Sunday 31 July 2016

#BREAKING NEWS>>>>JAMES LEMBELI ARUDI CCM KUTOKA CHADEMA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

*_Mhe Lembeli amerudi chama cha CCM hivi mchana wa leo katika mkutano mkubwa wa Mhe Mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli… Huko mjini Kahama. Anasema haoni sababu ya kwenda na “..safari ya uhakika isiyo na uhakika… kule hamna kitu.”_*

Irene Uwoya Asema Angeumudu ‘Ukuu’ wa Wilaya Kama Angepewa.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa filamu Irene Uwoya amefunguka kwa kusema kuwa kama angepata nafasi ya ukuu wa wilaya basi angefanya vizuri kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuongoza.

Irene Uwoyo

Muigizaji huyo ameimbia Bongo5 kuwa hakuwa na matarajio yakuteuliwa lakini kama angeteuliwa angeitendea haki nafasi hiyo.


“Mimi sijaomba wala sijawai kusema kama nataka hiyo nafasi, lakini kama ikitokea naiweza sana, nipo vizuri sana ndio maana hata nikathutu kugombea ubunge kwa sababu nilijua naweza kuongoza,” alisema Irene Uwoya.


Muigizaji huyo mahiri aligombea ubunge wa viti maalum Tabora lakini akakosa na kuhaidi kujipanga katika uchaguzi ujao.

Mama Diamond Anywea Kwa Zari Hassan.Fahamu zaidi hapa.

DAR ES SALAAM: Imevuja! Baada ya muda mrefu kusambaa kwa habari kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ‘haivi’ na mwandani wa msanii huyo, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’, imedaiwa kuwa kwa sasa bi mkubwa huyo amenywea kwa kumkubali Zari.


Taarifa hizo zilizopenyezwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia ya Diamond zimeeleza kuwa, hivi karibuni mama Diamond amesalimu amri na kutamka hadharani kuwa Zari ni kiboko kuliko wanawake wote ambao mwanaye amewahi kuwa nao.

“Mama Diamond kanywea kwa Zari na wala hana lolote la kusema, unajua Zari kamtuliza sana Diamond! Si kama alivyokuwa huko nyuma. Huwezi amini juzikati mama Diamond katamka kabisa kwamba hakuna mwanamke kama Zari maana amemtuliza Diamond vilivyo,” kilichonga chanzo hicho.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Risasi Jumamosi lilimpandia hewani mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo baada kuelezwa kila kitu bi mkubwa huyo alijibu kwa kifupi na kukata simu:

“Eeeh mwanangu…eee..”

Risasi Jumamosi liliendelea kumpigia simu mama Diamond baada ya kukata lakini hakuweza kupokea tena.

Zari na mama Diamond wamedaiwa kuwa katika msuguano wa chinichini kutokana na kutoelewana tabia na kila mmoja kutomzungumzia mwenzake kwa mazuri hivyo kwa mama Diamond kudaiwa kusema anamkubali mkwewe huyo, ni dhahiri kwamba amekubali yaishe! Chanzo.GBP

#YALIYOJIRI>>>Utajiri wa Dangote Washuka...Sasa Hayupo Katika List ya Matajiri Mia Duniani.Fahamu zaidi hapa.

Dangote

Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote, sasa anashika nafasi ya 104 kati ya matajiri duniani. Dangote ameshuka kwa mara ya kwanza kati ya matajiri bora 100 chini ya jua kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg billionaires ranking.

Bloomberg wamesema kwamba Dangote ameshuka sababu kubwa ikiwa ni kuporomoka kwa thamani ya pesa ya nchi ya Nigeria, Naira. Ambayo imeshuka kutoka 198 hadi 300, na inakadiriwa kupunguza karibu robo ya utajiri wa Dangote ambaye bado anawekeza vitega uchumi mbalimbali katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania.


Kulingana na ripoti hiyo ya Bloomberg billionaires, Dangote, aliyekuwa na utajiri wa dola za Marekani $15.4 billioni (Naira 3.05 trilioni) mwezi Machi mwaka huu mpaka sasa anamiliki utajiri unaofikia dola za Marekani bilioni 11.1 (Naira3.3 trillion), kwa maana tajiri kwa pesa za nchini kwao lakini maskini kwa pesa za dola ya Marekani.


Pamoja na kushuka kwake lakini bado kawazidi mabilionea wenye majina makubwa akiwemo mgombea uraisi wa Marekani, Donald Trump ($4.5) na msanii Oprah Winfrey ($3.1), anayetajwa kama mwanamke wa pili kwa utajiri duniani.


Kulingana na Jarida la Forbes la mwezi Juni 2015 ‘The World’s Billionaire’ rankings, mfanyabiashara huyo anamiliki utajiri unaokadiriwa kufikia $12.7 billion dollars na alikuwa akishika nafasi ya 51 miongoni mwa matajiri duniani na nafasi 71 ya watu wenye nguvu duniani.

#BURUDANI>>>Mwana FA ataja wasanii wake bora wa Hip Hop bongo.Fahamu zaidi hapa.

Mwanamuziki Mwana FA amefunguka na kuwataja wasanii wawili ambao yeye siku zote amekuwa akiwakubali kutokana na uwezo wao na kazi kubwa waliyoifanya katika muziki wa Hip Hop Tanzania.
Msanii Mwana FA akiwa na Mbunge wa jimbo la Mikumi Professor Jay

kiasi cha kuwafanya watu waamini muziki huo siyo uhuni bali ni kazi.

Mwana FA kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV alisema Professor Jay pamoja na marehemu Albert Mangwea ndiyo wasanii wake wawili bora wa siku zote katika muziki wa Hip hop Tanzania.

"Wasanii wangu bora kwa kipindi chote kwenye muziki wa Hip hop ni marehemu Albert Mangwea pamoja na Professor Jay hiyo nasema na kuna siku nilishawahi kuandika hilo, mpka Professor alinipigia simu na kuniuliza mzee una nini unataka kufa nini?. Watu hawajui tu huyu Professor Jay kwanza ndiyo mtu aliyefanya muziki wetu huu kwanza uanze kuheshimiwa, mwanzoni nyimbo zilikuwa na ujumbe wa fujo fujo fulani, kwa hiyo muziki wetu ulikuwa hauchukuliwi 'serious' lakini baada ya chemsha bongo kila kitu kikabadilika" alisema Mwana FA

Mbali na hilo Mwana FA alisema kuwa Professor Jay ni msanii ambaye alifanya yeye kidogo aache muziki sababu Mwana FA alikuwa anataka kufanya muziki bora lakini alipokuwa anasikiliza kazi za Professor Jay akaona hawezi kufanya kazi bora kama hizo.

"Unajua mimi siku zote huwa nataka kuwa best kwa kile nachofanya sijui kwa wasanii wengine, sasa baada ya kusikia ngoma ya Professor Jay 'Chemsha bongo' mimi nina nyimbo zangu nilikuwa nimeandika nikarudi nyuma nakajiuliza sasa mimi nawezaje kuwa 'best' kwa ngoma hizi? Yaani alinikatisha tamaa lakini nikarudi na kuanza kujipanga upya" alisema Mwana FA.

#MICHEZO>>>SAMATTA AENDELEA KUFUNIKA UBELGIJI APIGA BAO DAKIKA YA 90 NA KUIBEBA GENK.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta amezidi kuonyesha makali yake nchini Ubelgiji baada ya kuifungia KRC Genk bao muhimu lililoipa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Oostende.

Karelis ndiye alikuwa wa kwanza kufunga upande wa Genk, ilikuwa ni katika dakika ya 50, Samatta akaongeza katika dakika ya 90+1, yaani katika ile dakika moja ya nyongeza.

Bao hilo la Samatta limekuwa lililoibeba Genk kwa kuwa, Musona aliifungia Oostende bao dakika 90+3 ikiwa ni ya mwisho kabisa baada ya kuongezwa dakika tatu.

Kama ingekuwa bado wanaongoza kwa bao moja la Karelis, maana yake Genk wangeambulia sare ya bao 1-1 baada ya dakika 90.

#MICHEZO>>>Bayern munich na Manchester United zawa tishio.Fahamu zaidi hapa.

Bayern munich yafata mwenendo wa Manchester United baada ya hiyo jana,Man United kuifunga goli 5 timu ya Galatasaray kwa 2. Haya yafuatayo ni matokeo:-

Inter milan 1-4 Bayern munich
Icardi 90'

J.Green 7' 30' 35'
Ribery 12'


#MICHEZO>>>Wanacha wa SIMBA waongozwa na Agenda 10 za mkutano mkuu wa Simba leo.Fahamu zaidi hapa.

Wanachama wa simba sc wamejitokeza kwa Wingi leo katika ukumb wa Police mess kwa ajil ya mkutano mkuu leo wa mwaka 2016

Hii ndio List ya Agenda 10 za mkutano mkuu wa Simba leo.

#MICHEZO>>>>CHUJI ATUA KMC FC, LENGO NI KUIPANDISHA LIGI KUU, YACHUKUA WACHEZAJI MBEYA CITY, KAGERA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amezindua rasmi kikosi cha kuipandisha KMC FC katika Ligi Kuu  Bara na moja ya mambo aliyofanya ni kumkabidhi jezi yake kiungo mpya wa timu hiyo, Athumani Iddi ‘Chuji’.

Chuji ambaye ni nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Mwadui FC amejiunga na timu hiyo tayari kabisa kuhakikisha msimu uhao inapanda daraja.
Pamoja na Chuji wengine ambao wamesajiliwa na KMC FC ni Eric Mawala (kutoka Mbeya city), Issa Ngoah (Simba), Rashid Roshwa (Kagera Sugar), Lembele Jerome (Kagera Sugar) na Mussa Kidu (JKT Ruvu).

#MICHEZO>>>BAADA YA ZOEZI LA KUKWANGUA, VIFUSI VITAJAZWA ZAIDI ILI KUANZA UJENZI WA UWANJA HUU WA SIMBA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Uwanja wa Simba uliopo Bunju umeanza kukwanguliwa lakini imeelezwa kutamwagwa kifusi zaidi ya tani 100 tena.

Imeelezwa baad ya zoezi hilo, kitakachofuata ni suala la kusawazisha kabla ya kuanza kuwekwa kwa nyasi bandia.

 
Hivyo pamoja na zoezi la kuukwangua uwanja, inaonekana ndiyo mwanzo kabisa na zoezi bado.

Uongozi wa Simba umeanza kulifanyia kazi zoezi hilo takribani wiki sasa na mambo yamekuwa yakienda kimyakimya.


Taarifa za ndani zinaeleza, uwanja utakuwa ni kwa ajili ya mazoezi na baada ya hapo zitajengwa hosteli kwa ajili ya wachezaji kuweka kambi.

Halafu baada ya hapo kutakuwa na mwendelezo wa kuanza kujengwa majukwaa ya muda na mabadiliko yatafuatia kuwa majukwaa ya kudumu kulingana na uongozi ulio madarakani unatakaje.

TAZAMA PICHA JINSI LOWASSA ALIVYO ZUILIWA KUINGIA POLISI AKIWA NA MBOWE LEO HII.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia  na Maendelea (Chadema), Freeman Mbowe  leo july 31 amewasili makao makuu ya jeshi la polisi kuitikia wito wa kuhojiwa na jeshi hilo huku hali ya  usalama ukiwa imeimarishwa   kabla na baada ya Mbowe kuwasili .
 
Mbowe akiwa na msafara wa magari nane walikutana na ulinzi huo makali ambapo  magari ya Mbowe na Wakili Peter Kibatala ambaye alikuwa na Tundu Lissu ndio yaliruhusiwa kuingia. 

Gari la Edward Lowassa na viongozi wengine wamezuiwa kwenye geti la kuingia kituoni hapo ambapo geti hilo limezibwa na gari la maji ya kuwasha ili kutoruhusu gari yoyote kutoka au kuingia



#YALIYOJIRI>>>>>Lowassa Uso Kwa Uso na Nape Nnauye Wakati wa Kuaga Mwili wa Mwandishi wa Tanzania Daima.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga. 

Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.

Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini.

Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa.

Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga liwa katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakiamuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya kufika.
 Familia ya Marehemu Joseph Senga ikiwa ni yenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akizungumza.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza.

BAADA YA KUTOKA JELA HATIMAYE KOFFIE OLOMIDE APOST PICHA AKIWA NA MKEWE NA WATOTO WAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Embattled Congo musician, Koffi Olomide shares photo with his beautiful wife, Alaine

Didi Stone shared a photo of her embattled father, Koffi Olomide and mother, Alaine on Instagram moments ago. The 16-year-old captioned it: “My loves”
 
Meanwhile, the Congolese music maestro is a free man after spending two days of supposed 3-month jail term for assaulting one of his dancers at the Jomo Kenyatta International Airport, Kenya. He was released from prison on Thursday morning.

#YALIYOJIRI>>>Lowassa afunguka mengi Leo....Adai hakuna mwenye hati miliki Ya Nchi.Fahamu zaidi hapa.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowasa amemtaka Rais John Magufuli kuwa na utamaduni wa kufanya mazungumzo na wanasiasa wenzake ili kufikia muafaka wa mambo mbali mbali ya kisiasa nchini.

Lowasa ameyasema hayo leo wakati wa mahojiano na Tido Mhando kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni  ya Azam. Lowasa amesema kuwa siasa ni mazungumzo na siyo kutoa tu amri kama anavyofanya Rais Magufuli.

Kadhalika Lowassa amesema kila mtu ana wajibu wa kuheshimu amani ya nchi na hakuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii.

“Serikali haipaswi kuwa na ghadhabu, inapaswa kuwa na tabia ya kuzungumza. Sisi sote ni Watanzania kwa nini tunaogopa kuzungumza. Mazungumzo ndiyo njia bora ya kufikia maridhiano. Pia Rais Magufuli aitazame Zanzibar, tunasikia watu wanashughulikiwa kwa njia mbalimbali, wanakamatwa, hivyo hawezi kuikwepa Zanzibar kwani hilo ni suala lake.” alisema Lowassa.

Amesema CHADEMA ipo sahihi kutangaza operesheni ‘Ukuta’ hapo Septemba 1, mwaka huu na kwamba bado kuna nafasi ya kufanya mazungumzo kabla ya tarehe hiyo kufika ili kuepusha hali ya migogoro itakayojitokeza siku hiyo itakapofika.

Akizungumzia barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukemea operesheni hiyo, amesema barua hiyo imejaa ghadhabu zaidi kuliko kuongelea mambo ya msingi ambayo vyama vya upinzani vimekuwa vikionewa.

Akiongelea suala la wabunge wa upinzani kutoka na kususia bunge, Lowassa amesema hali hiyo ilisababishwa na kutokuwepo kwa Spika Job Ndugai ambaye kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi akiendelea na matibabu.

“Ndugai angekuwepo haya yote yasingetokea kwakuwa ni mtu makini sana na hata kwa Naibu Spika kuna tatizo la Kisaikolojia kwasababu aliingia bungeni kwa njia zisizoeleweka na hivyo kumfanya kushindwa kuhimili kiti vizuri,” amesema.

Hata hivyo amempongeza Rais Magufuli na kudai kuwa amefanya vizuri katika baadhi ya maeneo lakini kuna maeneo mengine ambayo angepaswa kuyapa kipaumbele zaidi akitolea mfano wa elimu na kudai kuwa badala ya kuanza na suala la madawati angeanza na kushughulikia maslahi ya walimu kwanza, na kutoa kipaumbele kwa tatizo la ajira nchini hasa kwa vijana.

Kuhusiana na harakati za Serikali kuhamia Dodoma, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu CHADEMA amesema viongozi wote waliotangulia tangu enzi za Mwalimu Nyerere walikuwa na ndoto za kuhamia Dodoma lakini kuna mambo yaliyokuwa yanaingilia mipango hiyo na mwisho kushindikana.

“Napongeza harakati na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Serikali yote Dodoma lakini napenda kuwaambia wasiende kwa kasi sana wasije wakavunjika miguu,” ameongeza.

Kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, Lowassa ametoa rai kwa Rais Magufuli aangalie hali ya Zanzibar kwani yanayoripotiwa kuendelea visiwani humo yanatia kichefuchefu ikiwemo watu kukamatwa na kuteswa.

“Tusiitenge Zanzibar na badala yake juhudi za makusudi zifanyike kuweka mambo sawa kwa kufanya mazungumzo kwani siasa ni mazungumzo,” amesisitiza Lowassa ambaye amedai kuwa ana matumaini makubwa ya kuingia Ikulu mwaka 2020.

Kuhusu kashfa ya Richmond kumfanya aondoke CCM kwa hasira baada ya kukosa ridhaa ya chama hicho katika kugombea Urais, Lowassa amesema hakuondoka CCM kwa hasira isipokuwa alituhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

“CHADEMA sikujipeleka mwenyewe bali Kamati Kuu CHADEMA ilinifata na kuniomba nijiunge nao katika kupeperusha bendera yao na mimi niliona ni ‘opportunity’ nzuri hivyo nikakubali nikajiunga nao na tukafanikiwa kupata kura zaidi ya milioni sita, idadi ambayo siyo ndogo hata kidogo,” amejinasibu Lowassa.

#Live>>>>Mahojiano ya Edward Lowassa na Tido Mhando.Fahamu zaidi hapa.

Saturday 30 July 2016

#MICHEZO>>>Man United yaendelea kuwa tishio michezo ya kirafiki baada ya hii leo kuichapa goli 5 timu ya Galatasaray.Fahamu zaidihapa.

Man United 5 - 2 Galatasaray

Ibrahimovic 4'
Rooney 55' 58' (Pen)
Fellain 62'
Mata 75'

Gumus 22'
Bruma 41'

#MechiYaKirafiki #