Friday 18 August 2017

VIDEO...Tundu Lissu Awalipua Siro na Kapilima..Adai Kuna Vijana Wametumwa Kumfatilia Maisha yake.

Leo Tundu Lissu ametoa ya Moyoni kwamba anawindwa na kufuatiliwa na vyombo vya Usalama. Amewasihi Vyombo vya Usalama vipambane na Wahalifu sio Wanaoikosoa Serikali

"Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.

Wakubwa hawa wa Vyombo vyetu vya Usalama wawaelekeze watumishi wao watumie muda na rasilimali za nchi hii wafanye kazi ya kupambana na Waharifu sio kupoteza muda wao na pesa zetu kuhangaika na raia ambao wanatimiza wajibu wao wa kuiwajibisha Serikali iliyoko Madarakani.

Kwahiyo Afande Sirro na Afande Kipilimba, fanyeni kazi ya kupambana na Wahalifu na tuachieni kazi ya kuwaajibisha walioko Madarakani kwa mjibu wa Sheria za Tanzania". VIDEO:


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment