Sunday 25 June 2017

Cristiano Ronaldo Hakamatiki..Haya Ndio Maajabu Mengine Aliyofanyia Nchi yake.

Cristiano Ronaldo akishangilia kibabe baada ya kuifungia Ureno bao la kwanza kwa penalti dakika ya 33 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya New Zealand baada ya Danilo kuchewa rafu usiku wa Jumamosi Uwanja wa Krestovskyi mjini St Petersburg katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mabara. Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Bernardo Silva dakika ya 37,  Andre Silva dakika ya 80 na Luis Nani dakika ya 90 na ushei. Matokeo hayo yanaifanya Ureno ifikishe pointi saba na kumalizana kileleni sawa na Mexico iliyomaliza na pointi saba pia baada ya kuifunga Urusi 2-1 na zote zinakwenda Nusu Fainali. Wenyeji Urusi wameungana na New Zealand kupanda jukwaani kitazama mechi za kumalizia michuano ya 2017

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment