Friday 22 July 2016

#MICHEZO>>>SAMATTA ATUPIA PENATI GENK IKISONGA MBELE EUROPA LEAGUE.Fahamu zaidi hapa.

Usiku wa Julai 21 Genk ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabili timu ya Buducnost kwenye michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi ya michuano ya Europa League.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa kwa Genk kufungwa bao 2-0, ilibidi umauliwe kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza kumalizika kwa matokeo ya 2-0 yaliyosabaisha matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2.

Ikumbukwe mchezo wa awali (Julai 14) takriban juma moja lililopita Genk ilipata ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani huku Samatta akifunga bao la pili.

Samatta akicheza kwa dakika zote 120, alifunga moja ya penati ambazo ziliisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Mikwaju ya penati kwa upande wa Genk ilifungwa na Dries Wouters, Mbwana Samatta, Bryan Heynen na Thomas Buffel na kuvusha Genk kwenda raundi ya pili kwa jumla ya penati 4-2.

Genk itapambana na klabu ya Cork City kutoka Jamhuri ya Ireland katika raundi ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza Europa League hatua ya makundi.

0 comments:

Post a Comment