Wednesday 10 January 2018

Joh Makini Afunguka Uhusiano Wake wa Kimapenzi na Mimi Mars.

Mwamba wa Kaskazini anayesumbua masikio ya wapenda burudani na ngoma ya 'Mipaka' Joh Makini amepangua tetesi za kujihusisha kimapenzi na mwanamuziki Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wake msanii Vanesa Mdee.


Joh Makini amepangua tetesi hizo kwenye Friday Night Live ya EATV ambapo amesema kwamba tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba yeye anamchukulia Mimi Mars kama mdogo wake kupitia heshima aliyojenga kwa wasanii hao ambao pia wanatokea kanda ya Kaskazini.

"A Big No. Mimi Mars ni kama mdogo wangu wa kike. Sisi ni familia moja aisee. Ni nani huyo ambaye anasambaza? alijibu Joh Makini kwa mtindo wa kuuliza.

Mbali na hayo Joh Makini amegoma kuweka wazi kuhusu mahusiano yanayodaiwa kuwa ni ya mdogo wake Nikki wa Pili na mpenzi wake Joan kwa madai kuwa hafahamu chochote.

Hata hivyo kumbukumbu zinaonyesha Joh Makini ni moja kati ya wasanii wachache hapa Bongo ambao amefanikiwa kuficha mahusiano yake kwa kipindi kirefu ambacho amesimama kwenye muziki.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment