Wednesday 10 January 2018

Taharuki Yazuka Mtwara Wakesha Wakinywa Uji kwa Kutekeleza Agizo la Mtoto Aliyezaliwa na Kuongea Papo Hapo.

Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.

Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji  huo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment