Friday 30 June 2017

Meya wa Ubungo Dsm, Amefanya Uzinduzi Huu Jana.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, leo Ijumaa 30 Julai 2017, amezindua kituo cha kisasa cha kukusanya kodi, ushuru na tozo mbalimbali katika eneo la Simu 2000 pamoja na Kuhamsisha wafanyabiashara,bodaboda na Abiria wa Mabasi madogo .

Hii itapunguza kero kwa  wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na eneo la Simu 2000, kulipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali ambapo awali walilazimika kwenda Kibamba zilizopo ofisi za Manispaa ya Halmashauri ya Ubungo.

Kituo hiki kipya kinategemea kuwasaidia wakazi wa Sinza, Makurumla, Mburahati, Mabibo, Makuburi, Ubungo na maeneo yote ya karibu.

Aidha amewataka Halmashauri ya Ubungo, kuwalinda na kuwatetea Bodaboda dhidi ya TANROADS na JESHI LA POLISI kwa kusajili vituo vya kupaki pikipiki na bajaji na kuwapa namba za utambuzi kwakuwa Bajeti ya Halmashauri 2017/218, inawategemea kuwapatia Bodaboda na Bajaji kiasi cha shillingi Billioni 4 kama chanzo cha mapato.Wakiendelea kughasiwa Halmashauri itazikosa pesa hizo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Msanii Bobi Wine Ashinda Ubunge Nchini Uganda.

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu kama, Bobi Wine ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo nchini humo.

Tokeo la picha la bobi wine
Bobi Wine mwenye suti katikati akikabiliana na Askari Polisi mapema wiki hii

Wine, ambaye aliwania kama mgombea huru, aliwashinda wagombea wenzake wanne katika jimbo la Kyadondo Mashariki mwa Uganda kwa ushindi wa kura 25,659 kati ya kura elfu  33,310 zilizopigwa.

Kwa mujibu wa Gazeti la New Vision la nchini humo limeeleza kuwa baada ya kutangazwa Gazeti hilo linasema baada ya kutangazwa kuwa mshindi, aliahidi kurudisha umoja na mshikamano jimboni humo.

“Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo.“amesema Bob Wine.

Mwanamuziki huyo mapema wiki hii alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa muda kabla ya kuachiwa huru.

Kiti hicho cha ubunge kiliachwa wazi baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC Kizza Besigye amempongeza mwanamuziki huyo kwenye kupitia ukurasa wake wa Twitter.


obi Wine alianza muziki mapema miaka ya 2000 kabla ya kujitosa kwenye siasa uchaguzi mkuu mwaka 2016 na ngoma ambayo ilimfanya ajizolee umaarufu nchini humo ni wimbo wake wa Situka.

Kwenye wimbo huo, anatoa wito kwa raia wa Uganda kuchangia katika vita dhidi ya rushwa na ukiukaji wa haki nchini mwao.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Bei ya Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa zashuka.

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imeshuka kwa asilimia moja ukilinganisha na bei iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kuanzia kesho, bei hizo zitashuka na kuuzwa kwa Sh37 kwa lita (sawa na asilimia 1.81 wakati dizeli itauzwa kwa Sh 14 kwa lita (0.73 asilimia). Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 19 kwa lita (sawa na asilimia 1.03)

Ukilinganisha na bei zilizotangazwa mwezi Juni, nishati hizo zitapungua pia katika bei ya jumla.

Kwa bei za jumla, mafuta ya petroli yamepungua na sasa yanauzwa kwa Sh 37.21 kwa lita(sawa na asilimia 1.92)na dizeli itauzwa kwa Sh 13.70 kwa lita(sawa na asilimia 0.77) na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 18.85 (sawa  asilimia 1.10)

Punguzo hilo la bei linatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katka soko la dunia.

Hata hivyo Ewura imetangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga itapanda ukilinganisha na ile iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kwa bei ya rejareja, petroli itapanda kwa Sh 43 kwa lita na dizeli itauzwa kwa Sh 4 kwa lita.

Kwa bei ya jumla, petroli mkoani Tanga imeongezeka na sasa itauzwa kwa Sh 43.07 na dizeli itauzwa Sh 3.81 kwa lita.

Ongezeko la bei ya mafuta kwa mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia kwa shehena iliyoingizwa bandari ya Tanga ukilinganisha na bei ya shehena iliyopokewa Aprili 2017.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Nahisi Mke wangu Anawapenda Kimapenzi Wanawake Wenzake.

I think my wife likes women
------------------------------------
I would like to know if there are other men out there who think their wives are into women? I think mine is. I went through her Phone the other day and I couldn't believe the Whats app chat I read between her and someone I thought was just her friend. Another married woman for that matter. Their chat was of a sexual nature, something you would expect between a man and a woman. This lady even sent photos of her boobs and private parts to my wife.
I eventually confronted my wife about it and she said they were just joking around. Who jokes around with p**sy photos? What should I do now?

LMAO at who jokes around with vag*na photos. No, nobody does! So what should he do, other than ask for a three.some? Lol. *kidding*

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tazama Diamond alivyo Copy Na Ku-Paste Video ya Jason Darulo.

SOKO la nyimbo katika dunia ya sasa linakuzwa na video za muziki, ubora wa video umekuwa ukichangia kuufanya wimbo kuwa mkubwa hata kama ni wa kawaida.

Kuna vitu vingi vinavyochangia video kuwa bora, baadhi ni ubora wa picha, ubora wa mandhari na ubora wa ubunifu wa kile kinachoonekana katika video husika.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday 29 June 2017

Hili lingine la Rayvanny na BASATA Kuhusu Mapokezi na Tuzo ya BET.

Siku moja baada ya mwimbaji Rayvanny kuwasili Bongo na kukutana na mapokezi makubwa Airport DSM akiwa na tuzo yake ya BET akiwa msanii kwanza wa Bongofleva kutwaa tuzo hiyo…story gumzo ni kuhusu kutooneakana mwakilishi wa BASATA Airport.

255 ya XXL ya Clouds FM leo June 29, 2017 imempata Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ambaye ameelezea sababu za kutoonekana mwakilishi wa Baraza hilo akisema kulikuwa na mawasiliano finyu kati ya Rayvanny na BASATA wakati anakwenda na kurudi kuchukua tuzo hiyo.


 “Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima.


“Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee.” – Godfrey Mngereza.

Wakati huo huo Rayvanny amefunguka akidai kuwa sasa hivi kila kitu kipo wazi kutokana na mitandao lakini pia BASATA walitakiwa kusoma chochote kipindi tu walipoona amechaguliwa kwa kuwa ndio wazazi wa muziki wa Bongofleva na kama viongozi wao walipaswa kutoa support.

 “Kwa mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa kipaumbele sisi kutusaidia.” – Rayvanny.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Bifu la Diamond na EATV & Radio..Je Litaweza Kumshusha Diamond Kimuziki?

Bifu la Diamond na Alikiba naliona linafifia kila siku iitwayo leo, huenda likaisha kimya kimya bila hata wao kuonekana wakiwa pamoja katika picha au kufanya wimbo lakini kwa upande wa Diamond namuona kwenye Bifu zito na Ipp Media Especially EATV & RADIO, Ila bifu la aina hii (Msanii na Media) huwa halizungumziwi sana kwasababu hiyo media yenyewe haitataka msanii huyo asikike kupitia vipindi vyao tofauti na bifu kati ya Msanii na Msanii watawaita kila mmoja kwa wakati wake na kupiga nao story nini chanzo cha bifu lao .
.

Mara nyingi msanii anapokuwa na bifu na Media hasa ile yenye nguvu na ushawishi, msanii hujikuta akishuka kimuziki. Mfano mzuri #Ruby na #Clouds. Lakini hili la EATV na Diamond kiukweli ni ngumu kutabili itakuwaje kwasababu EATV hawapo vizuri kama zamani na kwa upande wa Diamond yupo vizuri kimuziki na mashabiki zake ambao wapo active sana. Hivyo ni ngumu kusema kuwa EATV ndio watayumba kwasababu ile ni taasisi na vile vile ni ngumu Diamond kushuka kimuziki kisa EATV kwasababu yupo pamoja na Media yenye nguvu kwasasa (Clouds) .
.

Sijawahi kuona Msanii aliyeshuka kimuziki kisa alikuwa na Bifu na EATV ila CLOUDS....ishawatoa wengi kwenye ramani na Wasanii hao hao EATV walijaribu kuwashika mkono lakini hawakuwa na nguvu hiyo.


TOA MAONI YAKO HAPA


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Lowassa Awasili Polisi na Kuhojiwa.......Atakiwa Kurudi Tena July 13

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa  amewasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo (Alhamisi) kama alivyoelekezwa siku ya Jumanne wiki hii baada ya kuhojiwa kwa saa nne.

Lowassa amewasili saa 5:52 asubuhi akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe huku ulinzi mkali ukiwa umewekwa katika makao makuu hayo.

Kando na hao walikuwepo watu wengine aliombatana nao, lakini walizuiliwa kuingia na askari walioimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Askari hao pia waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo na kuwataka kusogea mbali ya viunga vya makao makuu hayo.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi Lowassa aliondoka katika makao makuu hayo huku Mbowe akieleza kuwa ametakiwa kurudi Julai 13 kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika

Lowassa alitakiwa kufika polisi leo tena kwa tuhuma za kutoa kauli ya kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23 na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Jumatatu wiki hii Lowassa alipokea wito wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz kwenda kuhojiwa juu ya tuhuma hizo na alitakiwa kuripoti saa 4 asubuhi siku ya Jumanne.

Lowassa aliwasili Jumanne saa 3:58 asubuhi kama alivyotakiwa akiwa na msafara wa magari manne ambayo yaliyosindikizwa na magari mawili ya polisi.

Alihojiwa kwa saa nne mfululizo kabla ya kuachiwa kwa dhamana saa 8:15 mchana na kuelekea nyumbani kwake, Masaki ambako alizungumza na vyombo vya habari.

Baada ya kuachiwa, wakili wake Peter Kibatala ambaye pia alikuwepo katika mahojiano hayo alisema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena kwa DCI leo saa sita mchana ili kujua taratibu watakazoambiwa.

Kibatala alisema Lowassa alihojiwa kwa kosa la uchochezi kwa kauli yake aliyoitoa Juni 23 na kwamba baada ya kuhojiwa aliandika Maelezo ya Onyo juu ya kauli yake ambayo imetafsiriwa kuwa ni ya kichochezi.

Maelezo hayo ya onyo yanaweza kutumika dhidi ya Lowassa kama akifikishwa Mahakamani.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

IGP Simoni Sirro atembelea Kijiji alichouawa Mwenyekiti na Mtendaji Huko Kibiti.

Baada ya  mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.

IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.
IGP Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.
IGP Sirro aizungumza na Wananchi wa Mangwi alipowatembelea baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji
IGP Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa Wananchi wa kijiji cha Mangwi

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News>>>Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFF.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.

Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.

Usaili wa viongozi wanaogombea uongozi TFF unafanyika kuanzia leo hadi keshokutwa wakati huo Malinzi atakuwa mahabusu.

Malinzi amefikishwa leo mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine.

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa.

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji.

Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Mr Blue Ft Jr unaoitwa "Siwezi".

https://my.notjustok.com/track/download/id/237013


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Dawa Mpya ya UKIMWI Yaanza Kutumika Kenya.

Hatimaye Kenya imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia vidonge vya ugonjwa wa Ukimwi ambavyo vinaweza kuboresha afya na kurefusha maisha ya maelfu ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi na ambayo hayakubali tiba nyingine.

Jina la dawa hiyo kitaalamu ni Dolutegravir (DTG), lakini itajulikana kama Tivicay, na inazalishwa na ViiV Healthcare, kampuni ambayo sehemu kubwa ya hisa zake inamilikiwa na GlaxoSmithKline.

DTG imekuwa dawa ambayo ni chaguo la kwanza la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa miaka miwili iliyopita katika nchi za watu wenye kipato kikubwa kwa kuwa ina athari chache, ni rahisi kutumia kuliko dawa za ARV zinazotumika sasa (yaani kidonge kimoja kidogo kila siku).

Kwa kutumia dawa hiyo, kuna uwezekano mdogo kwa wagonjwa kutengeneza usugu, kwa mujibu wa tovuti ya unitaid.eu.

Mwaka 2015, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza DTG iwe chaguo la kwanza kwa watu wazima na vijana, lakini hadi siku za karibuni watu wanaoishi na VVU katika nchi kama Kenya walikuwa hawawezi kupata dawa hizo.

Vidonge hivyo, ambavyo vilipitishwa kutumika nchini Marekani mwaka 2013, sasa vinagawiwa kwa wagonjwa 20,000 nchini Kenya kabla ya kupelekwa Nigeria na baadaye Uganda, kwa kusaidiwa na Unitaid, ambao ni wakala wa afya.

DTG ni dawa ambayo inatumiwa na watu wenye VVU ambao hawakuwahi kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi ya ARV.

“Nilikuwa na tatizo la mara kwa mara la kutokuwa na hamu ya kula,” alisema mkazi wa Nairobi, Doughtiest Ogutu alipozungumza na taasisi ya Reuters Foundation.

Ogutu alianza kutumia dawa hizo mwaka huu kwa sababu tiba nyingine hazikuwa zinamfaa.

“Hamu yangu ya kula imerejea, mwili wangu unafanya kazi vizuri.”

Ogutu, ambaye ameishi na VVU kwa miaka 15, alisema kiwango cha VVU mwilini mwake kimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka virusi 450,000 hadi 40,000 tangu aanze kutumia DTG.

Nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa zikiathiriwa sana na Virusi vya Ukimwi kwa miongo kadhaa na karibu robo tatu ya wakazi wake wana Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS) linalenga kuwa asilimia 90 ya watu watakaogundulika kuwa na VVU wawe wamepata dawa hiyo ifikapo mwaka 2020.

Karibu asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU hawawezi kutibiwa kwa kuwa dawa hazifanyi kazi mwilini mwao, alisema Sylvia Ojoo, mkurugenzi wa Shule ya Afya ya Chuo Kikuu cha Maryland nchini Kenya, ambaye anasimamia dawa hizo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

MREMBO Anayesemakana ni Mdogo wa Zari (Asmah Honey) Awakana Zari , Patrick PCK na Irene Uwoya.

Mrembo wa haja anayejulikana mitandaoni kama Asmah Honey amejikuta katika wakati mgumu baada ya ku andikwa kuwa yeye ni mdogo wa Zari na anatoka kimapenzi na Mwanaume Mpenda kiki za Bure Patrick PCK , Honey ametuhabarisha kuwa Ndugu zake na marafiki wanampigia simu kuhusu tuhuma za kufumaniwa na kupigwa mawe na Irene Uwoya kitu ambacho kinamwaribia CV yake.......

ASMA HONEY NI NANI?
Mrembo Asmah Honey Amewasiliana na sisi moja kwa moja na kudai kuwa yeye ni Mnyaruada kwa kabila na kwasasa anaishi Burundi, Amesema Tanzania Huwa anakuja tu kwa ajili ya kufanya biashara zake

KUHUSISHWA NA ZARI HASSAN
Asmah anadai mwenyewe haelewi kwanini watu wanamwita mdogo wake na Zari Kwani Hawana udungu wowote na Mama watoto huyo wa Diamond kutoka Uganda, Mtandao mmoja mkubwa Bongo ulitoa habari yenye kichwa cha Habari kinachosema 'Uwoya Amfanyia Kitu Kibaya Mdogo wake Zari " Kitu ambacho si Kweli, Mwenyewe Adai hata Zari Hajawahi kumuona Live zaidi ya Kwenye Mitandao..

KUTOKA KIMAPENZI NA PATRICK PCK
Asmah Honey amedai hizo ni kiki tu anazotafuta Mwanaume huyo kwani hajawahi toka nae kimapenzi zaidi ya kumsikia tu , Adai huyo Mwanaume hivi karibuni amekuwa akitumia wasichana tofauti kwa ajili ya kujitafutia Kiki magazetini na mitandoani
Ikumbukwe mwanaume huyo ameshaandikwa pia kuwa anatoka na Irene Uwoya na Mrembo Mwingine anayeitwa Kibonge Sexy

WOLPER KUMFUMA NA PCK NA KUMRISHIA MAWE

Mwenyewe amedai habari hiyo iliyoandikwa na mtandao mmoja mkubwa Bongo sio ya Kweli kwani yeye tarehe hizo zilizoandikwa kuwa alifumaniwa hakuwepo Tanzania , Asmah Pia amekana kumfahamu Irene Uwoya kama mke Mwenza Kwa PCK na Kudai anamuona tu mitandani

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

A to Z Kuhusu Kibano cha Malinzi na Mwenzake Takukuru.

RAIS wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa, wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutokana na tuhuma za rushwa.


Akizungumza na Nipashe jana, Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Takukuru Makao Makuu, Mussa Misalaba, alisema waliwakamata wawili hao juzi kabla ya kuwahoji kwenye ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana.


"Tunaendelea na uchunguzi dhidi yao na viongozi mbalimbali wa TFF," alisema Misalaba.


Hata hivyo, Misalaba alisema kwa sasa hawawezi kuweka wazi kila kitu kwa sababu bado wangali wakiendelea na uchunguzi ambao daima huongozwa na misingi ya sheria.


"Katika uchunguzi wetu tunaongozwa na misingi ya sheria, kanuni na taratibu. Hatuwezi kuweka wazi kila jambo.


"Kikubwa Watanzania waelewe kuwa tuna uchunguzi ambao tumekuwa tukiufanya TFF kwa muda mrefu. Tunawashikilia hao wawili (Malinzi na Mwesigwa) na tunaendelea kuwahoji kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Ushahidi tunao, lakini kwamba tutafanya nini, hiyo ni siri ya uchunguzi,” alisema Misalaba.


Pamoja na wawili hao, ofisa huyo wa Takukuru alisema kila kiongozi au mdau wa TFF anayedaiwa kuhusika katika tuhuma hizo za rushwa anachunguzwa, hivyo kuna uwezekano wa kuhojiwa zaidi na hatua kuchukuliwa kadri matokeo ya uchunguzi yatakavyoonyesha.


"Tunafanya uchunguzi wetu kule TFF. Yeyote atakayekuwa amehusika katika ule mkondo, tutamfikia," alisema.


"Kuna tuhuma kule TFF kwamba kuna mambo kadhaa ambayo yamefanyika. Sisi tupo kila mahali na tumejipanga. Hatusubiri kuletewa taarifa tu."


HOJA ZA RIPOTI ZA UKAGUZI

Ingawa Misalaba hakuwa tayari kutaja aina ya rushwa ambayo Malinzi na viongozi wenzake wa TFF wanatuhumiwa, Nipashe inafahamu kwamba kiongozi huyo ni miongoni mwa wadau wa soka waliohusishwa na madai ya uchotwaji wa mabilioni ya shilingi kwenye akaunti za TFF kinyume cha taratibu hivi karibuni.


Ripoti ya ukaguzi maalum wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa timu ya taifa (Taifa Stars) iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inabainisha hofu ya kuwapo kwa matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa TFF, akiwamo Malinzi.


Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe mwezi uliopita kwamba iliandaliwa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa TFF na TBL.


Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaainishwa katika mkataba wa TBL na TFF.


Pia ripoti ya ukaguzi wa hesabu za fedha za TFF iliyotolewa Januari 19, mwaka jana na Kampuni ya Ukaguzi ya TAC Associates, inaibua maswali ya kiukaguzi kuhusiana na matumizi ya mamilioni ya shilingi uliofanywa na watendaji wa TFF kwa kushirikiana na wadau wa soka nchini.


Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Desemba, 2011 uliidhinisha kampuni hiyo kuwa mkaguzi wa nje wa hesabu za shirikisho kwa miaka mitano kuanzia mwaka ulioishia Desemba 31, 2011.


Ripoti hiyo inabainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia Agosti 15, 2014 hadi Septemba 30, 2015, TFF ililipa jumla ya Sh. milioni 274.072 kwa aliyekuwa Katibu wa Chama cha Soka (FAT sasa TFF), Michael Wambura na kampuni mbalimbali bila kuwa na nyaraka stahiki kuthibitisha malipo hayo.


Mbali na Malinzi, wadau wengine wa soka waliotajwa katika ripoti hizo mbili zenye kuibua maswali kadhaa ya kiukaguzi ni pamoja na Mwesigwa na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.


Mbali na kutofuata matakwa ya Kanuni za Fedha za TFF, ripoti hizo zinabainisha kuwa wadau hao wa soka walipewa fedha hizo bila kukatwa kodi ya serikali, kinyume cha Sheria ya Kodi ya Mwaka 2008.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mchezaji Donald Ngoma si wa Mchezo..Akata Mzizi wa Fitina...Yanga au Simba? Jibu Hili Hapa.

Mshambuliaji wa  Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za timu hiyo wamethibitisha taarifa za usajili huo kwa kuandika “Donald Ngoma Raia wa Zimbabwe ni mali ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.”

Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga wapinzani wa Yanga, Simba kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini ‘ ambapo alitua nchini usiku wa jana na  mchana  wa leo amesaini mkataba huo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday 27 June 2017

DAVID Kafulila Afunguka Haya Kuhusu Escrow.

WAKATI gumzo nchi nzima likiwa ni wizi mkubwa ambao haujawahi kufanyika wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Tegeta Escrow, imeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wakihatarisha maisha yao na wengine wamepoteza ubunge kwa sababu ya kupinga ufisadi huo.

Vinara wa kufichua sakata hilo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ndiyo waliofichua mambo hayo kwa nyakati tofauti.

Kafulila aliyehojiwa na gazeti hili wiki iliyopita alisema kundi lao la kupiga vita ufisadi huo lilikuwa hatarini kwa sababu kuna fedha zilikuwa zinatumika ili kuzima wizi huo.

Marehemu Deo Filikunjombe (ushoto), Davidi Kafulila, Zitto Kabwe pamoja na David Silinde.

“Hata wenzetu wabunge walikuwa wakitupinga na kwa kweli tulikuwa katika wakati mgumu, hata hivyo, hatukuacha kupigania jasho la umma ambalo lilikuwa limeliwa na watu wachache,” alisema Kafulila.

Alisema kuna wabunge ambao walikuwa wakiunga mkono vita hiyo nao walikuwa hatarini lakini kuna wengine ambao walikuwa upande wa mafisadi.

“Nashukuru kuna baadhi ya wabunge walikuwa wakiunga mkono vita dhidi ya ufisadi wa Escrow lakini baadhi walikuwa upande wa mafisadi. Ilikuwa hatari kwa sababu fedha zilikuwa zikitumika kuhujumu mpango mzima,” alisema Kafulila.

ZITTO ANENA
Naye Zitto katika andiko lake maalum amesema ili kuepuka kuuawa hasa kwa sumu, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa ambaye likuwa makamu wake kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe alimleta dada yake (Zitto) mjini Dodoma ili awapikie chakula kwa ajili ya usalama wao.

Zitto alisema katika uchunguzi wao juu ya wizi huo alikutana na wengi akiwemo aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

Siku niliyokutana naye nilimwambia: “Nimetoka kuonana na (namtajia jina na cheo – kwa sasa nalitunza si vema kumtaja), amenipa nyaraka zote za fedha zilizotunzwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow na kutolewa kulipwa PAP kama mmiliki wa IPTL. Sisi PAC tunataka sasa ufanye ukaguzi maalumu wa suala hili.”

BADE NA DK. HOSEA
Alisema kiongozi huyo na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rashide Bade pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takururu), Dk. Edward Hosea walitoa ushirikiano mkubwa kufanikisha kazi yao.

“Tulipata msaada pia wa aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, alitoa msaada mkubwa sana kwa kamati. Naye akatukanwa kuwa hakuwa msomi na alipata ziro akiwa kidato cha sita. Vyombo vya habari vilishangilia sana vioja hivi vya waziri kutaja matokeo ya shule ya mbunge bungeni ili kumvunjia heshima mbele ya jamii,” alisema Zitto.

Akaongeza kufafanua: “Ili kujenga umoja ndani ya Bunge nilimwomba spika (Anne Makinda) kuniongezea wajumbe kwenye kamati, ombi ambalo lilikubaIiwa. Tuliongezewa wajumbe kadhaa, akiwemo ndugu Kangi Lugola, Suleiman Zedi na Dkt. Hamis Kigwangalla.

“Hawa walikuwa ni viongozi wa Kamati nyingine. Lengo letu lilikuwa ni kuongeza nguvu kwenye Kamati ya Uongozi na pia sauti zenye uelewa. Tulitaka kuwe na taswira kubwa ya Kamati, isiwe tu ni PAC, iwe ni ya vyama vyote na yenye taswira ya kitaifa. Jambo hili lilitusaidia sana.

“Wakwapuaji nao walijipanga kwenye fedha. Walikuwa wanagawa fedha kwa kila mbunge anayechangia. Sisi tuliamua kuwachezea mchezo wa kupanga wachangiaji wetu wazuri siku ya mwisho na wao wakajaa kuchangia siku ya pili ya uwasilishaji wa taarifa bungeni, Alhamisi Deo Filikunjombe alifanya kazi hiyo ya mkakati.

“Spika Makinda na kabla yake Naibu Spika Ndugai walitupa ushirikiano mkubwa.
Ndugai alituambia wakati wa kukabidhiwa ripoti, namnukuu “Waelezeni Watanzania ukweli. Nipo nanyi.” Kweli alikuwa nasi na ili kutupunguza nguvu akapewa safari ya ghafla ya kwenda Paris.”

KUSHINDWA KWA WABUNGE
Habari za ndani zinasema baadhi ya wabunge waliokuwa wakipinga ufisadi huo walifuatwa majimboni mwao na mafisadi ili kuhakikisha hawarudi tena bungeni.

Baadhi ya wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Anna Kilango Malecela (Same Mashariki), David Kafulila (Kigoma Kaskazini) na James Lembeli (Kahama Mjini), Suleiman Zedi (Bukene), huku wengine wakiponea chupuchupu akiwemo Zitto, Kangi Lugora, Dk. Khamisi Kigwangalla na Spika Job Ndugai


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

HATIMAYE..Rayvanny Akamilisha Ndoto yake Kwa Jason Derulo.

Kushindwa kutumia fursa kwa kila nafasi unayoipata imeonekana ni dhambi kubwa kwa wasanii wa WCB. Hatimaye Rayvanny amekamilisha ndoto yake aliokuwa akiiota kwa muda mrefu.


Hitmaker huyo wa Zezeta, ambaye siku chache zilizopita alinyakuwa tuzo ya BET, amefanikiwa kukamilisha kufanya kazi na Jason Derulo kutoka Marekani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Ray ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika, “God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii 😂lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”

Baada ya wasanii hao kukamilisha kazi yao hiyo walijumuika pamoja katika kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ambapo Ray alijikuta akiambulia za uso kutoka kwa Jason. Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye Coke Studio Afrika wiki chache zilizopita.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

CCM yaendelea na Operesheni ya Kutumbua Wasaliti.

KATIBU wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema viongozi na watendaji watakaoitumia CCM kwa faida yao binafsi siku zao zitahesabika.

Aidha, Polepole alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara na daraja kati ya wananchi na serikali yao ili kuhakikisha kinawasemea watu wengi, maskini na wanyonge ambao haki zao zimeporwa na kupokwa kwa muda mrefu.

Akihutubia mkutano wa ndani wa viongozi wa matawi na kata wa chama hicho waliochaguliwa karibuni, katibu mwenezi huyo aliwataka viongozi na watendaji ndani ya chama hicho kuacha kukitumia kwa faida yao binafsi bali watangulize mbele maslahi ya wengi, vinginevyo siku zao zitahesabika.

Katibu huo alikuwa akizungumza na mabalozi na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa akiwa katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Ziara hiyo ina lengo la kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2025 pamoja na kuimarisha uhai wa chama hicho.

“Viongozi wasio waadilifu ndani ya Chama watambue huu ni wakati mwingine... waanze kubadilika," alisema Polepole "maana hatutowavumilia watu wanaotumia mali za chama chetu kwa manufaa yao."

"Watambue siku zao zinahesabika... wale wote walio na makandokando ya uovu wasipate nafasi ya kupata uongozi wowote ndani ya chama.
"Tunawatafutia engo ya kula vichwa vyao.”

Aidha Polepole alimpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya.

Naye katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alikemea mnyukano miongoni mwa watendaji wa serikali na viongozi wa kisiasa waliomo kwenye vyombo vya dola unaofukuta katika baadhi ya halmashauri mkoani Mwanza.

“Kuna shida katika baadhi ya watumishi walioaminiwa


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Gabo amzungumzia Kanumba na Wema Sepetu.

Msanii wa Filamu Tanzania, Gabo amesema si kweli tasnia ya filamu imeshuka baada ya kifo cha Steven Kanumba.

Muigizaji huyo ameeleza kuwa watu wengi wanaamini kutokuwepo Kanumba kumedhoofisha soko kutokana alikuwa wenye kuleta changamoto ambayo kwa sasa haipo.

“Sio kweli industry ipo vile vile, kwa hiyo jamaa alikuwa analeta changamoto kwa wacheza sinema wengi sana hivyo baada ya kuondoka ule ushindani ukawa umeshuka, hicho ndio kitu ambacho wanakikosa,” Gabo ameiambia Bongo Dot Home ya Times FM na kuongeza kuwa

“Lakini mimi nisema waendelee kuwa na mapenzi ya dhati ila wasiste kutoa malalamiko yao na kukosoa pale ambapo wanahisi pameenda tofauti kwa sababu changamoto za watu pekee ndio zinabadilisha.Tunajua hapo tunakosea inabidi tufanye hivi, kwa hiyo tunaenda tunabadilika kutokana na mawazo ya watu,” amesema Gabo.

Katika hatua nyingine Gabo amemuelezea muigizaji Wema Sepetu ni mtu wa namna gani katika ufanyaji kazi hasa pale walipokuwa wakishoot filamu yake mpya ‘Kisogo’.

“Ni dada mmoja ambaye yupo na utaratibu wake, ukiufuata na kuusikiliza utafanya nae kazi vizuri sana na atakuwa yupo poa sana. Ukiwa nje ya huo utaratibu unaweza kumuona ni msumbufu na ukamuona kero kwenye kazi,” ameeleza Gabo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Young Killer unaoitwa "True Boya".

https://my.notjustok.com/track/download/id/235508

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa WEUSI unaoitwa "Amsha Dude".

https://my.notjustok.com/track/download/id/235506


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

WAANDISHI wa TBC Wanyang'anywa Kamera.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 9:00 alasiri katika Barabara ya Darajani­ Mnazi Mmoja, eneo maarufu la Shule ya Sekondari Ben Bella mjini Unguja.

Akizungumza na gazeti la Nipashe, dereva wa gari la TBC Mohammed Awadhi alisema walitoka ofisini eneo la Maisara wakielekea Vuga katika majukumu yao ya kazi, lakini walipofika eneo hilo walivamiwa na kuporwa vifaa vya kazi ikiwamo kamera.

Alisema majambazi hao walikuwa na gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikiwafuatilia kwa nyuma lakini hawakuweza kuitambua namba zake.


Tulipofika eneo la Shule ya Ben Bella ghafla ile gari ya majambazi ikatuzingira mbele ya gari yetu,” alisema.

“Watu wawili walishuka na kulazimisha kuwa wapewe begi lililokuwa katika gari ambalo ni begi la vifaa vya kazi.

Awadhi alisema walianza kunyang’anyana begi hilo na majambazi hao kabla ya kupiga kelele za kuomba msaada kwa wananchi.

Alisema wananchi walipotaka kusogea eneo la tukio, majambazi hao walitoa bastola na kutishia kuwapiga, na ndipo walipofanikiwa kuchukuwa begi na kuondoka nalo kwa kutumia Noah ambayo haikuwa na namba sahihi.

Mimi fikra zangu nadhani walijua lile begi ambalo lina vifaa vyetu vya kazi kuna fedha kwa sababu (katika) jengo la ofisi yetu pia kuna beki,” alisema Awadhi. “Hivyo walipoona tunatoa gari nadhani walijuwa tunatoka benki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wahalifu hao ambao wanaweza kuhatarisha maisha ya wananchi.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Quick Rocka & OMG unaoitwa "WATASEMA".

https://my.notjustok.com/track/download/id/235505


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Kauli ya CHADEMA Baada ya Lowassa Kuitwa Polisi Leo Kwa Mahojiano.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.

Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.

Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.

Imetolewa  Jumatatu, Juni 26, 2017 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa