Thursday 22 June 2017

USAJILI:Mashabiki wa Yanga SC Wachoma Jezi ya Niyonzima.

Kuondoka kwa mchezaji Haruna Niyonzima ndani ya klabu ya Yanga SC, kumeonyesha kuwaumiza mashabiki wa klabu hiyo ambapo moja kati ya kundi la mashabiki wameamua kuchoma jezi ya mchezaji huyo.

Mashabiki wakionekana kuichoma moto jezi yenye jina la Niyonzima na namba 8 mgongoni namba ambayo hutumia mchezaji huyo uwanjani

Hapo jana Klabu ya soka ya Yanga ilitoa taarifa ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kuafikiana.

kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa alisema Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hawataweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kutokana na kushindwa kkuafikiana katika mazungumzo.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment