Thursday 18 January 2018

Breaking News>>>Katibu Mkuu wa Chadema Augua Ghafla Akimbizwa Amana.

Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji amepelekwa Hospitali ya Amana kutokana na kuzidiwa ghafla.

Habari kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Shani Mwaruka amesema Mashinji amepokelewa hospitalini hapo na kueleza kuwa bado anapatiwa huduma ya kwanza katika chumba cha dharura.

Haijajulikana mara moja ni ugonjwa gani unamsumbua ila taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu ni kwamba ana mwezi mzima  alikuwa anaumwa akiwa nyumbani.

Katibu Mkuu wa CUF,  Maalim Seif  ameenda kumjulia hali Dk Mashinji amefika hospitalini hapo majira ya saa saba ikiwa ni muda mfupi tangu atoke kumsalimia mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombare Mwiru, aliyelazwa hospitali ya Muhimbili.
Chanzo: Mwananchi
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment