Friday 22 July 2016

#YALIYOJIRI>>>Ripoti ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam Baada ya Kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa silaha......Pia Wamezungumzia Kiasi Walichokusanya Ndani ya Siku 6.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa sugu 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Aidha pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi hilo pia wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210, na misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Katika hatua nyingine ,kikosi cha kupambana  na wizi wa simu cha polisi kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote wakazi wa jijini  Dar es salaam.

Hata hivyo kamanda Sirro aligusia  zoezi zima la uhakiki wa silaha na kusema kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna changamoto kadhaa zilizojitokeza

Kamanda  Sirro amesema  idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa wilaya zote tatu ni 11,602 na jumla ya silaha 14107 zilihakikiwa.

Pia kasema Jumla ya silaha 66 zilisalimishwa kutokana sababu mbalimbali ikiwamo mmiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu silaha. Zoezi la uhakiki wa silaha limeiingizia Serikali mapato kiasi cha Mil 198.8

Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es salaam limeweza kujikusanyia kiasi  cha shilingi 562,860,000/= kutokana na ukamataji wa makossa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar 15/7/2016 hadi 21/7/2016.
  1.    Idadi Ya Pikipiki Zilizokamatwa  -1,413
  2.      Idadi Ya Magari Yaliyokamatwa  –17,349
  3.      Daladala Zilizokamatwa           -7220
  4.      Magari Mengine (Binafsi Na Malori)- 10,129
  5.      Jumla Ya Makosa Yaliyokamtw-  18,762
6. Bodaboda Waliofikishwa Mahakamani Kwa Makosa Ya Kutovaa Helmet Na Kupakia Mishkaki   ni 49

0 comments:

Post a Comment