Sunday 25 June 2017

Siku Moja Tu watu wang’oa Bango la Mtaa wa Victor Wanyama.

Unaweza usiamini, jana tu ilitolewa zawadi ya mtaa, asubuhi ya leo tayari bango la Mtaa wa Victorr Wanyama limeng’olewa.

Taarifa zinaeleza wako ambao walitaka kuiba bango hilo kwa ajili ya vyuma chakavu lakini wengine wanaeleza, wako waliochukizwa Wanyama kupewa jina la mtaa Tanzania.

Jana, Meya wa Manispaa ya Ubongo Boniface Jacob, alimtunuku mtaa, Kiungo wa Tottenham ya England Victor Wanyama raia wa Kenya.

Jacob ambaye ni Meya akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alimkabidhi Wanyama mtaa ambao awali ulikuwa unajulikana kama Viwandani na sasa utajulikana kama Victor Wanyama.

Mtaa huo uko Ubungo katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment