Tuesday 16 January 2018

Breaking News>>>Sugu Apelekwa Mahabusu Baada ya Kunyimwa Dhamana.

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu ya gereza la Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya na kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.

“Kosa walilolitenda washtakiwa ni kutoa maneno ya fedheha yanayomtaja rais kuwa muuaji hivyo wakiwa nje wanaweza kupata matatizo kwa wananchi ambao hawajapendezwa na maneno hayo,” alidai Wakili Pande.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya ambapo Sugu anadaiwa kutamka kuwa rais ni muuaji.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment