Tuesday 26 July 2016

#MICHEZO>>>Charles Boniface Mkwasa atangaza kikosi cha Taifa Stars kuikabili Nigeria.Fahamu zaidi hapa.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini Julai 30 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Nigeria unatarajiwa kuchezwa mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Mkwasa amesema ametoa nafasi kubwa kwa wachezaji vijana ili kuwapa uzoefu lakini ameongeza kuwa, atahitaji wachezaji wote kwasababu licha ya mechi hiyo kutokuwa na umuhimu wowote kwa timu zote mbili, lakini bado inaumuhimu linapokuja suala la kupanda katika viwango vya FIFA.

Kambi itaanza August 1-5 lakini wachezaji watatakiwa kuripoti kambini Julai 31 kwenye kambi ambayo itatajwa hapo baadaye

Wachezaji wote wa wanaocheza soka nje ya nchi wataungana na timu moja kwa moja Nigeria na baada ya mchezo huo watarejea tena kwenye vilabu vyao.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kilichotangazwa kwa ajili ya kambi ambayo inatazamiwa kuanzia August 1 hadi 5 mwaka huu.

MAKIPA
Deogratius Munish, Beno Kakolanya (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC)


WALINZI
Oscar Joshua,  Kelvin Yondani, Juma Abdul (Yanga SC), Erasto Nyoni, Agrey Morris (Azam FC) Mohamed Hussein (Simba SC).


VIUNGO
Farid Musa, Himid Mao (Azam FC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude (Simba SC), Ibrahim Rajab ‘Jeba’ (Mtibwa Sugar FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Simon Msuva, Juma Mahadh (Yanga SC).


WASHAMBULIAJI
Joseph Mahundi (Mbeya City), Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate (Simba SC), John Bocco (Azam FC) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

0 comments:

Post a Comment