Tuesday 22 December 2015

#YALIYOJIRI>>>Makampuni 27 yanayochimba Tanzanite kwenye Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara huenda yakafutiwa leseni, sababu ya ukwepaji kodi. Yapewa hadi Januari 5 kuweka mahesabu sawa.Fahamu zaidi hapa.

Jumla ya Kampuni 27 zinazojihusisha na uchimbaji wa madini ya Tanzanite Mkoani Arusha zitanyang'anywa leseni kwa sababu ya kushindwa kulipa kodi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Amos Makalla amebainisha kuwa uchunguzi unaoendelea unaonyesha kuwa makampuni ya uchimbaji madini yanahusika sana na wizi ukwepaji kodi.

Kamati hiyo ilikutana kuanzia tarehe 10 mwezi Disemba mpaka tarehe 17 kuongelea suala hili.

Makalla amesema kuna wachimbaji takribani 5,000 wanajihusisha na uchimbaji wa Tanzanite na madini mengine ya rangi. Amesema wachimbaji hao wanahusishwa na ukwepaji mkubwa wa kodi wa bilioni.

Amesema kuwa makampuni mengi yanapata faida kubwa lakini hayalipi kodi, alisema Makalla.

Kufuatia hali hiyo mamlaka za mikoa husika zimetoa muda mpaka Januari 5, makampuni yote kuweka vitabu vya mahesabu sawa na kulipa kodi zilizokwepwa.

Muda huo mpaka Januari 5 pia wamepewa raia wa kigeni waliovamia kwenye machimbo na kujihusisha na shughuli za uchimbaji bila kuwa na vibali. Amewataja Raia hao wa kigeni kuwa ni wale wanaotokea nchi za India, Congo na Kenya.

Wiki iliyopita Mfanyabiashara mwenye asili ya India alikamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) akijaribu kutorosha madini ya Tanzanite yenye thamani ya Dola laki Tatu.

0 comments:

Post a Comment