Saturday 12 December 2015

#MICHEZO>>>SIMBA FC NA AZAM FC ZATOSHANA NGUVU LIGI KUU TANZANIA BARA JIONI YA LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Timu ya Azam FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo, yanaifanya kila timu ijiongezee pointi moja, Azam FC ikifikisha 26 na Simba SC ikitimiza 22 baada ya timu zote kucheza mechi 10.  Azam FC inaendelea kuwa kileleni baada ya Yanga SC nayo kulazimishwa sare ya 0-0 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo hivyo kufikisha pointi 24, wakati Simba SC ikibaki nafasi ya nne.  Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Azam FC wakitangulia kupitia kwa Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ kabla ya Simba SC kusawazisha kupitia kwa Ibrahim Salum Hajib ‘Kadabra’
  Ibrahim Salum Hajib akishangilia goli baada ya kusawazisha.
 Winga Farid Mussa wa Azam FC akitoa pasi mbele ya beki wa Simba SC, Hassan Isihaka
John Bocco akiwatoka mabeki wa Simba SC leo Uwanja wa Taifa.
Baada ya hapo, timu hizo zilirudi kucheza kwa kujihami zaidi licha ya mabadiliko yaliyofanywa na makocha wote, Waingereza, Stwart Hall wa Azam na Dylan Kerr wa Simba SC.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Said Mourad, Erasto Nyoni, Serge Wawa, Himid Mao/Kipre Balou dk46, Abubakar Salum/Didier Kavumbangu dk71, Jean Baptiste Mugiraneza, John Bocco, Kipre Tchetche/Mudathir Yahya dk81 na Farid Mussa.
Simba SC; Vincent Angban, Emery Nimubona/Kessy dk84, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Said Ndemla, Jonas Mkude, Danny Lyanga/Kizza dk68, Ibrahim Hajib na Abdi Banda/Mwalyanzi dk81.

0 comments:

Post a Comment