Monday 29 February 2016

Habari Katika Magazeti ya Tanzania siku ya Jumanne ya March 1 yako hapa.


Breaking News>>>WAZIRI MKUU AAGIZA DAKTARI WA HOSPITALI YA LIGULA MKOANI LINDI ASIMAMISHWE KAZI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.

  • Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa.
  • Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
  • Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
  • Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.

Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.


Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.


Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. "Dirisha la wazee lipo?" akajibiwa hakuna. "Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo" nalo pia akajibiwa halipo. "Je wazee wana daktari wao", hakupata jibu.


"Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee  na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,"  alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.

Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba "tuna jambo, tuna jambo" wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.

Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu.

"Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji."


"Tarehe 12 Februari  baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani".


"Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?" Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza. 


Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.


Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo. 


Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.


"Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho," alisema. 


Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.


Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.
Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua.

Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana.

Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana huu.

#YALIYOJIRI>>>>WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MTWARA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.
 Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016.

Angalia video ya Nay Wamitego inayoitwa "Shika Adabu Yako".Hapa hapa.


#YALIYOJIRI>>> MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR'AN TUKUFU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar.

 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Abubakar Mohamed, aliyepata pointi 86 kwa upande wa washindani wa Juzuu 30, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar.
 Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu
 Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana.
 Dua baada hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, kufunga mashindano hayo.
 Mshiriki Rajab Juma, mshindi wa pili aliyepata pointi 78 katika Juzuu 30
 Mshiriki Mbwana Dadi, mshindi wa tatu aliyepata pointi 75 katika Juzuu 30.
 Mshindi wa kwanza katika juzuu 30, Abubakar Mohamed, aliyepata Pointi 86, akitafakari kabla ya kupanda jukwaani kushiriki.
 Abubakar Mohamed, mshindi wa kwanza akishiriki.

Download nyimbo mpya ya Harmonize_Ft_Diamond_Platnumz inayoitwa "Bado".Hapa hapa.

Toka Lebel ya WCB Harmonize katuletea hii  ambayo amemshirikisha Boss wake, Diamond Platinum kwenye Audio ya Bado’ kutoka kwa producer Flaga na Laizer kutokea lebel ya WCB

Unaweza ukaisikiliza nyimbo ya Harmonize ft Diamond Platinumz ‘Bado’ hapa chini.

#Breaking News>>>WANAFUNZI WACHEZEA BAKOLA ZA FFU LEO JIJINI DAR.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mwanafunzi wa chuo cha St. Joseph kampasi ya Dar es Salaam akiwa miguuni wa Askari leo mara baada ya kuishiwa nguvu wakati wakitawanywa na Askari hao jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakiandamanda kuelekea wizara wizara ya elimu, Sayansi na mafunzo ya Ufundi.
 Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph tawi la jijini Dar es Salaam wakitawanywa na askali wa kutuliza Ghasia (FFU) leo wakati wanafunzi hao wakiandamana wanaelekea wizara ya elimu, Sayansi na mafunzo ya Ufundi kudai kushinikiza chuo hicho (Kampasi)tawi la Arusha kifunguliwe.











#YALIYOJIRI>>>RAIS MAGUFULI AMEFANYIA KAZI SUALA LA BANDARI YA DAR ES SALAAM-SYROSE BHANJI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

  Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwatambulisha wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliofika ofisini kwake leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwaajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano.

BUNGE la Afrika Mashariki limesema kuwa changamoto zilizokuwepo katika Bandari ya Dar es Salaam zimeweza kufanyiwa kazi na Rais Dk.John Pombe Magufuli na kufanya Bandari hiyo kutoa huduma kwa ufanisi.

Hayo ameyasema leo Mwakilishi Bunge hilo, Shy Rose Bhanji wakati Wabunge wa Afrika Mashariki Tanzania walipokutana na Spika Bunge, Job Ndugai kwa ajili ya kufahamiana kutokana wabunge hao wanatokana na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa Bunge la Afrika Mashariki lilikuwa walikuwa wakizungumzia juu ya bandari ya Dar es Salaam katika utoaji uwa huduma lakini sasa Rais Dk.John Pombe Magufuli ameweza kufanyia kazi.
Shyrose amesema wataendelea kutoa ushirikino kwa Rais katika kutumia farsa yake ya Hapa Kazi Tu katika kuwahudumia watanzania.

Nae Mwakilishi wa Spika Owen Mwandumbimbya ambaye ni Afisa Habari wa Bunge amesema kuwa Spika atatoa ushirikiano kwa wabunge kupitia kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy Rose Banji akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufika katika ofisi  ndogo za bunge kwaajili ya kumpongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika, Shy Rose Banji jijini Dar es Salaam leo katika Ofisi ndogo za Bunge.

#YALIYOJIRI>>>>Jeshi la Polisi Zanzibar Latoa Ufafanuzi Kuhusu Madai ya CCM Kutaka Maalim Seif Akamatwe.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni  zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar. 
 
Akiongea  na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.

Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza  kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine

==>Zaidi, bonyeza hapo chini kumsikiliza

#MICHEZO>>>IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.

Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana katika kazi yetu hii ya mpira, napenda kushukuru kwa sapoti kubwa ninayoipaa kutoka kwa familia yangu na mwisho napenda kumshukuru Allah kwa kuendelea kunibariki na neema zake kila siku”
Akimakabidhi tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu ulianzishwa kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa ni utamaduni wetu katika kuwapongeza na kuonesha kuthamini jitihada zinazofanywa na wachezaji wetu katika kuutafuta ushindi wa msimu huu”
Napenda kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu yanapopatikana, aliongeza Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula.
Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba”.
Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa Januari, 2016 litaanza February 29 2016. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi Januari, 2016.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

#YALIYOJIRI>>>Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya yateketea kwa moto.Fahamu zaidi hapa.

Askari wa Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini humo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa, na jitihada za kuuzima zinaendelea.







Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, kikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, wakiwa nje ya Shule yao wakiangalia bila kujua cha kufanya wakati Mabweni yao yakiteketea kwa moto.