Saturday 12 December 2015

#YALIYOJIRI>>>Sumaye atangaza rasmi kuwa mwanachama wa Chadema.Fahamu zaidi hapa.

Waziri  mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye amtangaza  rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na  amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti  wa chama hicho Mh.Freeman  Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa  CCM na  kudai  kuwa  anaunga mkono  mageuzi yanayofanywa na vyama  vinavyounda  katiba  ya  wananchi (UKAWA) bila  kuweka  wazi  kuwa yuko kwenye chama kipi  kati ya  hivyo amesema asa ameamua  kujiunga na CHADEMA.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa  jimbo la Arusha  kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa Sumaye  amesema anataka  kuungana na wanamageuzi wenzake katika  kuendeleza  harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado  zinaendelea.
Akizungumza  baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho  Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama washirika wa  UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi  azma yaoya  kuleta ukombozi  nchini iko  pale pale.
Awali aliyekluwa  mgombea uras wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado kuna fursa yakufikiwa   kwa malengo yao .
Chanzo
                                                       http://www.itv.co.tz/news

0 comments:

Post a Comment