kuwa Tunda naye ana mimba ya Diamond,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina.

Alipobanwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda juu ya kuwa na uhusiano na kubeba mimba ya Diamond, Tunda alidai kuwa jamaa huyo ni sawa na kaka yake, lakini akakiri kuwa na mimba.

WEMA

Katika tukio la wikiendi iliyopita, Wema alibanwa na Global TV Online juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo alisema: “Utoto umekwisha, tunasapotiana na hatutaacha kufanya hivyo. Najua watu wanasema kwa sababu ‘kapo’ yetu ilikuwa gumzo mno kwa mashabiki wetu.”


DIAMOND

Kwa upande wake Diamond, alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Wema na kwamba ilikuwaje hadi akamwalika kwenye tukio hilo alisema:

“Mimi ndiye niliyempigia simu nikamuomba aje kwenye iventi yetu na amekuja, hakuna ubaya, amekuja kutusapoti, kunakuwa na mambo mengi kwa sababu tulikuwa wapenzi zamani, lakini kwa sasa tunapeana sapoti ya kazi zetu tu.”

Kuhusu Tunda na Mobeto, Diamond alisema: “Kuhusu Tunda…yupo hapa, niliwaalika wote, nimemuona yumo…oya Tunda hebu njoo (akapotezea).

“Hivi ina maana kila mtoto mzuri mimi nina…(akimaanisha anakuwa naye kimapenzi), si kweli…”

“Kuhusu Mobeto, kama nilivyosema, niliwaalika wote , lakini hajafika.”

KIFUATACHO…

Kufuatia kilichojiri kati ya Diamond na Wema kisha kusambaa kwa picha za video na mnato, wafuatiliaji wa mambo ya ubuyu wanadai kuwa, kwa vyovyote Wema atakuwa amemtibua upya Zari hivyo anatarajiwa kujibu mapigo muda wowote.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha.

MUDA mchache baada ya kushuhudia timu yake ikipata bao la pekee katika dakika za nyongeza dhidi ya Tanzania Prisons juzi, Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, alijikuta akiingizwa mjini na vibaka kwa kuibiwa mkoba wa fedha wakati akishangilia bao hilo.

Pluijim aliibiwa mkoba huo uliokuwa na simu aina ya Sumsung Pro 9 yenye thamani ya Sh. 1,575,700,  pochi ('wallet'), leseni ya udereva kwa nchi mbili Tanzania na Ghana, fedha za Dola 100 za Marekani, fedha taslimu Sh. 200,000 za Tanzania na funguo za gari lake aina ya Prado.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi, alisema baada ya ushindi huo, mashabiki walishangilia sana kiasi cha mhalifu kutumia mwanya huo kuiba mkoba wa kocha huyo hivyo kulazimika kuripoti polisi na msako mkali kuanza.

Askari wakiongozwa na taarifa za kitengo cha makosa ya mtandao kwa kutumia namba ya simu ya Pluijim iliyokuwamo kwenye mkoba, walifanikiwa kupata begi hilo likiwa limetupwa eneo la mtaa wa Kindai baada ya mwizi kubaini anafuatiliwa na polisi.

Mbughi alisema kweye mkoba huo polisi walifanikiwa kukuta vitu vyote isipokuwa fedha ambazo mwizi alitoweka nazo.

Pluijim alipatiwa vitu vyake vyote isipokuwa fedha, lakini amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako kumbaini aliyehusika na uhalifu huo.

Aidha, jeshi hilo limetahadharisha wapenzi na mashabiki wa soka kujihadhari dhidi ya wezi wanaoingia uwanjani kwa nia mbaya huku wakikusudia kufanya uhalifu wakati wa kushangilia ushindi au bao linapofungwa.

Katika mchezo huo Singida United ilipata bao pekee dakika sita za nyongeza kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Elinywesia Sumbi, ‘Msingida’ aliyeingia uwanjani dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

 Chanzo Nipashe

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kuolewa Mke wa Pili si Dhambi- Tausi Mdegela.

KOMEDIANI matata wa Bongo Movies, Tausi Mdegela amefunguka kuwa, ikitokea akapata mwanaume wa kumuoa, hata kama ana mke haina shida kuolewa mke mwenza au wa pili kwani kama ni Muislam, dini inaruhusu.


Tausi alifunguka hayo juzikati baada ya kuzagaa kwa habari kwamba anatarajia kuolewa na mwanamuziki wa Taarab, Prince Amigo na kueleza kuwa, siyo kweli, bali ilikuwa ni kava la wimbo wake, lakini ikitokea amepata mwanaume, yupo tayari kuolewa mke wa pili.

“Kuolewa mke wa pili siyo dhambi, ikitokea nimepata wa kunioa, hata kama ni mke wa pili, sioni shida ilimradi awe Muislam kwa kuwa dini inamruhusu,” alisema Tausi.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kimenuka Kenya...Raila Odinga Hatarini Kushtakiwa kwa Uhaini.

MAMLAKA za Kenya, jana zilizima vituo vya televisheni kuzuia matangazo 'live' ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa mwaka jana uliobishaniwa.

Alijitangaza kuwa "rais wa watu" mbele ya maelfu ya wafuasi wake katika mji mkuu wa Nairobi.

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti, mwaka jana, yalibatilishwa kutokana na  madai ya ukiukwaji wa kanuni.

Uhuru Kenyatta alishinda uchaguzi wa marudio Oktoba, lakini Odinga hakushiriki, hivyo Kenyatta aliapishwa kuongoza muhula wa pili Novemba, mwaka jana.

Alivionya vyombo vya habari kutotangaza shughuli ya jana na mwanasheria wa serikali alisema kufanya hafla hiyo ni kosa la uhaini.

Hata hivyo, vituo vikuu vya TV vilionyesha tukio hilo kupitia mitandao yake ya kompyuta, kwenye YouTube na Facebook.

Akiwa ameshika Biblia mkono wake wa kulia katika bustani ya jijini Nairobi, Odinga alitangaza kuwa anajibu "wito wa ngazi ya juu kuchukua ofisi ya rais wa watu wa Jamhuri ya Kenya."

Watu wamechoshwa na wizi wa kura katika uchaguzi na tukio hilo lilikuwa hatua kuelekea ujenzi wa demokrasia sahihi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, Odinga aliuambia umati uliokuwa ukishangilia.

Aliyekuwa mgombea mwenza wake, Kalonzo Musyoka, hakuwapo kwenye hafla hiyo. Odinga alisema ataapishwa siku nyingine.

Akizungumza awali na televisheni ya Kenya ya KTN, Odinga alisema kufungwa kwa vyombo vya habari "kumethibitisha kuwa tumeporomoka kufikia kiwango cha Uganda", ambayo ilisimamisha matangazo ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi mwaka 2016.

"Kuapishwa kwake" kulikuwa na lengo la "kuonyesha dunia kuwa tunachofanya ni halali kisheria, kikatiba na kitu ambacho huwezi kukielezea hata kidogo kuwa mapinduzi", alisema zaidi.

Vituo vitatu binafsi vya televisheni - NTV, KTN na Citizen TV - vilizima matangazo kuanzia saa 3:10 asubuhi.

Citizen TV iliiambia BBC kuwa mamlaka za serikali ziliwalazimisha kuzima matangazo kutokana na mipango ya kuonyesha mkusanyiko huo.

Watazamaji wa KTN walishuhudia vioo vya luninga zao vikishika rangi nyeusi wakati mtangazaji akisoma taarifa kutihibitisha kuwa mamlaka ya mawasiliano ilikuwa ikizima matangazo.

Kuzimwa kwa 'signo' ya matangazo ya vyombo vya habari si jambo la kawaida hapa Kenya.

Palikuwa na wasiwasi jana huku baadhi ya shule katika mji mkuu wa Kenya zikifungwa kwa sababu ya tukio hilo, na watu kutojua nini kingetokea.

Polisi awali walizingira viwanja hivyo, lakini baadaye wakaondoka.

Chanzo: BBC

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Maskini...Familia Yahofia Tundu Lissu Kufukuzwa Hospitali.

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.

Lissu amelazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Luvein nchini Ubelgiji tangu mapema mwezi huu baada ya kutibiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa miezi minne.

Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa miezi ni mitano sasa Lissu hajapata stahiki zake kimatibabu kama Mbunge.

“Tumemaliza miezi mitano tangu kutokea kwa tukio la kushambuliwa kwa Lissu na Bunge kama taasisi limeshindwa kutoa fedha za matibabu kwa mwenzao," alisema Mughwai.

“Sasa Lissu atalaumiwaje? Akilia Mungu wangu mbona umeniacha, Bunge langu mbona limeniacha... au wanataka afukuzwe hapo hospitalini kwa kukosa fedha za matibabu?

“Mpaka sasa hatujui kinachoendelea. Tunaweza kusema ni siasa au kwa namna nyingine tunaweza kutafsiri kuwa sababu Lissu ni mkosoaji mzuri wa serikali bungeni.

“Waheshimiwa hawa wanataka mwenzao kuwa kilema au kupoteza maisha? Cha msingi wanapaswa kutoa haki za msingi ambazo sisi tumeona zinacheleweshwa kwa makusudi.”

Bunge lilishasema hata hivyo kwamba Lissu alifuata matibabu nje ya nchi kinyume na utaratibu wa bima ya afya ya wabunge, hivyo kuwa kikwazo cha kuhudumiwa kwake.

Lissu (49) alipigwa risasi tano na watu wasiojulikana akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba 7, mwaka jana. Jumla ya risasi 32 zilirushwa na watu hao kwa mujibu wa taarifa za Bunge.

Akizungumzia mawasiliano ya familia na ofisi ya Bunge, alisema Desemba 15, mwaka jana, alitoa mrejesho kwa vyombo vya habari kuhusu barua waliyoandikiwa na Katibu wa Bunge ikiwataka familia hiyo kutoa ufafanuzi wa haki zipi ambazo Lissu anatakiwa kupewa na Bunge.

Alisema waliandika barua ya kuomba ufafanuzi huo, Desemba 13, mwaka jana, na barua hiyo ilipokelewa na Ofisi ya Bunge Desemba 18, mwaka jana na ilipokelewa kwa njia ya barua za haraka ya DHL.

“Tulichoomba ufafanuzi ni kuhusu fedha za matibabu, stahiki za usafiri wa kwenda nje ya nchi pamoja na posho ya kujikimu kwa yule anayemuangalia hospitalini," alisema.

“Bunge ilitoa majibu Desemba 10, mwaka jana, kupitia kwa Katibu wa Bunge ambapo alidai kuwa barua hiyo iliwaelekeza kurudia utaratibu wa kufuata utaratibu ambao bunge linatumia kwa ajili ya matibabu ya wabunge pindi wabunge wanapokwenda kupewa matibabu,” alisema.

Aidha alisema baada ya kurudia kufanya marekebisho ya barua hiyo, Katibu wa Bunge aliwajibu Januari 10, mwaka huu, kuwa Wizara ya Afya imeunda timu ya madaktari bingwa kwenda Nairobi kumuangalia Lissu wakati wakitambua kuwa mbunge huyo Januari 6, mwaka huu, alishasafirishwa kwenda nje ya Afrika kwa ajili ya matibabu.

Akizungumzia afya ya Lissu, Mughwai alisema kwa sasa anaendelea vizuri na mazoezi ya viungo, ili kuimarisha afya yake.

Alisema aliwasiliana na Lissu Jumapili ambapo alimweleza anaendelea vizuri na mazoezi akiwa anafanya mara tatu kwa siku.

Alisema mazoezi anayofanyishwa kwa sasa ni kupanda ngazi sita na kuvuta vitu vizito.

Aidha alidai kwa mguu ambao ulipata majeraha makubwa unaweza kustahimili kusukuma kitu chenye uzito kwa kilo 25 na kwamba mazoezi yataendelea hadi hapo atakapo kuwa vyema kiafya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Rais Magufuli Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki.

Jonas Kamaleki- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo  atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, 2018 kuanzia saa moja na nusu asubuhi, Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Dar es salaam.

Hayo yalisemwa na Mrakibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO).

Mtanda alisema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali mbali na manejimenti mipakani.

Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti.

Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa mujibu wa Mtanda.

Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao. Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi mbali mbali.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

TID: Kuwa Karibu na Makonda Kumenifanya Nikose Show.

Msanii wa muziki, TID amelalamika kuwa baadhi ya watu wanamfanyia figisu figisu ili asipate show kutokana na ukaribu wake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Muimbaji huyo amefunguka hayo katika kipindi cha Eight cha TVE kwa kudai kuwa hali hiyo inampa tabu sana.

“Kuna watu wananibania kupata dili, wengine wanaenda mpaka kwa waandaaji sipati show. Napata dabu kweli,” amesema TID.

TID ameongeza kuwa Mhe. Makonda ni mtu ambaye yuko poa sana na watu na kila anachokifanya anakuwa na uhakika nacho.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday 30 January 2018

Zitto Ataja List ya Viongozi Ambao Atawateua Ikitokea Amekuwa Rais wa TZ.

Mchana wa leo January 30, 2018 kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika watu ambao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali za serikali kama atakuwa Rais wa Tanzania.

Ameandika kuwa atamchagua Mwanaharakati Maria Tsehai Sarungi kuwa Balozi wa Umoja wa Taifa huku Kaimu wake akiwa Mwanzilishi wa Nyama Choma Festival Carol Ndosi.

Amewataja pia Mbunge wa  Arumeru Mashariki Joshua Nassari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu kuwa atawachagua kuwa Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ulinzi wa Jamii na Biashara za Umma).

Zitto pia amewataja Mbunge wa Tarime Esther Matiko kuwa Waziri wa TAMISEMI, na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) mkoa wa Geita Upendo Peneza kushika nafasi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hata hivyo Zitto ameongeza kuwa ambaye atamteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hamtaji jina lakini yeye mwenyewe anajijua. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Raila Odinga Apuuza Kauli ya Serikali...Adai Kuapishwa Kwake ni Alali.

Kiongozi wa Muungano wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amejitokeza katika viwanja vya Uhuru na kuapishwa kama Rais wa Watu wa Kenya.
-
Viongozi wengine wa Muungano huo, wakiwemo Kalonzo Musyoka, amabye ndiye alitarajiwa kuapa kama Makamu wake, Musalia Mudavadi na Moses Wetang'ula hawakuepo katika tukio hilo lililochukua chini ya dakika 10.
-
Kiongozi huyo alipuuza madai sherehe hizo za kuapishwa ni jaribio la kuipindua serikali na kuongeza upinzani utauonyesha Ulimwengu kuwa kuapishwa huko ni sahihi kisheria

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama.

Matokeo ya kidato cha nne yametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa Necta,  Dk Charles Msonde

==>Yatazame hapo chini


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday 25 January 2018

Hali si shwari Soka la Majirani Zetu Kenya.

Hali si hali nchini Kenya, rais wa shirikisho la soka nchini humo Nick Mwendwa amesema kujiondoka kwa baadhi ya wadhamini waliokuwa wakidhamini shirikisho hilo pamoja na michezo ya ligi kuu kumelifanya soka la nchi hiyo kuanza kuyumba na wasiwasi umetanga kwamba huenda ligi ikasuasua lakini huenda timu ya taifa ikatetereka kwa sababu kama ligi haitochezwa kwa ushindani uliokusudiwa moja kwa moja timu ya taifa itaathirika.

Changamoto hiyo imekwenda mbali kidogo kwa sababu wadhamini wakubwa ambao walikuwa wakitoa kiasi kikubwa cha fedha katika soka la Kenya, kuondoka kwao pia kunaweza kufanya soka likadidimia.

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Nation David Kalimwa amezungumzia hali ya mchezo wa soka nchini Kenya baada ya kuondokewa na udhamini wa baadhi ya makampuni.

“Hali ya sintofahamu imelikumba soka la Kenya baada ya kuondokewa na wadhamini wakubwa Sport Pesa kujiondoa katika udhamini pamoja na mashirika mbalimbali ikiwamo vilabu vikuu hapa nchini Kenya AFC Leopard na Gor Mahia pamoja na klabu ya daraja la pili Nakuru All Stars na shirikisho la soka la Kenya Football Kenya Federation (FKF) na wasimamizi wa ligi kuu ya Kenya ambao wote walikuwa wananufaika kwa udhamini wa takribani dola milioni sita za Marekani kwa mwaka sawa na shilingi milioni 600 za Kenya.”

“Sport Pesa wamejiondoka kwenye udhamini kwa sababu serikali ya Kenya imeongeza kodi kwa makampuni yote ya betting, kujitoa kwa Sport Pesa kumeleta shida mbalimbali ambapo wasimamizi wengi wa soka hapa nchini wamesema labda hakuta kuwa na maendeleo ya michezo lakini rais wa FKF Nick Mwendwa ambaye alidai wanafanya mazungumzo na serikali kuona kama itaweza kudhamini michezo hiyo ya ligi bada ya Sport Pesa kujiondoa.”

“Kampuni ya Sport Pesa pia ilikuwa ikilipa mshahara wa kocha mkuu wa Kenya pamoja na mkurugenzi wa ufundi wa FKF kwa hiyo kujiondoa kwa Sport Pesa kunaweza kufanya wawili hao kukosa mishahara.”

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Baada ya Kubwagwa na Heri Muziki Diva Anyapia Penzi la Soudy Brown.

Baada ya kubwagana na mpenzi wake Heri Muziki, Diva amefunguka mipango yake ya kuwa na Soudy Brown.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm amesema kwa sasa yupo tayari kubadili dini kwa ajili ya Soudy Brown ambaye ni mtangazaji mwenzake katika kituo hicho.

“Soudy Brown ndio kila kitu kwangu niseme hivyo, urafiki wangu uko karibu kupita kiasi like hakuna kama Soudy I think he my only true love,” Diva ameiambia Bongo5.

“Kwa sababu yeye ni mtoto wa kislam akiniongeza kwenye list nitabadilisha dini na nitaitwa Amina,” amesisitiza.

Hata hivyo ameongeza kuwa tayari anamjua mpenzi wake Soudy Brown ila kitu ambacho watakaa na kujadili. Diva kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Waambie’ ambao amewashirikisha  Mr. Paul na Mwana FA.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tundu Lissu: Nimemtolewa Risasi Nyingine Mwilini.

Siku 35 baada ya Tundu Lissu kusema mwili wake bado una risasi moja baada ya kutolewa nyingine 15, jana mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) amelieleza Mwananchi kuwa madaktari wamemtoa kipande cha risasi kilichokuwa mwilini mwake.

Hata hivyo, mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari lililokuwa nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7 mwaka jana, alisema chuma hicho ni tofauti na risasi iliyonayo mwilini, ambayo alielezwa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi, Kenya kuwa iko sehemu mbaya, lakini isipotolewa haiwezi kumdhuru.

“Leo (jana) madaktari wamenitoa kipande cha chuma katika sehemu ya makalio ambacho nilipokuwa Nairobi (Kenya) madaktari walikiona lakini kilikuwa ndani ya nyama wakashindwa kukitoa,” alisema Lissu kwa njia ya simu kutoka Ubelgiji ambako alipelekwa Januari 7 kwa ajili ya tiba ya mazoezi.

“Kipande hiki kilisogea na wamekitoa. Ni tofauti na ile risasi ambayo iko mwilini mwangu.”

Akieleza kiundani kuhusu hali yake, Lissu alisema anaendelea vizuri.

“Huu mkono wa kushoto ambao ulikuwa na tatizo, wameunyoosha na kuufanyia mazoezi kweli kweli na huu mguu wa kulia ambao ndio wenye tatizo, unaendelea vyema,” alisema.

“Huku ni mazoezi tu. Kwa siku nafanya mazoezi kwa saa nne, Naingia saa 3:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi, narudi tena saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Mwisho naingia mazoezini saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni. Hiyo ndiyo ratiba yangu kwa siku.”

Alisema katika mazoezi hayo anatumia magongo maalumu pamoja na kiti cha magurudumu.

“Mfano, huu mguu wa kulia natakiwa kuukanyagia kwa kilo 20 hadi 25 katika mzani na mimi nina kama kilo 90. Ninapoukanyagia ninaulizwa kama unauma, ikiwa sijasikia maumivu ina maana sijafanya kitu, kwa hiyo ni kazi kwelikweli,” alisema.

Kuhusu muda ambao anatakiwa kufanya mazoezi hayo mpaka atakaporejea katika hali yake ya kawaida, Lissu alisema bado hajajua.

“Ah bwana we, hapa madaktari wamegoma kunieleza hilo, lakini wameangalia katika maungio ya goti la mguu wa kulia kuna mfupa haujaunga vizuri, ni lini utaunga hilo sijajua,” alisema.

Mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya siku hiyo usiku.

Desemba 21 mwaka jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam, Lissu alisema madaktari wa Nairobi walimueleza kuwa risasi iliyokuwa imesalia mwili haina madhara.

Alisema risasi saba zilitolewa na madaktari hao, jambo lililomaanisha kuwa risasi nyingine nane, zilitolewa na madaktari wa Tanzania, saa chache baada y

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hakimu Amekataa Kujitoa Kusikiliza Kesi ya Sugu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite amekataa kujitoa kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na mwenzake.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30,2017.

Awali, leo Alhamisi Januari 25,2018 Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye.

Hakimu Mteite amesema sababu zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa.

Baada ya hakimu kukataa kujitoa, mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo.


Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili wengine.

Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi Februari 2,2018  na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Membe na Lowassa Uso kwa Uso Nyumbani kwa Gwajima.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe walipokutana leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala.

Lowassa, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na Bernard Membe kwenye msiba wa mama mzazi wa Askofu Gwajima.
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala jijini Dar es SalaamDownload  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mawakili Watatu wa Sugu Wajitoa.

Mawakili wa utetezi katika kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga wamejiondoa kutokana na kutokuwa na imani na muenendo wa kesi hiyo na kuwataka watafute Mawakili wengine.


Uamuzi huo wa Mawakili hao watatu ambao ni Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo umetolewa leo (Alhamisi) baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Michael Mteite, kugoma kujitoa katika usikilizaji wa kesi hiyo kama walivyotaka washtakiwa hao hapo awali kwa madai hawana imani nae.

Aidha, Hakimu Mteite alisema kuwa miongoni mwa sababu za yeye kuendelea na kesi hiyo ni kuwa Mahakama inayojukumu la kutoa dhamana au kutotoa kwa jinsi itakavyoona pia kuhusu ugumu wa kesi hiyo alikua anaamanisha ni kwamba inamvuto huku akidai hataweza kuendesha kesi hiyo kwa kumuogopa mtu kwa maana alikula kiapo.

Hata hivyo Wakili wa Jamhuri Joseph Pande aliiambia Mahakama kwamba Mawakili wa utetezi kujitoa kwenye kesi hiyo ni jambo la kawaida kwa kuwa wana sababu zao mbalimbali ambazo hawawezi kuzizungumza licha ya kuwa awali upande wa utetezi walikubali kuendelea na kesi hiyo.

Pamoja na hayo, Sugu na Masonga waliomba Mahakama kutoa (kuwapa) muda wiki mbili ili waweze kutafuta Mawakili wengine wawasimamie kesi yao hiyo kwa sababu wapo rumande hivyo itawachukua muda mrefu kujipanga na kuwatafuta na endapo itashindikana basi watajitetea wenyewe.

Kutokana na ombi hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahamaka ya Hakimu Mkazi Mbeya Michael Mteite aliwakubalia washtakiwa hao  matakwa yao na kuiharisha kesi hadi Februari 8 mwaka huu ambao itasikilizwa kwa mara nyingine.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mtoto Abakwa na Kuuawa Kikatili na Dereva ‘Boda Boda’.

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye pia ni mwanafunzi ameuawa kikatili baada ya kubakwa na muendesha pikipiki akiwa anaenda shule.



Imeelezwa kuwa Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 14 alikuwa anasoma darasa la sita katika shule ya Msingi ya Vikonge iliyopo wilayani Tanganyika mkoani Katavi.

Mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha ya kisu ubavuni mwake na sehemu zake za siri kunyofolewa .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi Jumanne tarehe 23 Januari 2018 saa moja asubuhi umbali wa kilometa moja na nusu kutoka shuleni kwake.

“Asubuhi hiyo ya tukio, marehemu akiwa ameongozana na mdogo wake wa kiume huku wakielekea shuleni walikutana na mwendesha pikipiki maarufu ‘bodaboda’ ambaye alikuwa hawamfahamu na kuwaambia kwamba atawapa lifti. Marehemu alipopanda mwendesha bodaboda alimzuia mdogo wake wa kiume asipande ambapo aliondoka akiendesha pikipiki hiyo kwa kasi isiyo ya kawaida huku kaka wa marehemu akiikimbilia bila mafaniko.“amesema Kamanda Nyanda.

Kamanda Nyanda amesema kuwa mdogo wa marehemu alitembea kwa miguu kuelekea shuleni baada ya kuchoka kuifukuza pikipiki hiyo, ghafla aliiona pikipiki ile iliyombeba dada yake ikiwa imeegeshwa karibu na kichaka kando ya barabara inayoelekea shuleni kwao na akaipita.

“Kaka wa marehemu bila shaka kutokana na umri wake kuwa bado mdogo baada ya kufika shuleni hakushughulika kumtafuta dada yake, aliingia darasani na kuendelea na masomo kama kawaida na baada ya muda wa masomo yaani saa nane na nusu alianza safari ya kurejea nyumbani bila kumtafuta dada yake,” ameeleza Kamanda Nyanda.

Hata hivyo, baada ya mtoto huyo kufika nyumbani wazazi wake walishtuka kumuona akiwa pekee yake ndipo walipomuhoji alikomuacha dada yake ndipo alipowasimulia kila kitu.

“Wazazi wa marehemu baada ya kupata maelezo hayo walipatwa na mashaka hivyo walimtaka mdogo wa marehemu awapeleke kwenye eneo alipoina pikipiki iliyombeba dada yake ikiwa imepakiwa karibu na kichaka. Mtoto huyo aliwaongoza wazazi wake ambao walikuwa wamefutana na majirani zao hadi kwenye eneo la tukio, walishtuka kuona kuwa kuna nyasi zilikuwa zimelala ndipo walipoona mwili wa marehemu ukiwa umechomwa kisu ubavuni huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa,“amesema Kamanda Nyanda.

Hili sio tukio la kwanza kutokea wilayani humo ambapo mwaka jana mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kipanga, Wilayani Tanganyika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 13 alikutwa amebakwa hadi kufa na mwili wake kutelekezwa vichakani.

Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na msako mkali kuwabaini wahusika wa tukio hilo ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Walichosema TAKUKURU Baada ya Kukamilisha Upelelezi Kesi ya Malinzi

January 25, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake umekamilika.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, pia jalada la kesi hiyo wameshalifanyia kazi ambapo upelelezi wamekamilisha.

Swai amedai kuwa jalada la kesi hiyo watalirudisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kama alivyowaagiza walirudishe kwake ili alikague tena baada ya upelelezi wao kukamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi February 8,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418 na washtakiwa wote wamerudishwa rumande 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Sababu 5 Zinazosababisha Uume Kuwa Mdogo (Kibamia)...Soma Hapa Kidume Ufahamu.

Kundi kubwa la wanaume ambao wanashindwa kufurahia tendo la ndoa kutokana na kuwa na uume mdogo kupita kawaida...
Wanaume walio na tatizo hili wengi wao huwa hawana confidence ya kuingia katika mahusiano na wasichana ama wanawake wanao fahamiana nao kutokana na kuogopa " siri" zao kujulikana hususani pale uhusiano wao unapofika mwisho..Ikitokea mwanaume akiwa katika uhusiano na mwanamke "mcharuko" ( asiye mstaarabu ) mwanamke huyo anaweza kuanza kumvua nguo hadharani kwa kumtangazia kwa watu kuwa na uume mdogo . " Mwanaume utakuwa wewe!" na lugha za namna hiyo hutawala midomoni mwa wanawake hawo....


Matokeo yake sasa wanaume walio na tatizo hili huamua kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wanao fahamiana nao, na badala yake huamua kuanzisha tabia ya kuwa wanajamiiana na wanawake wanaouza miili yao amakujihusisha na upigaji punyeto n.k.

NINI CHANZO CHA UUME KUWA MDOGO.

1. Kupiga Punyeto kwa muda mrefu..
Hali hii husababisha kusinyaa kwa uume na hatimaye uume kurudi ndani.
2. Kuugua chango la uzazi.
3. Magonjwa ya utotoni.
4. Kutahiriwa mapema
5. Kurithi kutoka kwa wazazi :

Wanaume wengine wana maumbile madogo kwa sababu wamerithi maumbilehayo kutoka kwa wazazi wao. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa