Tuesday 31 October 2017

Wabunge Acheni Kuwashwa Washwa na Kufanya Mambo ya Umbea- Ndugai.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu , na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea.

Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News: Zitto Kabwe Aachiwa kwa Dhamana Akamatwa Tena.

Saa chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kukamatwa na Jeshi la Polisi  na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe Dar es salaam, aliachiwa kwa dhamana lakini amekamatwa tena na kupelekwa kituo cha Polisi cha Kamata kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Katibu na itikadi na uenezi wa ACT WAZALENDO amesema “baada ya kukamatwa tena amepelekwa kwenye kituo cha Polisi Kamata, hatufahamu ni sababu gani zilizofanya akakamatwa tena, tuna tafsiri kama Chama mwenendo wa sasa wa kumshughulikia Zitto ni kujaribu kumnyamazisha“ 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Profesa Jay Atupa Dongo Hili “Mkimaliza Hoja Yenu Mfu ya Ufisadi Muwatimue Mapema Msisubiri Waondoke Wenyewe".

Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametoa ujumbe unaoonekana kama ushauri kwa vyama vya siasa huku ukilenga matukio ya hivi karibuni ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Katika Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Profesa Jay ameandika “Mkimaliza hiyo HOJA yenu Mfu ya UFISADI, leteni tuhuma za wote waliobaki huko na Muwatimue mapema msisubiri waondoke wenyewe... TUMEELEWANA”?
Ujumbe huu wa Profesa Jay umekuja ikiwa ni chini ya saa 24 toka Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge pamoja na nyadhifa zingine ndani ya chama ikiwemo kujivua uanachama.
Kwa upande mwingine ujumbe huo umechukuliwa kama jibu kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kilijibu suala la Nyalandu kuhama kwa hoja ya kuwa ni miongoni mwa wanachama wengi wasio waadilifu ambao wameamua kuondoka kabla ya Panga kuwafikia.
Hata hivyo Profesa Jay amegoma kufafanua undani wa ujumbe huo iwapo umelenga kupuuza hoja hiyo ya Ufisadi. Awali Profesa Jay aliandika ujumbe wa kumpongeza Nyalandu kwa uamzi wake na kumkaribisha Chadema. “Hongera sana my brother Lazaro Nyalandu kwa Ujasiri na kusimamia kile unachokiamini!! KARIBU SANA KIUMENI SPEAK YOUR MIND”, aliandika Profesa Jay.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mtandao wa WhatsApp Waruhusu Kufuta Ujumbe,Picha Uliotuma kwa Mtu Usiyemkusudia.

Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo.

WhatsApp is rolling out the Delete for Everyone (Recall) feature for all users! 🎉https://t.co/3bnbgxtPvU

— WABetaInfo (@WABetaInfo) October 26, 2017

WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa.



Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia.

Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart  ndani ya mwaka huu.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makubwa manne ndani ya mwaka huu ambayo yataifanya programu ya WhatsApp kuwa ya kisasa zaidi.

Twambie wewe mtumiaji wa programu pendwa ya WhatsApp umeyapokeaji mabadiliko haya. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Monday 30 October 2017

Hatimaye Mmoja wa Watoto Pacha Waliotenganishwa India Afungua Macho.

Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India.
Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake.

Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha.
Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa,
Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus.

Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hizi Hapa Faida na Maajabu Yanayotokana na Kunywa Maji ya Uvuguvugu Kila Asubuhi.

Inawezekana unatumia kikombe cha chai  au kikombe cha  kahawa kila siku asubuhi, wengi wao hutumia maji ya kawaida ili kuanza siku vizuri. Hivi vitu vimekuwa
ndio tabia ya kila siku , hata hivyo wachunguzi wanasema kunywa maji ya uvuguvugu  asubuhi wakati tumbo halina kitu unapata faida  za kiafya zaidi.

Madactari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu   yaliotiwa  liau au ndimu ili  kupunguza radical ndani ya mwili. Kutumia maji ya moto  inaongeza na kufungua utumbo ili kukufanya wewe upate haja kubwa kwa urahisi.
Na hapa kuna faida 7  za vitu vinavyotokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi.

1.Yanasaidia kuondoa Mikunjo.

Kunywa maji inakusaidia usizeeke mapema,hakuna mtu anaependa kuzeeka mapema.hata hivyo  sumu ndani ya mwili inaweza kukufanya uzeeke mapema. Wakati mwili wako unapotoa sumu  utapunguza magonjwa   na uzee. Maji ya  moto usaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa. Zaidi sana  yanasaidia kurejesha cells za ngozi iwe inaonekana kuvutia na nyororo.

2.Huepusha maumivu.

Dawa ya nguvu  ya kutegemea kupunguza maumivu wakati wa hedhi ni maji ya moto, yanafanya misuli ya tumbo  irelax  na kupungua kwa maumivu. Maji ya moto husaidia mzunguko kapirali  na misuli katika mwili pia.

3.Yanasaidia kupunguza uzito.

Inawezekana unajaribu kupunguza uzito  na umesikia kuwa maji ya moto asubuhi yanaweza kuwa ni msaada mkubwa kwako. Hii ni kweli., maji ya moto yanaongeza joto la mwili, ambalo  linabadilisha ongezeko la  kiasi cha metabolic, kuongezeka kwa metabolic  mwili unakuwa na uwezo wa kuchoma carories siku nzima.

Kama ukianza na kunywa maji ya moto yenye limau. Utausaidia mwili wako kuvunja vunja mafuta  yalioko ndani.

4.Yanaboresha digestion.

Unapokunywa maji ya moto asubuhi unastimulate  digestion yako  na  kuusaidia mwili kuwa na digestion bora. Kunywa maji ya baridi ya ya kula chakula inaweza kusimamisha digestion yako, na mwili wako ukawa  na matatizo, maana maji yabaridi yana gandisha mafuta yalioko kwenye chakula na kufanya digestion iwe ngumu kwako. Ni bora ukatumia maji ya moto kuliko ya baridi.

5.Yanaboresha mzunguko wa damu mwilini.

Kunakuwa na mlimbikizo wa  mlolongo wa nervous na mlimbikizo wa mafuta mwilini , lakini unapotumia maji ya moto yanaenda kuondoa hio migandanizo. Hii process inaflash sumu yote  ndani ya mwili na kuufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri na kufanya misuli kupumzika.

6.Inasaidia Usivimbilwe.

Watu wengi wamekuwa wakivimbiwa na kujisikia vibaya kutwa nzima na hata kwenda kwa dactari kwa ajili ya matibabu, kuna wengine  husaidiwa kwa kupigwa   bomba ili kupata nafuu , hata kuanza kutumia dawa mbalimbali.

Ukianza kutumia maji ya moto asubuhi kabla ya kula kitu chochote utasaidia  movement  yote. Hutasikia kuvimbiwa wala kushindwa kupata haja kubwa. Utapata kwa raha mstarehe.

7.Yanakufanya Upate Usingizi Vizuri.

Unapotumia maji ya moto  wakati wa chakula cha usiku, na kabla ya kwenda kulala, utaufanya mwili wako kurelax na  kulainisha nerves zako. Hii itakufanya ulale vizuri na kuwa na utashi mzuri kwa ajili ya kuamka asubuhi.

Tumeona  faida 7 za kushangaza   ambazo zinaweza kutokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi na jioni . Anza sasa kutumia maji ya moto kila siku ili uone faida  nzuri  tulizosoma hapo juu kwa ajili ya manufaa yako .

Mimi nimeanza  kujaribi na nimeona kuna faida, anza na wewe leo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mbivu Mbichi Leo Hatima ya Ubomoaji Mjengo wa Mchungaji Getrude Rwakatale.

HATIMA ya ubomoaji wa nyumba ya kifahari ya Mchungaji wa kanisa la TAG Mikocheni, Getrude Rwakatare, inatarajiwa kuanza kujulikana leo wakati Naibu Waziri mpya wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola atakapotoa ripoti.

Wiki iliyopita Lugola aliomba Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kumpatia taarifa ya kukwama mwaka jana kwa ubomoaji wa 'hekalu' hilo lililopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Rais John Magufuli alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Oktoba 7 ambapo miongoni mwa sura mpya ni Naibu Waziri Lugola ambaye amechukua nafasi ya Luhaga Mpina aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

"Taarifa tayari ipo ofisini kwangu (tayari) nitaipitia Jumatatu (leo)," alisema Lugola ambaye alikuwa kwenye ziara mikoani wakati akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki. "Umma unataka kujua, hivyo siyo jambo la kucheleweshwa."

"Niliagiza nipatiwe taarifa ya tangu (sakata) ilivyoanza ili nijue ugumu (wa kubomoa) umetokana na nini halafu nitakwenda kushauriana na waziri wangu kile kilichojiri katika hiyo taarifa."

Mwanasheria wa NEMC, Heche Suguta alithibitisha kutekeleza agizo la naibu waziri kwa kuwasilisha taarifa ya jengo hilo liliopo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 ofisini kwake.

"Siwezi kuzungumza chochote lakini alichokitaka waziri wangu tulitekeleze kabla ya muda aliotupatia," alisema Suguta ambaye pia alikuwa msimamizi mkuu wa bomoabomoa hiyo. "Tayari tumefanya hivyo."

Mchungaji Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kwa kipindi cha pili, alihamia katika hekalu hilo Agosti 30, 2012 ambapo taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema waumini wa kanisa lake wapatao 300 walifika kushuhudia sherehe ya uzinduzi wa nyumba hiyo.

Nyumba hiyo ni moja kati ya 8,000 zilizokuwa zibomolewe mwishoni mwa mwaka 2015 katika operesheni maalum ya kuondoa makazi kwenye fukwe, kingo za mito, maeneo ya wazi na mabondeni.

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Wakala wa Misitu (TFS) iliweka alama ya X kwenye kuta za nyumba hiyo wakidai imo katika hifadhi ya Bahari ya Hindi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria, na kwamba pia imejengwa kwenye hifadhi ya mikoko.

Iliachwa baada ya mchungaji huyo kwenda mahakamani kufungua kesi ya kusimamisha zoezi hilo akipinga madai kuwa imejengwa ndani ya mita 60 kutoka fukwe ya bahari.

Aidha, mmiliki huyo alidai ujenzi wa nyumba hiyo ulishajadiliwa na kesi yake kuhukumiwa na Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi ambayo ilimuona Mch. Rwakatare hakuvunja taratibu zozote za ujenzi. Hukumu hiyo ilitolewa Mei 22, 2015.

Dk. Rwakatare, ambaye pia alikuwa mbunge wa viti maalumu kwenye Bunge lililopita, alipoteza nyumba nyingine nne zilizokuwa kwenye kiwanja namba 314 Mbezi Beach baada ya kubomolewa kwa tuhuma za kuvamia eneo hilo. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu.

12 Government Jobs, Ministry of Finance and Planning

2 Jobs at KNCV Tanzania

Job at Dodoma Christian Medical Center (DCMC), Pharmaceutical Technician

5 Jobs at Karatu District Council

Job Opportunity at UNHCR, CRR Officer

Job at Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC)

Internship Opportunities at Mwananchi Communications Limited

3 Job Opportunities at BBC

Nafasi zingine ingia

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Zitto Kabwe Yamemfika Hapa Aitaka Chadema Kuunganisha Nguvu Ili Kuing'oa CCM.

Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amevitaka vyama vingine vya upinzani ikiwemo CHADEMA, kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanaing'oa CCM kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani.

Zitto Kabwe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi huo, na kusema kwamba wamegundua iwapo wataunganisha nguvu na kuachiana baadhi ya kata, watafanikisha kukitoa chama cha CCM, na hatimaye kutimiza malengo yao ya kushikilia kata hizo.

"Iwapo vyama vyote vya upinzani vikituachia sisi kugombea kata za Kijichi tutaishinda CCM, na iwapo sisi tukiwaachia kata ya Mbweni wataishinda CCM, tunaomba wenzetu tuweke nguvu ya pamoja, tushinde Kijichi na Salanga, tumefanya utafiti tumeona tuna nafasi kubwa ya kushinda Kijichi, tuna nafasi kubwa ya kugawa kura na wenzetu Mbweni”, amesema Zitto kabwe

Zitto Kabwe ameendelea kusema kwamba ...”Tunawaambia wenzetu kupitia nyie, tuna adui mmoja tu CCM, tuache majivuno, ushirikiane, na sisi tumeonyesha 'good faith' tumewaachia Mbweni, tunawaomba wa-extend hiyo good faith, na wakihitaji maada tutawasaidia, ili kwenye kata zote zinazofanya uchaguzi Dar es salaam CCM ishindwe”.
Hivi karibuni kunatarajiwa kufanyika chaguzi ndogo ndogo za madiwani katika maeneo mbali mbali nchini, kwa mujibu wa sheria na katiba za nchi. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Breaking News>>>Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema

Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia (CCM) kwa kile alichodai hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini.

Taarifa ambayo ameitoa leo Nyalandu amesema kuwa ameamua kuachana na CCM na sasa anaomba kuungana na CHADEMA kama watapendezwa na yeye kujiunga huko.
Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
halikadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa" aliandika Nyalandu
"Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA" alisisitiza
Mbali na hilo amesema kwa sasa anafikiria kujiunga na CHADEMA kama watakuwa tayari
"Mimi naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
Hivyo, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
"nimemua kujiuzulu kiti Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI" 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Friday 27 October 2017

Madaktari watenganisha pacha walioshikana vichwa.

Pacha walioshikana kichwani Jaga na Kalia

Madaktari wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameshikana katika kichwa.

Wavulana hao wa miaka miwili Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi ICU, kulingana na madaktari.

Kundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.

Wavulana hao walizaliwa wakiwa na wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Randeep Guleria aliambia vyombo vya habari vya India kwamba siku 18 zijazo zitakuwa muhimu ili kuthibitisha ufanisi wa uchaguzi huo.

Pacha hao wanaotoka katika kijiji cha mashariki cha jimbo la Orissa walikuwa wameshikana katika kichwa, hali inayoitwa 'craniopagus'. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tanesco Yafunguka Tatizo la Kukatika Umeme Ghafla.

Tunaomba radhi wateja wetu
Imetokea hitilafu gridi ya taifa na kusababisha umeme eneo lote la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa kukosa umeme.

Tatizo hili linashughulikiwa na umeme utarudi baada ya muda mfupi

=======

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRIDI YA TAIFA​

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa majira ya Saa 12:30 imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na kusababisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Jitihada zimefanyika ili kurejesha umeme na baadhi ya Mikoa imeshaanza kupata huduma ya umeme

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

25/10/2017

=======
UPDATE: Oktoba 26, 2017

Tunapenda kuwataarifu Wateja wetu waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 majira ya Saa 12:03 Asubuhi imetokea hitilafu tena kwenye Gridi ya Taifa na kusabisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Mafundi wanafanya jitihada usiku na mchana ili kuhakikisha hali hii haijirudii na umeme unarejea katika hali ya kawaida kwa haraka

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi...

TANESCO 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa