Wednesday 10 January 2018

Ole Sendeka Akanusha Sauti Inayosambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Asema Imetengenezwa na Wapinzani Ili Kumgombanisha.

Saa chache tu baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii sauti iliyodhaniwa kuwa ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akijadili namna ya utendaji wa Bunge na Awamu ya Tano ya Rais Magufuli mwenyewe ametolea ufafanuzi.

Ameeleza kuwa sauti hiyo siyo ya kwake na kwamba imetengenezwa na kuongeza kwamba sauti hiyo imetengenezwa na wapinzani ili kumfarakanisha yeye na viongozi wa serikali na walio chini yao.

“Naomba mzipuuze habari hizi kwa kiwango kinachostahili kwani zote ni uzushi mtupu , badala yake elekezeni macho, fikra na mikakati yenu katika uchaguzi unaokuja.” – RC Ole Sendeka

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment