Tuesday 15 August 2017

Maskini.. Huyu Ndiye Binti Aliyepigwa na Mke wa Mugabe na Kusababishiwa Majeraha.

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumsabababishia majeraha binti mmoja aliyemkuta na wanawe wawili wa kiume mjini Johannesburg, Afrika Kusini juzi Agosti 13 alikokuwa amekwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya mguu.

Mugabe akiwa na mke wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Bulawayo 24 ya nchini Zimbabwe na jumbe mbalimbali zilizotumwa kupitia mtandao wa Twitter mjini Johannesburg na Harare, zimedai kuwa Grace Mugabe alimshambulia binti aliyefahamika kwa jina la Gaby kwa kutumia waya wa umeme baada ya kumkuta na wanae wawili, Robert Jr (25) na Chatunga (21).


Watoto hao wawili ambao wapo mjini humo kimasomo wanafahamika kwa kula bata zaidi kuliko kusoma, kitu ambacho ndio lengo la wao kuwepo nchini humo.

Hivi karibuni Robert Mugabe Jr, na Chatunga Bellarmine, walifukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi eneo la Rivonia baada ya kusababisha usumbufu kutokana na kelele za muziki na watu
waliokuwa wakija katika nyumba hiyo.Hata baada ya kufukuzwa, walitakiwa kuikarabati nyumba hiyo.

Msichana huyo aliyepigwa na Grace alipata jeraha kichwani kwake na kwamba walinzi walikuwa wakishuhudia namna anavyoshambuliwa na mke huyo wa Rais wa Zimbabwe.


Toa Maoni yako Hapa Chini:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment