Sunday 20 August 2017

Serikali Yamjibu Tundu Lissu Sakata la Ndege Kushikilia Canada kisa Madeni.

Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8 nchini Canada.

Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

"Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia" alisema Zamaradi Kawawa

Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli

"Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli  katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa

Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo

"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa

Hapo Jana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ndege hiyo imeshindwa kuwasili nchini kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania nakupelekea kukamatwa kwa Ndege hiyo mali ya Tanazania.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment