Saturday 30 April 2016

Niva Atoboa Sababu ya Nay wa Mitego Kuachwa na Shamsa Ford.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa filamu nchini Niva Super Mariyoo, ambaye alionja joto ya jiwe kwa muda fulani baada ya kutajwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika adabu yako’ na kusema “Huyo msanii huyo hana hata chumba cha kupanga ila anaishi kwenye gari”.
Niva amefunguka na kusema kuwa Nay wa Mitego siku zote huwa anaimba watu maarufu ili apate kiki na kusema msanii huyo kutokana na kufanya nyimbo mbovu mbovu ndiyo maana hata siku moja hajawahi kupata tuzo.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS Niva Super Marioo amedai kuwa ni kweli kwa sasa wanawake wengi wanafanya kazi na kutafuta riziki na wanakuwa wanawasaidia baadhi ya wanaume ambao kazi yao kukaa nyumbani kama Imma Chogo ambaye ni (Nay wa Mitego).

“Kimaisha mimi Imma Chogo hajanifikia sema sisi wengine huwa hatupendi kujiweka wazi sana, kama kweli mtu unamiliki nyumba, una kwako kwanini hutulii na familia? kama kweli wewe unajiona ni Gentle Man kwanini wanawake wanakukimbia? Star anakimbiwa? mimi najua Star anakimbiliwa. Mimi silelewi bali napewa mahaba ya dhati na mwandani wangu”. Alisema Niva.

“Mimi namkubali sana Shamsa Ford sababu aliona kabisa yeye ni classic sana kuliko Nay wa Mitego na ndiyo maana hajadumu naye akaachana naye, Nay wa Mitego tatizo haudumii na ndiyo kesi kubwa na Shamsa. Shamsa alikuwa akitoka kupiga movie lile bwana mkubwa linaanza kulialia oohh mara gari halina mafuta mara sijui nini, sasa yeye muziki wake yeye kweli kabisa kwanini anashindwa kumnunulia hata vitu anajinunulia mwenyewe” Niva aliongezea.

HATIMAYE JOTI AANZISHA TV YAKE YA VICHEKESHO…TAZAMA KICHEKESHO ALICHOANZA NACHO AKIWA KATIKA NYUMBA YA WEMA SEPETU.Fahamu zaidi hapa.

Wasanii wa vichekesho nchini wameanza kuamka na kutambua kuwa Youtube ni mtandao unaoweza kuwapa mkwanja mzuri kama wakiutumia ipasavyo. Joti ameamua kuja na series za vituko vyake ambavyo anaweka Youtube kwaajili ya kuvunja mbavu mashabiki wake. Check hiyo video ya kwanza.


#BREAKING NEWS>>>LOWASSA ASIMAMISHWA NJIANI NA WANANCHI WA DUMILA MORO..WATU WAMWITA RAIS.Fahamu zaidi hapa.

Kwa habari zaidi endelea kufatilia hii blog "Www.hebronmalele.blogspot.com"

#YALIYOJIRI>>>>Mbunge Prof. Anna Tibaijuka amemtaka Rais Magufuli aache kutumbua nyama akidhani ni majipu.Fahamu zaidi hapa.

Amesema “Naafiki kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi, labda itasaidia kukamatwa na kushitakiwa mafisadi wenyewe. Maana wengine tunatolewa kafara na mtandao hauguswi, labda zitaachwa kukamuliwa nyama na kuziita majipu”.

Akiongea na Count Down ya Clouds Fm Prof Tibaijuka amesema yeye ni muhanga wa ufisadi. Amesema kuna mtandao wa mafisadi unaotoa watu kafara na wenyewe hauguswi.

“Naafiki kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi, labda itasaidia kukamatwa na kushitakiwa mafisadi wenyewe. Maana wengine tunatolewa kafara na mtandao hauguswi, labda zitaachwa kukamuliwa nyama na kuziita majipu”. Alisema Prof Tibaijuka.

My take:
Mtandao huu ni upi? Unalindwa na nani? Hivi Prof ni msafi au anajitetea?


#YALIYOJIRI>>>>Wabunge wa CCM Wakataa Bunge Kuonyeshwa LIVE…….Wapinzani Waamua Kujirekodi Kwa Simu Zao.Fahamu zaidi hapa.

Wabunge wa CCM jana waliibuka kidedea walipowazidi wenzao wa upinzani kwa kura za sauti “Siyooooo” kuikataa hoja ya kutaka matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja ‘live’ na televisheni.

Hiyo ilitokea jana wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utumishi na Utawala Bora) na kuzua mvutano mkali uliosababisha bajeti hiyo ipitishwe kwa utaratibu wa wabunge kutohoji kitu chochote (guillotine).
 
Wakati hoja yao hiyo ikipingwa kila kona, tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, wabunge hao wa upinzani sasa wamebuni mbinu mpya ya kujirekodi wenyewe wakati wakichangia mijadala mbalimbali bungeni na kurusha sauti zao kwenye mitandao ya kijamii na kupeleka sauti hizo kwenye redio zilizopo katika maeneo ya majimbo yao.
 
Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Salehe ndiye aliyeibua hoja hiyo akitaka kushika mshahara wa waziri kwa maelezo kuwa kuzuia Bunge kurushwa ‘live’ ni kinyume na utawala bora na haki ya kupata habari.
 
Hoja hiyo iliungwa mkono na  Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, Masoud Abdalla Salim (Mtambale-CUF), Rose Kamili (Viti Maalumu -Chadema), Ester Matiko (Tarime Mjini – Chadema) na Mussa Mbarouk (Tanga Mjini – CUF).
 
Wabunge wa CCM waliopewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuchangia hoja hiyo ni Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Kangi Lugola (Mwibara), Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) pamoja na Waziri Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.
 
Ilivyokuwa  Bungeni
 Baada ya Salehe kutaka ufafanuzi wa kina huku akisisitiza kuwa uamuzi huo unakiuka Katiba ya nchi na haki ya kupata habari, Kairuki alisema kwa mujibu wa Ibara ya 18 na 100 ya Katiba zinazozungumzia uhuru wa kupata habari, uamuzi huo ni sahihi na hakuna mwananchi aliyenyimwa taarifa.
 
Maelezo hayo yalipingwa na Salehe, safari hii akifafanua kuwa matangazo ya Bunge yanarekodiwa kwa saa saba na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) kwa saa moja tu, huku wabunge wa upinzani wakiondolewa na kuonyeshwa wa CCM pekee.
 
Alitaka vyombo vya habari vya elektroniki kuruhusiwa kurekodi shughuli za Bunge na kurusha maudhui wanayoyataka, badala ya kupewa video na studio ya Bunge ambayo huondoa michango na hoja za wapinzani.
 
Mchungaji Msigwa, Masoud Abdallah, Kamili, Matiko waliungana na Salehe na kusisitiza kuwa nchi nyingi barani Afrika zinarusha ‘live’ matangazo ya Bunge huku wakihoji sababu za TBC kurusha moja kwa moja harusi na kushindwa kuonyesha shughuli za Bunge.
 
Mbarouk alikwenda mbali akitaka Bunge kuanza shughuli zake usiku ili kuendana na utetezi wa Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuwa usiku wananchi wengi wanakuwa majumbani mwao hivyo wanapata nafasi nzuri ya kufuatilia Bunge.
 
Matiko: Juzi Rais John Magufuli kazindua Daraja la Kigamboni, TBC ilikata matangazo ya Bunge ili kuonyesha uzinduzi huo. Yaani ya kwenu mnataka yaonyeshwe ila haya ya Bunge yasionekane. Mnakiuka demokrasia.
 
Ghasia: Demokrasia siyo Bunge kuonyeshwa ‘live’. Wakulima na wafugaji hawawezi kuona Bunge asubuhi ndiyo maana yanarushwa usiku.
 
Serukamba: Mbona wabunge wa Chadema wanaonyeshwa katika matangazo ya TBC. Hoja kwamba maagizo ya Serikali hayatawafikia watendaji si kweli.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju alisema wapinzani hawajiamini na hawaaminiki huku akiwataka wasome ibara ya 100 ya Katiba; “Bunge kuonyeshwa au kutoonyeshwa hakuongezi kitu jimboni. Wanaozungumza ni wabunge siyo televisheni.” 
 
Akihitimisha hoja, Kairuki alipinga maelezo ya Salehe na kutoa mfano wa nchi ambazo matangazo ya Bunge hayarushwi moja kwa moja.
 
Kutokana na mvutano huo Chenge aliwahoji wabunge wanaoafiki hoja ya Salehe waseme “ndiyooo”, wapinzani pekee wakasema ndiyoo, aliposema wasioafiki waseme siyo, wabunge wa CCM kutokana na wingi waliitikia kwa sauti kubwa siyoooo, na Chenge akasema anadhani wasioafiki wameshinda.
 
Wapinzani  Waamua Kujirekodi kwa simu
Kwa zaidi ya mara tano,wabunge wa upinzani wameshuhudiwa wakijirekodi ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kutumia simu zao za mkononi, wanapotoka nje huulizana kama wameshatumia video na sauti hizo katika mitandao ya kijamii.
 
Juzi, Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utawala Bora) alirusha sauti yake katika mitandao ya kijamii na kusema hiyo ni moja ya njia ya kuwafanya wananchi wajue kinachoendelea bungeni

#YALIYOJIRI>>>>MR. BLUE KASEMA – KUWA SUGU AMEHATARISHA NDOA YAKE.Fahamu zaidi hapa.

MKALI wa Muziki wa Hip Hop, Bongo Kheri Sameer ‘Mr Blue’ ameendelea kumporomoshea lawama Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa usumbufu aliokuwa anampa ili kuiachia ngoma yake ya Freedom ulimsababishia ‘rabsha’ ndani ya ndoa yake. 
 

Shutuma hizo anazozitoa Blue ni mwendelezo wa ‘drama’ inayoendelea kati yake na Sugu ambayo kwa sasa ndiyo habari ya mjini kufuatia madai ya Blue kuwa mheshimiwa huyo alimzunguka kwa kuuchukua wimbo wake huo ambao mwanzo yeye alimshirikisha, akaurekodi upya huku akifuta mashairi yake lakini kama haitoshi ‘akashuti’ video, jambo ambalo Blue analiona kuwa ni uonevu.
 

“Kwanza Sugu alinisababishia matatizo ndani ya ndoa yangu mpaka nikawa sipokei simu zake. Alikuwa ananipigia simu kila muda na kila siku akiuliza ‘project’ inatoka lini hadi mke wangu akawa anauliza kuna nini kati yetu.
 

 Mwanzoni nilimweleza hali halisi lakini kwa namna Sugu alivyokuwa ananisumbua ilifika hatua mke wangu akadhani kuna jambo lingine tofauti, kukawepo na rabsha za hapa na pale lakini sasa nimeweka mambo sawa,” alisema Blue.
 

Alipotafutwa Sugu kuhusu suala hilo, hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu lolote.

#YALIYOJIRI>>>>Makonda Asema hataki kuwaona wasanii nyumbani kwake,Ni Baada ya Kumtosa kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi.Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.

“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.

“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda.

Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.

Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.

Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.

#YALIYOJIRI>>>Watu kadhaa wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air kupata ajali katika Uwanja wa Bukoba leo.Fahamu zaidi hapa.

Watu kadhaa wamenusurika  kufa baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa ya Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo  kama inavyo onekana pichani.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30,2016.

#YALIYOJIRI>>>Wafanyabiashara Walioficha Sukari Waanza Kukamatwa.Fahamu zaidi hapa.

Kauli  ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameficha sukari ili kutengeneza uhaba sokoni utakaopandisha bei ya bidhaa hiyo, imedhihirika baada ya baadhi ya wafanyabiashara hao kuanza kukamatwa wakiwa na vidhibiti.

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo kuanza kupanda, Waziri Mkuu Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali kuagiza sukari yake nje itakayouzwa kwa bei elekezi kwa wananchi ya Sh 1,800 kwa kilo, ili kuzuia ongezeko hilo haramu la bei.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi alitangaza polisi kuwashikilia wafanyabiashara wawili wa mjini hapa kwa tuhuma za kukutwa na zaidi ya mifuko 655 ya sukari, sawa na tani 24.3, ikiwa imekifichwa kwenye stoo zao.

Kwa mujibu wa Amanzi, wafanyabiashara hao walikamatwa kwenye msako ulioendeshwa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Singida pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Amanzi alisema kuwa msako huo uliendeshwa baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameficha sukari, ili waje kuiuza kwa bei ya juu kwa wateja wao kwa kisingizio kuwa kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.

“Katika msako huo, tumemnasa Mohamed Alute Ally (44), mfanyabiashara wa eneo la Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39), mfanyabiashara wa eneo la Minga katika manispaa ya Singida aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa mwito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuficha bidhaa zote muhimu, ikiwemo sukari na mchele, bali waiuze kwa bei halali kwa wateja wao. 

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Mchina, amesema msako mkali unaohusisha kikosi kazi maalumu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama utaendelea kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa kuhodhi bidhaa kwa sababu yoyote ile ni kosa la uhujumu uchumi.

Mmoja wa Wakala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mjini, Salim Nagji, amesema mfuko mmoja wa sukari huuzwa Sh 92,650 lakini tangu sukari iadimike mfuko unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na Sh 2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya Sh 1,800.

#YALIYOJIRI>>>>Mapendekezo Ya Sheria Ya Wazee Kuwasilishwa Bungeni.Fahamu zaidi hapa.

NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni.

“Mimi pamoja na Waziri wangu, Ummy Mwalimu baada ya kupewa jukumu la kuongoza wizara tuliunda kikundi cha wazee kwa ajili ya kuamua mambo makubwa mawili ambayo tutayatekeleza likiwemo la pensheni kwa wazee wote,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema suala jingine ambalo wamepanga kulitekeleza ni utoaji wa huduma ya bure kwa wazee, ambapo watawapatia bima ya afya ili wasiendelee kusumbuka.

Kwa upande wake Waziri Mkuu aliwahakikishia wazee hao kwamba Serikali inawatambua na ndiyo sababu ya waliamua wawe na sehemu ya kufikishia malalamiko yao ambayo ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Kuhusu ombi la wazee hao kwa Rais Dk. John Magufuli la kuwa na uwakilishi Bungeni kwa kupitia nafasi zake 10 za uteuzi, Waziri Mkuu alisema amelipokea na atalifikisha kwa Mhe. Rais.

Pia amewataka wapanue taasisi yao na kuimarisha mtandao uweze kujulikana na wazee wengi zaidi, wawe na viongozi kuanzia ngazi za vijiji ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na utoaji wa huduma za afya kwa wazee katika hospitali mbalimbali alizotembelea na kukuta yameanzishwa madirisha maalumu ya kuhudumia.

Akizungumzia kuhusu suala la wazee kupewa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI aliwataka waandaaji wa matamasha na semina za mafunzo hayo kujumuisha watu wote wakiwemo wazee.

Naye Mwenyekiti wa mtandao huo , Bw. Sebastian Bulegi alisema lengo la kumtembelea Waziri Mkuu ni kumuomba awafikishie shukurani zao kwa Rais Dk Magufuli kwa kuwapatia wizara maalumu inayoshughulikia masuala yao.

“Vile vile shukurani hizi tufikishie kwa mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli kwa kufanya wazee kuwa agenda yake ya kwanza na tayari ameshatembelea makazi ya Nunge Kigamboni (Dar es Salaam) na Bukumbi (Mwanza),”alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na wajumbe wanane wa mtandao huo unaoundwa na Asasi 26 za wazee katika ngazi za wilaya na mkoa kutoka mikoa ya Kigoma, Tanga, Arusha, Mwanza, Lindi na Dodoma, aliiomba Serikali isimamie kutokomeza mauaji ya wazee.

Ombi jingine alilolitoa kwa Serikali ni utekelezwaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003, Sera ya Matibabu bure kwa wazee, mafunzo ya kupambana na UKIMWI pamoja na uwakilishi katika ngazi za kutoa maamuzi.

Pia wazee hao wamemhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamekubali ombi linalotolewa na viongozi wakuu wa nchi la kuwataka wawaombee ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980, DODOMA.
JUMAMOSI, APRILI 30, 2016.

Download nyimbo ya Ferooz inayoitwa "Nimejifunza".Hapa hapa.


#YALIYOJIRI>>>>TCRA Yatoa Onyo Kwa Wafanyabiashara Wanaobadili IMEI za Simu FEKI ili Kuwahadaa Wananchi.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano, kuacha kuwahadaa wananchi kwa kutoa punguzo ili kuwashawishi kununua simu bandia na kutishia kuwafunga miaka 10 jela, faini ya Sh30 milioni au vyote kwa pamoja watakaobainika.

Hatua hiyo imekuja wakati mamlaka hiyo ikiwa katika hatua ya kutekeleza mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi, huku ikitarajia kuzima simu feki ifikapo Juni 16.

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Mhandisi James Kiraba alisema kuna wafanyabiashara wajanja wanaobadilisha namba za utambulisho za vifaa vya elektroniki (IMEI) ili kuwahadaa wateja kuwa simu zao siyo feki.

Kwa ujanja huo, namba ya utambulisho inakuwa inatumika na simu zaidi ya moja na kutambulika na mfumo licha ya kuwa ni feki.

Pamoja na kuonekana ni halisi kwa kipindi wanachozinunua, alisema simu hizo zinazobadilishwa IMEI nazo zitazimwa Juni 16 kwa kuwa ni feki.

“Mamlaka inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mikononi (mobile devices), kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 au faini isiyopungua Sh30 milioni au vyote kwa pamoja,”alisema.

Alisema kumekuwa na udanganyifu kwa baadhi ya wauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu.

Kiraba alisema wananchi wanapaswa kuwa makini na hilo, huku wakihakikisha kuwa simu zao zimehakikiwa ili kuzuia usumbufu wa aina yoyote, utakaoweza kujitokeza wakati kipindi cha mpito kitakapomalizika.

Alisema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30 Desemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 13 Machi.

Alisema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 huku simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia nne, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13, uchambuzi huu unahusisha makampuni yote ya simu nchini,” alisema.

MH SUGU AMNUNULIA MPENZI WAKE WASASA GARI AINA YA LEXUS AZUA GUMZO MTANDAONI.Fahamu zaidi hapa.

Ripoti kutoka mitandaoni zinasema kuwa Muheshimiwa Mbunge Sugu Amemzawadia Gari aiana ya Toyota Lexus kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa mpenzi wake ajulikanae kama Happiness, Sugu na mpenzi wake huyo mpya wamekuwa gumzo mitandaoni hasa baada ya aliyekuwa mpenzi wa Sugu wa zamani Faiza Ally kusema bado anampenda Sugu….Wadau wengi tunasubiri kuona Faiza atasema nini kuhusu hilo kwani amekuwa sio mvumilivu wa kukaa kimya kinapokuja suala la Sugu
Hizi Hapa ni Baadhi ya Comments kutoka kwa wadau mitandaoni:
mrs_j6316 @mwakobadoris :njoo umuone Mrs sugu au first lady was Mbeya yetu mpaka raha wallah afu ametulia hadi uso
full_mikuki :Maskini bahati hizi wengine acha tuzae tu
fine_mushy: Tenaaaaaa sio Harrier bubu Maana Kuna Harrier Kma Harrier mamaeeeee kitu LEXUS hiooooo
official_chagga_girl: Kuna watu wanakufaa ukoo,haaa haaa @tit4tati

#YALIYOJIRI>>>>Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC ) Lakanusha Kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.Fahamu zaidi hapa.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. 

Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia.

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. 

Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

 Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:
1. Akaunti ya Mapato ya Gesi
Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2.  Akaunti ya Uendeshaji
Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3.  Akaunti ya Kulipia Deni
Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. 

Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

Friday 29 April 2016

VIDEO>>>MWILI WA PAPA WEMBA WAWASILI DR CONGO HII HAPA.

Jana mwili wa nguli wa musiki wa rumba Papa Wemba uliwasili nchini kwao Congo DR na haya ndiyo yaliyokuwa mapokezi yake.

#MICHEZO>>>FARID MUSA TAYARI KAPIMWA AFYA, ATASAINI DEAL SPAIN.Fahamu zaidi hapa.

 Habari njema kuhusu winger wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Farid Musa ni kwamba, leo amefanyiwa vipimo vya afya ili kujua ufiti wake, Tenerife wamesema ikiwa atafanikiwa kufaulu vipimo hivyo, wangependa wamchukue kwa mkopo wa miaka miwili (2).
 Farid Musa ameongezewa wiki moja nyingine ya majaribio na Club Deportive Tenerife ya nchini Hispania ambako ameenda kusaka mafanikio ya soka la kulipwa nje ya Tanzania.
Yusuf Bakhresa ambaye yuko pamoja na Farid nchini Hispania, ameiambia www.shaffihdauda.co.tz kwamba inavyoonekana mpaka sasa Farid ananafasi kubwa ya kubaki kwenye klabu hiyo.