Thursday 31 August 2017

Kamati ya Nidhamu TFF Yawatolea Tamko Msuva, Chirwa NA Kaseke.

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemkuta na makosa ya utovu wa nidhamu aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga anayekipiga nchini Morocco, Simon Msuva ambaye imempa onyo kali la barua.

Mbali na Msuva, wengine waliokuwa wakijadiliwa na kamati hiyo kwa utovu wa nidha kwenye michezo ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara ni Obrey Chirwa (Yanga) na Deus Kaseke (Yanga) ambao wamesamehewa.

 
TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Chidi Benz achanganyikiwa, adai ametoka Cuba kufanya wimbo na 2Pac, ameapa kumleta 2Pac bongo.

Chidi Benz adai ametoka Cuba kufanya wimbo na 2Pac, ameapa kumleta 2Pac bongo hivi karibuni, na kila siku wanaongea kwa simu. Tazama

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mtatiro amwambia Diamond sio kila anaemsifia Alikiba ni adui wake.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mahakama Imekataa Kupokea Vielelezo vya Msokoto wa Bangi Kwenye Kesi Inayomkabili Wema Sepetu.

Bado kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi inaendelea kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo leo ilikua ni siku nyingine tena kesi hiyo imeendelea.

Mpya ya leo ni kwamba Mahakama hiyo imekataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Wema na wenzake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro >>> “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani“

Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wamachinga wa Ubungo Wapewa Siku 3 Kuondoka.

WAFANYABISHARA wadogo wadogo, maarufu kama wamachinga, zaidi ya 2,000 walio katika makutano ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela katika eneo la Ubungo Mataa, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam-

Wamepewa siku tatu kuondoka katika maeneo hayo kwa hiari, ili kupisha ujenzi wa mradi wa barabara za juu (fly over).

Baada ya amri hiyo, wamachinga hao waliridhia kuhamia katika soko la Mawasiliano, ambalo limetengwa na Manispaa ya Ubungo kwa ajili yao, baada ya kufanya mazungumzo na Meya wa Manispaa hiyo, Boniface Jacob.

"Tunawapa siku tatu, leo (jana) endeleeni na shughuli zenu hadi Jumamosi mchana muanze kuondoka," alisema Meya Jacob. "Atakayekutwa hapa Jumapili, mimi simo."

Alisema aliamua kufanya mazungumzo na wamachinga hao, ili kuwapatia suluhisho la wapi pa kwenda kufanya biashara zao badala ya kuwaacha na maswali.

Aidha, Meya Jacob alisema wametenga eneo lenye ukubwa wa hekari 12 katika kituo cha Mawasiliano, ambacho ni moja ya vituo vikubwa vya daladala, ambalo litatosha wafanyabiashara 5,000.

"Wamachinga mlioko kando ya barabara eneo hili la Ubungo ni 2,000," aliwaambia meya huyo. "Mawasiliano kuna eneo la kutosha la wafanyabiashara 5,000."

"Hivyo nawasihi kuhamia kule na kama atakuwapo atakayelazimisha kubaki hapa ahakikishe anakaa nje ya mipaka iliyoweka kwa ajili ya kazi hii au kwenda eneo lolote ndani ya jiji la Dar es Salaam."

Jiwe la msingi la mradi huo liliwekwa na Rais John Magufuli mahala hapo Machi 20, mwaka huu.

Rais Magufuli, katika hotuba yake ya uzinduzi, alitaka ujenzi ukamilike kabla ya miaka miwili na nusu ya ratiba ya ujenzi.

BILIONI 186.8/-
Jacob pia alisema vijana wenye ujuzi mbalimbali watapata ajira katika mradi wa flyover na kwamba mama lishe ameshawapatia fursa ya kuwauzia chakula wafanyakazi na vibarua zaidi ya 5,000 watakaohusika na mradi huo.

Mradi wa flyover Ubungo utajengwa na mkandarasi kampuni ya China ya CCECC kwa Sh. bilioni 188.7, ambapo kati ya hizo, Benki ya Dunia (WB) imetoa Sh. bilioni 186.8 na serikali Sh. bilioni 1.9 za usanifu mradi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo, alisema mradi huo unatarajiwa kuanza muda wowote. Alionyesha mipaka, kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na kuwapa muda wa kuondoka eneo hilo.

Mfanyabiashara katika eneo hilo la Ubungo Mataa, Jumanne Nasoro, alisema hawana budi kupisha eneo hilo kwa sababu wasipopisha wanaweza kuharibiwa mali zao.

Pia aliiomba serikali kukarabati na kuweka miundombinu imara katika masoko wanayopangiwa kuhamia, ili kuondokana na changamoto ya wateja kutokuingia humo kwa sababu mbalimbali.

Wakati huo huo, Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema wameanza ukarabati wa soko na eneo la Mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha kuingia na kutoka ndani ya soko hilo.

"Kuna mpango pia wa kupitisha barabara ya mwendo kasi kwa ajili ya kushusha abiria katika kituo cha Mawasiliano hali ambayo itasaidia kuboresha biashara katika soko letu katika siku za usoni," alisema Jacob.
 
TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Waliopanga Ratiba ya Ligi Kuu Kuwajibishwa na TFF.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Kidao amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi wa Bodi ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba.

Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba ya ligi ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo mmoja tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena.

“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,” alisema Kidao.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.


TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Wolper Alizwa na Umati wa Vijana Uliojitokeza Jana Kufanya Usail TRA.

Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Wolper aumizwa baada ya kuona idadi kubwa ya watu waliojitokeza kufanya usaili wa TRA jana na kusema anawaonea huruma yatima ambao hawana mtu wa kuwapigania ili kuweze kupata kazi hizo.

Wolper amebainisha hayo baada ya picha iliyokuwa ikionyesha umati wa vijana waliojitokeza kwa wingi kufanya usaili  wa TRA kwa awamu ya kwanza ambao umefanyika jana na kuendelea leo ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

"Nikiangalia picha kama hizi naumiaga sana na nilivyo na machozi ya karibu basi nalia kabisa. Yaani naona hata wadogo zangu ni miongoni mwa hawa wanaopigania nafasi ya kupewa kazi na ukizingatia nimesomesha kwa tabu sana tena nilikuwa sina hata biashara huku nikisaidiana na wazazi wangu. Roho inauma pale ambapo mdogo wako anakwambia Dada nimepata kazi ya kujishikiza kwa wiki tatu nitalipwa laki na nusu kule Mkoani Mbeya kijijini tena hapo ni uliyemfikiria akipata 'degree' yake atakuja japo kuinua familia ama ajitegemee mwenyewe lakini siyo hivyo", aliandika Wolper.

Pamoja na hayo, Wolper aliendelea kwa kusema "mimi najiuliza unaposema ipo siku sijui hiyo siku ni ipi. Haya wote hao waliojitokeza huku wanaohitajika ni wachache yaani kwa uwiano ni kama mtu mmoja achaguliwe kati ya watu 140 kwa sababu ni watu 56,000 kwa nafasi 400 kama 'data' ziko sahihi, Mungu wangu bora hata mdogo wangu ataomba hela ya vocha na kula na kulala atapata. Lakini vipi waliyosomeshwa na wazazi wa kambo au kwa msaada", alihoji Wolper.
Huu ndiyo ujumbe aliyoandika Wolper katika instagram yake.

Jacqueline Wolper siyo mtu wa kwanza kuonyesha hisia zake juu ya tukio lililotokea siku ya jana katika usaili huo kwa maana kila aliyeweza kuona picha hiyo hakuweza kujizuia kutoa dukuduku lake la moyoni.


TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Jeshi la Polisi Lawaonya Wakina Amber Lulu na Wengine Wanaopiga Picha za Utupu na Kuzirusha Mitandaoni.

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limetoa onyo kwa watu wanaopiga picha za utupu na kuzirusha mitandaoni, huku likisema kuwa litawachukulia hatua watu hao kwani wanavunja sheria.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa, amesema vitendo hivyo ni uvunjaji wa sheria za makosa ya kimtandao na haviwezi kuvumilika.

“Hilo ni kosa kama kosa lingine, ni uvunjaji wa sheria za makosa ya kimtandao, mtu yeyeote akija kulalamika Jeshi Polisi halitalifumbia macho, kwa sababu vitendo hivyo ni udhalilishaji wa utu wa mtu wa hali ya juu na haviwezi kuvumilika, ukithibitika unafanya kitendo hicho Jeshi la Polisi halitakuacha salama, litakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”, alisema Kamanda Mambosasa.

Vitendo vya upigwaji wa picha za utupu na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii vimekuwa vikishamiri nchini Tanzania, ambapo hivi karibuni msanii Amber Lulu alifikishwa katika kituo cha polisi cha Ubungo kwa kosa hilo
TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tuesday 22 August 2017

Mwanamke Achoka Kuwa Single Aamua Kupita Barabarani na Bango Akitafuta Mume wa Kumuo.

Mwanamke mmoja nchini Kenya ameingia katika barabara za mji mkuu Nairobi, akiwa na bango lenye maandishi yanayosema kuwa anatafuta mwanamume wa kumuoa.

Akiwa amevaa nguo nyeupe sawa nguo inayovaliwa Bi harusi, Pris Nyambura mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, alikuwa na bango lililosema.

"Ninahitaji bwana, nina mtoto msichana wa umri wa miaka saba"

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Korea Kaskazini Yatishia Kujibu Zoezi la Kijeshi la Marekani.

Korea Kaskazini imetishia kujibu vikali zoezi la pamoja la kijeshi lililofanywa na majeshi ya Korea Kusini pamoja na yale ya Marekani.
Msemaji wa jeshi kutoka Kaskazini alisema kuwa anatazama kwa makini kile ilichokitaja mchezo wa kivita wa Marekani .

Pyongyanga imetishia kurusha makombora katika bahari ya kisiwa cha Guam ambacho kina kambi kubwa ya wanahewa wa Marekani .

Wasiwasi huongezeka wakati wa zoezi hilo la pamoja la kila mwaka, na kwamba hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la masafa marefu linaloweza kushambulia Marekani.
Mwaka uliopita Pyongyang ilijibu zoezi hilo la kijeshi kwa kufanyia majaribio kombora lake.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Roma: Mimi si Kada wa CHADEMA na Sijawahi Kuwa Kada wa Chama Chochote.

Msanii Roma Mkatoliki ambaye anaimba muziki wa Hip hop kwenye game ya bongo, amekikana chama cha CHADEMA na kusema kuwa hajawahi kuwa mwanachama wa chama hicho kama ambavyo wengi wanaamini, na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.


Roma ambaye hivi karibuni alikutwa na sakata la kutekwa na kuibua sintofahamu nyingi, amesema kwamba hajawahi kuwa mwanasiana na hajawahi kuwa na kadi ya chama chochote.

"Mtu akisema nipo kwenye siasa za upinzani siyo jambo sahihi na siyo jambo ambalo nalifurahia kwa sababu mimi sina kadi ya chama chochote, mimi siyo mwanachama wa chama chochote, na mtu akisema nusu ya watanzania wanajua uko CHADEMA sijui ana uthibitisho gani kwa sababu sina kadi ya chama, na mimi nasimama kati kati", alisema Roma Mkatoliki.

Roma hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa 'Zimbabwe' ambao umeibua hisia kwa wengii, kwa kuelezea tukio zima la utekwaji wake ulivyokuwa. Wimbo ambao mpaka sasa umeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kitu ndani ya wiki moja.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mcheza Mpira Okwi Ajitapa Kufunga Goli Moja Katika Mchezo wa Kesho.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi Yanga ‘Ngao ya Hisani’ kesho (Jumatano) atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete kusema ni magoli mangap

Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika ‘gongo wazi’ Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.

“Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda”, alisema Okwi.

Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema “nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri”, alisisitiza Okwi.

Okwi ameanza tambwe hizo ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi siku ya kesho (Jumatano) ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzake.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo wa Fid Q Ft. Diamond Platnumz & Rayvanny unaoitwa "Fresh Remix".

https://my.notjustok.com/track/download/id/261570


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mahakama Yaelezwa Jinsi MKOJO Wa Yusuf Manji Ulivyochukuliwa na Kupimwa.

Mashahidi wawili akiwemo Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ofisa wa Polisi, Ramadhan Kingai leo  wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi Mfanyabiashara Yusuf Manji alivyopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mbali ya Kingai ambaye ni Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya dawa za kulevya inayomkabili Manji, Shahidi mwingine ni E.1125 Copro Detective Sospter.

Mashahidi hao walitoa ushahidi wao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis kueleza kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya ushahidi.

Akiongozwa na Wakili Vitalisi, Shahidi Kingai amedai kuwa February 9, 2017 akiwa Ofisini kwake Central alikuwa na kazi mbalimbali ikiwemo ya kuripotiwa kwa watuhumiwa wa Dawa za kulevya waliotajwa na RC Makonda.

Amedai katika watuhumiwa hao alimpokea Yusuf Manji na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima baada ya kuripoti wenyewe kituoni hapo.

“Baada ya kufika nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa dawa za kulevya nilielekeza Manji na Gwajima wapelekwe kwa Mkemia Mkuu kupimwa, kwa sababu tuhuma zao ni za dawa za kulevya, ambapo pia walienda kupekuliwa nyumbani mwao”

Shahidi huyo akadai kuwa amri ya kupimwa ilitekelezwa na Detective Copro Sospeter, ambapo baada ya kufanyika uchunguzi akapewa taarifa kwamba Manji anatumia Dawa za kulevya aina ya Benzodiazepines na Gwajima hatumii.

“Nikiwa kama Mpelelezi Mkuu niliichukua ripoti hiyo kisha nilielekeza Manji afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya ambapo baada ya kufunguliwa lilipelekwa kwa DPP”.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo alimuuliza shahidi huyo kwa nini dawa za kulevya (Benzodiazepines) alizozitaja Mkemia Mkuu ni tofauti na zilizotajwa kwenye hati ya Mashtaka (Heroin) ambapo shahidi huyo alijibu hajui na yeye hakuandaa hati ya mashtaka.

Shahidi wa pili, Detective Copro Sospeter akiongozwa na Wakili Vitalis alidai kuwa February 9, 2017 saa 5 asubuhi alikuwa Ofisini na alimpeleka Manji kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuchubguzwa.

Alidai kuwa maelezo ya kumpeleka Manji kwa Mkemja aliyapata kwa Kingai, ambapo alimpeleka kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

” Nilimchukua Manji na kumpeleka msalani ili ichukuliwe sampo ya mkojo wake ufanyiwe uchunguzi, ambapo kuna kielelezo cha fomu kuhusu suala hilo na naomba kipokelewe na Mahakama.”

Alieleza kuwa baada ya mtuhumiwa kuchunguzwa alichukua majibu kisha alirejeshwa Polisi na taratibu kufatwa.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hadi August 23, 2017.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Sumaye Afunguka Maneno MAZITO Kuhusu Sakata la Serikali Kuchukua Mashamba Yake.

Waziri  Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amevunja ukimya na kusema  kwamba watawala wanaendesha nchi  kwa visasi ndiyo maana tangu ahame Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)amezidi kuandamwa  ikiwamo kunyang’anywa mashamba anayoyamiliki kihalali.
 
Sumaye ambaye kwa sasa ni  Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani  Chadema, amesema tangu ajiunge na upinzani amekuwa akikumbana na vikwazo vingi, ikiwamo kudhauliwa pamoja na  kuporwa mashamba yake kwa kisingizio kwamba ameshindwa kuyaendeleza.
 
Amemtuhumu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwamba anajua ukweli kuhusu mashamba yake lakini hataki kuusema kwa kuwa ametumwa na mkubwa wake.
 
Ametaja mashamba aliyoporwa kuwa ni lile la Mvomero mkoani Morogoro na lililopo Mabwepande katika  wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambayo yote serikali imefuta hati za umiliki wake.
 
Amesema shamba la Mvomero linamilikiwa na mke wake Ester Sumaye ambalo lina ukubwa wa hekari 326, na kwamba huko alikuwa anafuga ng’ombe zaidi ya 200, kondoo 300, ghala la kuhifadhia chakula, trekta na nyumba mbili za kudumu.
 
Sumaye akizungumza na waandishi wa habari leo katika  ofisi za makao makuu kanda ya Pwani  (Chadema) , amesema mgogoro  huo ulianza mara baada tu ya yeye kuhamia upinzani.
 
Amesema muda wote aliokuwa ndani ya CCM,  hakuwahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala kusumbuliwa kuhusu mali zake yakiwamo mashamba.
 
“ Mara baada tu ya mimi kuhama wapo viongozi waliodiriki kusema huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kumnyang’anya mashamba, kama moja ya kunikomoa tu, hivyo ni dhahiri kuwa ni uadui kati ya serikali na mimi kwa sababu ya kuhamia upinzani.” amesema Sumaye.
 
“Mashamba hayo wanadai wameamua kuninyang’anywa kwa kuwa siyalipii kodi na kutoendelezwa hivyo yanatakiwa kuchukuliwa na kuwagawia wananchi kitu ambacho si weli kwani shughuli za kilimo katika mashamba hayo zilikuwa zikiendelea kama kawaida.”
 
Sumaye amemtaka, Lukuvi kutumia nafasi yake vizuri kwani kwa kuendeleza uadui wa  kisiasa hakuwezi kulisaidia taifa badala yake kutazidi kukandamiza demokrasia hapa nchini.
 
Sumaye ameionya serikali ya awamu ya tano na kuitaka iache  kulipa visasi kwa wapinzani na kuwatahadharisha  watawala kwamba dhambi itawatafuna kwani wapo viongozi wengine wa CCM wana mali nyingi na mahoteli makubwa kuliko shamba lake lakini hawaguswi.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Hatimaye Ester Bulaya Ahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH ) baada ya kufikishwa kwenye hospitali hiyo akitokea Hospitali ya Bugando, Mwanza.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen ilieleza kuwa, Bulaya alifikishwa hospitalini hapo jana usiku. "Tulimpokea jana usiku,"alieleza kwa kifupi.

 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amethibitisha pia kulazwa mbunge huyo MNH,  "amelazwa private, Sewahaji, wodi namba 18," alisema Halima Mdee.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Maneno ya Afande Sele kwa ‘umarioo’ Asema Unapunguza Nguvu za Kiume.

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amedai kuwa vijana wa kiume kujihusisha katika mapenzi na wakubwa zao ili kusaidiwa kiuchumi ni moja wa sabubu zinazopelekea upungufu wa nguvu za kiume.

Afande Sele ameeleza kuwa kitendo hicho kinamnyima uhuru binafsi muhusika kwa sababu unapokaa na mtu ambaye kila kitu unamtengemea unakosa uhuru wa maisha.

“Hata uwezo wako wa kufikiri unapungua kwa sababu unajikuta muda mwingi unafikiria kumfurahisha mtu. Muda mwingine hata mapenzi unakuta hujisikii kwa sababu mapenzi nayo ni ratiba lakini kwa sababu unaishi na mtu anakulea utafanya tu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Ndio maana leo hii suala la nguvu za kiume limekuwa ni agenda kubwa kwa sababu wanafanya vitu na watu siyo machaguo yao ila wakijiari kwenye vitu kama kilimo watakuwa na maisha ya uhuru sana,” amesisitiza.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Roma Mkatoliki Amtetea Mkewe...'Mke Wangu Kupost Instagram Atanipa Staili zote Hajakosea'.

Msanii Roma mkatoliki akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo EA Radio amesema aliulizwa ni staili ngapi mkewe amempa, akasema kwa kuwa neno style lina herufi nne basi ni staili nne
Alipoulizwa mkewe hajashtuka alipoona post yake imeenea sana, alisema hakuwa na cha kushtuka kwa kuwa hajakosea

 TAZAMA VIDEO:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mr Nice Azushiwa Janga Lingine Nchini Kenya.

Msanii wa mkongwe wa muziki, Mr Nice ambaye kwa sasa anaishi nchini Kenya amekuwa alizushiwa mambo mabaya na vyombo vya habari kila kukicha ambapo Jumatatu hii katika sherehe za kuapishwa kwa Sonko amezushiwa kitu kingine.

Muimbaji huyo katika show hiyo alidaiwa kuibiwa baadhi ya vitu baada ya kuvamiwa na mashabiki kitu ambacho amekanusha.

“Waandishi vilaza mnapenda kurukia sana hata msilolijua mimi katika show ya kuapishwa Sonko leo sijaibiwa na mtu yoyote,” Mr Nice aliandika Facebook “Kifupi ni kwamba mashabiki waling’ang’ana kucheza na mimi na bahati mbaya wakajikuta wamekata cheni zangu na pia leseni yangu ikadondoka nilikuwa nayo kwa mfuko wa koti la suti,”

Aliongeza, “Mkome kabisaaaa kutengeneza ishu za kipumbavu ili muuze vijikaratasi vyenu huko mtaani. Kenya iko sawa na hakuna tatizo lolote kabisaaaaaa na bado 21/8/2017 tuwache rafiki yangu Sonko achape kazi na Nairobi ifaidike naye,”

Miezi miwili iliyopita muimbaji huyo alizushiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

BREAKING NEWS: Tundu Lisu Adaiwa Kukamatwa Nje ya Mahakama na Polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu  amedaiwa kukamatwa leo Jumatatu mchana akitokea  Mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria  huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi  lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo.

Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa  na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Sunday 20 August 2017

ANAOMBA Ushauri..'Kila Akifika Kileleni Ananing'ata Shingoni.

Nautandika uzi wangu huu hapa kuomba ushauri nifanyaje au dawa yake ni nini katika tatizo hili linalonisibu!

Nina mpenzi wangu niko kwenye mahusiano mwezi wa tisa sasa hivi,tatizo ni pale tunapokuwa ndani ya sita kwa sita huwa ananing'ata .Hii hali humtokea mara nyingi sana hasa hasa kipindi kile ambacho anakuwa anafika orgasm(female),hapa nilipo ukinikagua vizuri kifuani nina makovu kadhaa hadi kuwa chest game inakuwa aibu

Yani inakuwa shida kiasi natakiwa kujihami mara nikiwa namshughulikia hasa pale anapokuwa anakaribia orgasm kwa kutafuta stail ya kujiweka mbali na mdomo wake-lakini kama unavojua kipindi hiki mtu anaongezeka nguvu mara 100 so mara nyingi mimi naishia maumivu,na nimekuwa type ya wanaume ambao na last long in bed (enough stamina) hivo basi katika one shot naweza hata ng'atwa mara 3

Nikimuuliza mwenzangu anasema yeye hua hajitambui anapofanya kitendo hiko(biting) na kuishia kuni promise atajitahidi kujizuia next time lakini wapi -game inaishiaga vilevile.Kwa hali hii mimi naona kero hadi nafikiria kumuacha hali nampenda tena sana,sasa kabla sijafanya hivyo naombeni ushauri nifanyaje au hii hali inatibika na dawa yake nini?

Abadala

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mahakama Yazuia Bomoabomoa kwa nyumba 286 Dar.

Wakati operesheni ya ubomoaji wa nyumba zilizoko ndani ya umbali wa mita 121.5 kutoka katikati ya Barabara ya Morogoro ikiendelea maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya jijini Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeziwekea kinga ya muda nyumba 286 zinazohusika.

Uamuzi huo wa Mahakama ulitolewa juzi na Jaji Leila Mgonya kutokana na maombi ya zuio yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wakazi hao 286 wa maeneo ya Ubungo- Maji hadi Kiluvya wakiomba itoe zuio la muda hadi kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Maombi hayo ya zuio la muda kusubiri uamuzi wa kesi ya msingi yamepangwa kusikilizwa Agosti 30 baada ya upande wa wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha hati ya kiapo kinzani.

Hata hivyo, wakati wakisubiri usikilizwaji wa maombi ya zuio la muda, wananchi hao kupitia kwa wakili wao, Benito Mandele waliwasilisha maombi ya dharura wakioomba mahakama hiyo iamuru hali iendelee kuwa kama ilivyo kwa sasa hadi maombi hayo yatakaposikilizwa.

Jaji Mgonya anayesikiliza shauri hilo alikubaliana na maombi hayo na kuamuru hali iendelee kuwa kama ilivyo kwa sasa hadi tarehe hiyo ya maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Kwa uamuzi huo, Tanroads ambayo ndiyo mtekelezaji wa operesheni hiyo haitaweza kuzigusa nyumba hizo hadi hapo mahakama itakavyoelekeza vinginevyo baada ya usikilizwaji wa maombi hayo ya zuio la muda kusubiri kesi ya msingi kumalizika.

Wakili Mandele alisema kuwa watakachofanya baada ya kupata hati ya amri hiyo ya mahakama wataitoa nakala nyingine na kuwagawia kila mdaiwa kwa ajili ya kuiweka kwenye nyumba yake.

Katika kesi ya msingi namba 284 ya mwaka 2017, wananchi hao wanaiomba mahakama itamke kuwa wao ni wamiliki halali wa maeneo hayo yenye mgogoro na kwamba hawapo katika hifadhi ya barabara.

Pia, wanaiomba mahakama hiyo iamuru kuwa kama Serikali inata kuwahamisha na kuyachukua maeneo yao, basi iwalipe fidia stahiki kwa mujibu wa sheria.

Tanroads imetoa notisi kwa wakazi wote walipo katika umbali wa mita 121.5 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro kila upande, kuanzia Ubungo - Maji hadi mpakani mwa Dar es Salaam na Pwani kuvunja nyumba zao kwa madai kuwa wapo kwenye hifadhi ya barabara.

Hivyo, Tanroads waliwataka wananchi hao kuondoka katika maeneo hayo ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

Wananchi hao wanapinga amri hiyo wakidai kuwa wanaishi katika maeneo hayo kihalali kwa kuwa wana hatimiliki halali na hawapo kwenye hifadhi ya barabara, huku wakihoji sheria iliyotumika kuidhinisha umbali huo wa mita 121.5.

Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wameamua kwenda mahakamani katika makundi tofauti na kufungua kesi tofautitofauti kupinga operesheni hiyo wakidai kulipwa fidia kama Serikali itawahamisha.

Mbali na kesi hiyo iliyotolewa amri hiyo, pia kuna kesi nyingine mbalimbali ambazo ziko katika hatua mbalimbali.

Kesi hizo nyingine ni ile iliyofunguliwa na Abdallah Maliki kwa niaba ya wenzake 570 ambao ni wakazi wa maeneo ya Kimara, Mbezi na Kiluvya dhidi ya Tanroads na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa upande mwingine.

Shauri jingine ni maombi ya kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi kupinga operesheni hiyo lililofunguliwa na Ephrahim Kavishe na wenzake wanne ili wawe wawakilishi wa wenzao zaidi ya 198 ambao ni wakazi wa Kimara Stop Over na Mbezi.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mmoja wa wajibu maombi hayo amewawekea pingamizi akiiomba mahakama hiyo iyatupile mbali maombi hayo huku akiainisha kasoro mbalimbali za kisheria.

Maombi hayo yanasikilizwa na Jaji Crencecia Makuru na amepanga kutoa uamuzi kuhusu pingamizi hilo Agosti 30, uamuzi ambao ndio utakaotoa hatima ya maombi hayo kama yataendelea kusikilizwa au yatatupiliwa mbali. 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Chege inayoitwa "Run Town".

https://my.notjustok.com/track/download/id/260547


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Serikali Yamjibu Tundu Lissu Sakata la Ndege Kushikilia Canada kisa Madeni.

Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8 nchini Canada.

Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

"Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia" alisema Zamaradi Kawawa

Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli

"Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli  katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa

Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo

"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa

Hapo Jana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ndege hiyo imeshindwa kuwasili nchini kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania nakupelekea kukamatwa kwa Ndege hiyo mali ya Tanazania.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Roma & Stamina ( Rostam ) unaoitwa "Hivi Ama Vile".


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa