Monday 25 July 2016

#MICHEZO>>>>MAN UNITED YAONDOKA CHINA BAADA YA MECHI YAO VS MAN CITY KUAHIRISHWA.Fahamu zaidi hapa.

Kikosi cha Manchester United kimeondoka Beijing nchini China baada ya mechi yao dhidi ya Man City kuahirishwa.



Mechi ya Man United dhidi ya Man City ilikuwa ipigwe leo lakini ubovu wa Uwanja wa Bird Nest ulioharibika kutokana na mvua za mfululizo ilisababisha mechi hiyo kuahishwa.



Man United wameondoka Beijing wakiongozwa na kocha wao mpya, Jose Mourinho ambaye ameikosa mechi hiyo dhidi ya mpinzani wake mkubwa, Pep Guardiola anayeinoa Man City.



MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED:

Julai 30 - Manchester United vs Galatasaray, Gothenburg, Sweden

Agosti 3 - Manchester United vs Everton, Old Trafford


Agosti 7 - Manchester United vs Leicester, Community Shield, Wembley

0 comments:

Post a Comment