Monday 19 June 2017

Marekani yaitungua ndege ya kijeshi ya Syria.

Marekani imeitungua ndege ya kijeshi ya Syria iliyokuwa ikijiandaa kuwashambulia wanamgambo wa IS ambao wamekuwa wakihatarisha maisha ya wananchi wa nchi hiyo huku umoja wa mataifa ukitaka kuwepo na usuluhishi.

Aidha, Marekani imesema kuwa imefikia hatua hiyo mara baada ya jeshi la Syria kuvishambulia vikosi vya Syrian Democratic Force SDF, vinavyoungwa mkono na Marekani  kwa lengo la kupambana na wanamgambo wa Islamic State.

Kwa upande wa Serikali ya Syria imesema kuwa ndege yake ilikuwa katika maandalizi ya kuwashambulia wanamgambo wa Islamic State na si vikosi vya Syrian Democratic Force vinavyoungwa mkono na Marekani.

Vikosi vya Syrian Democratic Force (SDF ) vinaungwa mkono na umoja unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana na wanamgambo wa Islamic State ambao wamekuwa tishio katika ukanda huo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment