Thursday 28 April 2016

#YALIYOJIRI>>>Mwili wa Papa Wemba wawasili DRC.Fahamu zaidi hapa.

Mamia ya watu wamekusanyika leo nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan

Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous  alifariki dunia April 24 baada ya kuanguka jukwaani akiwa anatumbuiza huko Ivory Coast  
Papa Wemba anatarajiwa kuzikwa  siku ya Jumanne  ya wiki ijayo

0 comments:

Post a Comment