Wednesday 27 April 2016

Mr Blue yupo kwenye dillema na anaomba ushauri wako. Ni kwasababu anadai wimbo wake Freedom aliomshirikisha Sugu umeporwa.Fahamu zaidi hapa.


Blue aliachia wimbo huo October mwaka jana na sasa Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini ameachia video ya wimbo huo akiwa peke yake baada ya kuinyofoa verse ya Blue na Kabayser imemuuma.
“Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli,” ameandika Blue kwenye Instagram.

“SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia. Sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu….????,”ameongeza.

Sugu ameshaachia video ya wimbo huo.

0 comments:

Post a Comment