Tuesday 22 August 2017

BREAKING NEWS: Tundu Lisu Adaiwa Kukamatwa Nje ya Mahakama na Polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu  amedaiwa kukamatwa leo Jumatatu mchana akitokea  Mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria  huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi  lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo.

Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa  na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment