Wednesday 20 April 2016

Haya Ndio Maneno ya Kaka ake na marehemu Man katuzo Baada ya Tunda man kudaiwa Kuchukua vitu vya Marehemu.Fahamu zaidi hapa.

 MAREHEMU MANKATUZO ENZI ZA UHAI WAKE
 TUNDAMAN

PICHA YA GARI BAADA YA KUPATA AJALI
Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki
Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.
Baada ya Taarifa hiyo toka kwa tundaman tumsikilize kaka yake na marehemu man katuzo akiongelea inshu ya ajali na ya tundaman kuhusika na upotevu wa vitu vya marehemu

0 comments:

Post a Comment