Friday 4 December 2015

#YALIYOJIRI>>Watuhumiwa 8 wa Upotevu wa Makontena 349 Wafikishwa Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.

WATUHUMIWA nane wa upotevu wa makontena 349 yaliyovushwa Bandarini ya Dar es Salaam bila kulipiwa kodi, miongoni mwao akiwemo Kamishna wa Kodi na Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi tarehe 17 Desemba kwa kuwa  mahakama hiyo haina uwezi wa kusikiliza  wala  kutoa dhamana ya keshi hiyo.

0 comments:

Post a Comment