Thursday 25 February 2016

#YALIYOJIRI>>>Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa vya Upasuaji.Fahamu zaidi hapa.

   Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akipokea msaada wa vifaa vya upasuaji na Dk Julieth Magandi (wa pili kushoto) wakipokea msaada huo kutoka kwa meneja wa shirika hilo, Bill Bali.
 Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru wakifungua boksi lenye msaada wa vifaa vya upasuaji.
Vifaa vilivyotolewa leo na shirika hilo.
 HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya Dola 38,56.70 za Marekani ambavyo vimetolewa na Shirika la kimataifa la misaada la Project Hope la Marekani.

Daktari wa hospitali hiyo Julieth Magandi amesema kwamba vifaa hivyo vitatumika katika shughuli ya upasuaji mbalimbali ukiwamo upasuaji wa macho na mishipa ya damu.

Dk Magandi amelishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa utaongeza tija katika kazi za upasuaji kwenye hospitali hiyo.

“Tunaomba msituchoke, tutakapohitaji msaada mwingine mtupokee ili Muhimbili endelee kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania,” amesema Dk Magandi.

Naye Meneja wa shirika hilo nchini, Bill Bali amesema kwamba lengo lao ni kutoa misaada mbalimbali ili hospitali hiyo itoe huduma bora za afya kwa Watanzania.

Bali amesema kwamba shirika hilo litaendeleza uhusiano kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kwamba wataendelea kutoa misaada katika maeneo mengi ya hospitali hiyo.


Vifaa hivyo vimepokelewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika ukumbi wa mikutano wa hospitali hiyo.

0 comments:

Post a Comment