Monday 28 December 2015

#HABARI>>>Diamond Amwaga Machozi Ukumbini.Fahamu zaidi hapa.

Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.

Tukio hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.

Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.

Wakati akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza gemu la Bongo Fleva vibaya.

Hata hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.

Kufuatia hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia machozi kaka yake huyo.

Diamond alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen, meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake. Kwa hiyo anyamaze.

Licha ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara ndani yake.

“Huna sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.

Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!

Kilio hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku hiyo katika kumbukumbu.

Sunday 27 December 2015

Angalia Video mpya Ommy Dimpoz - Achia Body.Hapa hapa.


Angalia Video ya Diamond Platnumz - Utanipenda.Hapa hapa.


#MICHEZO>>>Bondia Thomas Mashali amchapa Francis Cheka kwa pointi mjini Morogoro katika pambano la raundi 10, uzito wa Kg 77.Fahamu zaidi hapa.

Bondia Thomas Mashari amchapa Francis Cheka juzi kwa pointi mjini Morogoro katika pambano la raundi 10, uzito wa Kg 77.
Majaji wamempa Mashari pointi 94, 96 na 97 wakati mwenyeji Cheka amepata pointi 96, 93 na 93

#YALIYOJIRI>>>Baada ya Askofu Gwajima Kumkana Lowassa, Dkt. Slaa Amtaka Awaombe Radhi Maaskofu pamoja na Watanzania Kwa Kusema Uongo.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya Askofu Gwajima kusema kuwa hakuwa akimuunga mkono Lowassa, Dkt. Slaa amemtaka awaombe radhi Maaskofu pamoja na Watanzania kwa kuwadanganya. 
 
Amesema hakutegemea Askofu Gwajima kumkana hadharani Lowassa

======Hili ni Tamko la Dr. Slaa======
 
i) Ni muhimu kwa "Mshenga Gwajima" kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
 
ii) Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na " Mabadiliko" ya " Kuzungusha Mikono". Mshenga na UKAWA yake walitaka kutuaminisha sote kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa "Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko".

Lowassa aligeuzwa kuwa "Ajenda" badala ya ajenda za Msingi za Wananchi. Mungu amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru sana Mungu aliyenionyesha kuwa kati ya wawili hao, japo wote kila mmoja ana uchafu, Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa "mjini" na makuwadi kwa ulaghai na upotoshwaji uliopitiliza.

iii) Nilimtaka Gwajima awaombe radhi Maaskofu aliosema "wamehongwa na Lowassa na kuwa fedha hizo waligawiwa mbele ya Mavho yake.
 
 Alisema bila kumumunya maneno, kuwa.... Maaskofu wa ki lutheri alikwisha malizana nao" na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 wamehongwa Maaskofu 30 na kumtaja kwa jina Askofu Mkuu mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za kununulia gari la kiaskofu." 
 
Fedha hizo alidai zimetolewa na Lowassa kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli toka tena hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe Radhi hadharani Maaskofu hao kwani kauli hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu na kuwachafua.

Lakini, alitamka hayo akiona ni sifa, ndiyo maana nilimshangaa kiongozi wa dini ambaye badala ya kukemea anaona ni sifa. Kama wenzangu waliokuwepo na wao wana Misingi ya kusimamia basi watatoa ukweli wao, na kama wanachukia ufisadi basi watatoka hadharani kukemea tamko hilo lililotolewa mbele yetu watu 4 akiwemo Mshenga.

Nilipotamka hivi wengi walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu "Wamehongwa". Kama Askofu anaweza kufika mahali akawasingizia wenzake ni hatari sana na halihitsji kufungiwa Macho na masikio. 
 
Kama anavyosema Gwajima ni " kweli". Basi wote tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na wale tunaotegemea kusimamia maadili katika Jamii yetu.
 
Wako walioniambia Dr. Slaa unapata wapi ujasiri wa kuwasema viongozi wa dini. Sijawahi kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli utatamkwa hata kama ni mchungu, na uovu na uozo utasemwa tu hata kama umetendwa na nani. Ukitazama nyuso za wazi " haki haitatendeka milele.

iv) Katika busara ya kawaida, hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana Lowassa" hasa kabla ya kuomba radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube na mitandao mbalimbali ziko bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi asiye na dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba radhi.

v) Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana "bifu" binafsi na Gwajima. Ni kweli kibinadamu nimeumia sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki mkubwa na kupoteza nguvu zao nyingi na labda "kupoteza fursa ya kuiondoa CCM kwa muda mrefu ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki ndicho kinachonisukuma zaidi kuendelea kumkaba Gwajima hadi atakapoomba radhi kwa watanzania wanyofu.

Nawaomba Watanzania tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize tena Kauli mbalimbali alizozitoa Gwajima, tena wakati mwingine kwa njia ya Maombi kwa jina la Mungu. Hali hii isipokemewa kwa ukali sana ni hatari sana.

Ndugu watanzania wenzangu,pamoja na yote haya, ninawatakia Heri nyingi kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2016 uwe wa Baraka na mafanikio.
-Dk Willibrod Slaa

#YALIYOJIRI>>>Mrithi wa Dk Slaa CHADEMA Kujulikana Mwezi Ujao.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema mchakato wa kumpata katibu mkuu wake utaanza mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, ndiye mwenye jukumu la kupendekeza jina la Katibu Mkuu na kulipeleka katika Baraza Kuu kupigiwa kura, kisha kupitishwa.

Tangu Agosti 3, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Willibrod Slaa alipumzishwa na Baraza Kuu baada ya kutofautiana na Kamati Kuu baada ya chama hicho kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu ndiyo anakaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk Slaa.

Mchakato wa kumpata Katibu Mkuu umeanza kuibua hali ya sintofahamu, huku majina mbalimbali ya vigogo wa chama hicho yakitajwa, likiwemo la Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye ambaye hivi karibuni alitangaza rasmi kujiunga na Chadema.

Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5 inasema; (b) nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa kufanya uteuzi mpya katika muda usiozidi miezi mitatu tangu nafasi kuwa wazi, (c) muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu 6.3.5 (b) hautazidi mwaka mmoja (d) bila kujali sharti la kifungu 6.3.5 (c) hakutafanyika uchaguzi rasmi wa kuziba nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya uchaguzi mkuu wa kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.

Akizungumzia mchakato huo, Mwalimu alisema Baraza Kuu litakutana mapema Januari mwakani, kujadili masuala mbalimbali, likiwamo la kumpata Katibu Mkuu.

“Si kama chama kimekaa muda mrefu bila Katibu Mkuu. Yupo anayekaimu na kinachofanyika sasa ni kumpata Katibu kamili.”

“Baraza Kuu lilikutana litajadili suala hilo kwa kina na kuja na mapendekezo mbalimbali,” alisema Mwalimu na kusisitiza kuwa kila jambo litafanyika kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.

Alisema uongozi wa muda ndani ya chama hicho hauwezi kuzidi mwaka mmoja na nafasi ya kuteuliwa muda wa kukaa wazi hauzidi miezi mitatu kabla ya kuteuliwa kiongozi mwingine.

MATOKEO YA LIGI KUU UINGEREZA YAKO HAPA.


#MICHEZO>>>Atima ya Louis van Gaal ipo matatani ndani ya Manchester United.Fahamu zaidi hapa.

 HAYA CHINI NI MATOKEO YA MCHEZO WA JANA KATI YA Stoke City NA Manchester United AMBAPO Manchester United IMEPOKEA KICHAPO CHA MAGOLI MAWILI HUKU KOCHA WA Manchester United Louis van Gaal AKIENDELEA KUJIWEKEA MAZINGIRA MABAYA KATIKA AJIRA YAKE AKIWA AMEFUNGWA MICHEZO MINGI KWA MFULULIZO,HUKU SWALA HILO LA KUFUNGWA MICHEZO MINGI AKIACHIWA KOCHA WA ZAMANI WA Manchester United SIR ALEX FAGASONI.
Memphis Depay maskini kujihami mbizi kichwa, na kujaribu kupata mlinzi David de Gea, inaruhusu Glen Johnson mraba kwa Bojan
Bojan Krkic slides nyumbani kwa njia ya kukata tamaa United ulinzi kuweka Stoke mbele baada ya dakika 19 juu ya Boxing Day.

#HABARI>>>Rais Magufuli Akutana na Dkt. Shein Ikulu Dar-es-salaam.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu Jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpa taarifa Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko Tanzania Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.

Rais Shein amesema mazungumzo juu ya hali ya Zanzibar yanaendelea chini ya kamati maalum ambayo yeye ndiye mwenyekiti na wengine wakiwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Rais Mstaafu wa awamu ya tano wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour.

Amesema tayari kamati hiyo imeanza mazungumzo tangu tarehe 09 Novemba, 2015 na kwamba mazungumzo hayo yamelenga kujadili hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.

Rais Shein amebainisha kuwa mazungumzo hayo bado yanaendelea.

"Kwa hiyo nimekuja kumpa taarifa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya mazungumzo yetu ili aweze kujua kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake, na sisi ni jukumu letu kumpa taarifa hiyo" Alisema Rais Shein.

Aidha Rais Shein ameongeza kuwa mazungumzo hayo yatakapokamilika wananchi watajulishwa.

MAGAZETI YA JUMAPILI YA LEO DECEMBER 27 YAKO HAPA.


Friday 25 December 2015

#YALIYOJIRI>>Rais Magufuli Ashiriki Misa Ya Krismasi Kanisa La Mtakatifu Peter Jijini Dar Es Salaam Leo.Fahamu zaidi hapa.

 Rais Dk Magufuli na Mkewe wakiwa na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo baada ya Ibada yaKrismas
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyemkaribisha kusalimia wananchi bada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.

#YALIYOJIRI>>>Serikali Kuvunja Nyumba ya Waziri Mkuu wa Zamani Fredrick Sumaye.Fahamu zaidi hapa.

WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, ameingia matatani baada ya kudaiwa kuvamia eneo la wazi na kuanza kuzungushia uzio, bila kufuata sheria na utaratibu wa ujenzi.

Eneo hilo la kiwanja namba 719/1/3 lililopo Mkiocheni, mtaa wa TPDC, lilikuwa likitumika kwa ajili ya michezo, mikutano ya kisiasa, pamoja na mikusanyiko mbalimbali ya kijamii.

Kufuatia tuhuma hizo, timu ya maofisa ardhi inachunguza uhalali wa umiliki wake, hivyo wiki ijayo majengo yaliyojengwa kwenye eneo hilo yatavunjwa, endapo itathibitika alifanya uvamizi huo.

Mbali na Sumaye, vigogo wengine wanaodaiwa kuvamia kiwanja hicho ni aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais, Philemon Luhanjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Rungwe, Saul Amon, ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya S.H. Amon.

Awali kabla ya kuvamiwa kwa eneo hilo, ilielezwa kuwa iliyokuwa kampuni ya High Precision Technology Centre (HPTCMatsutisha), ilitumika kulilinda lisivamiwe miaka ya 1970.

Hivyo mikusanyiko mbalimbali za kimichezo, pamoja na shughuli za kisiasa ilikuwa ikifanyika katika kiwanja hicho, ambako hata baada ya kampuni hiyo kufa, ililiendelea kutumika kwa shughuli za kijamii.

Taarifa zinaarifu kuwa, Sumaye anaendelea na ujenzi katika eneo hilo bila kuweka kibao chenye kuonyesha wakandarasi wanaohusika na ujenzi huo.

Lakini pia, licha ya  baadhi ya nyaraka kudai kuwa kiongozi huyo mstaafu analimiliki eneo hilo kuanzia mwaka 1998, hajawahi kulalamika kimaandishi kwenye uongozi wa mtaa kuhusu shughuli zilizokuwa zikiendelea kwenye eneo hilo.

Shughuli hizo ni pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa kuweka kifusi, ili kusawazisha eneo hilo kuufanya uwanja utumike vizuri kwa ajili ya michezo.

Aidha wiki tatu zilizopita, Ofisa Mtendaji wa Mtaa huo Mwanaidi Omary, aliongozana na mmoja ya maofisa wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni hadi kwenye eneo hilo.

Ofisa huyo wa ardhi alitoa notisi ya mdomo na sio ya maandishi ya kusitishwa ujenzi huo akidai mpaka mmiliki awasilishe nyaraka serikalini.

Licha ya ujenzi huo kufanyika bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo kutokuwepo kwa kibao kinachoonyesha mkandarasi anayehusika na ujenzi, lakini ofi sa huyo hakuchukua hatua zozote za kisheria.

Katika kutaka kujua ukweli wa mzozo huo,  barua iliyoandikwa na serikali ya mtaa kwa Halamashauri hiyo kuhoji ujenzi huo imepatikana. Barua hiyo yenye kumbukumbu namba MKT/SER/MT/ TPDC/05/2015, iliyoandikwa Desemba 11, mwaka huu na kupokelewa Desemba 14, bado haijatolewa ufafanuzi na mkurugenzi kama ilivyokuwa ikielekeza.

Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema serikali itavunja uzio na shughuli za ujenzi zinazoendelea kwenye eneo hilo itakapobaini ukweli, ifikapo Jumatatu.

Thursday 24 December 2015

MAGAZETI ALIYAMISI YA LEO DECEMBER 24 YAKO HAPA.