Wednesday 9 August 2017

Mama Diamond Afunguka Makubwa "Mtoto wa Hamisa Mobetto ni Mjukuu Wangu".

Baada ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto kujifungua mtoto wa kiume na story zikisambaa kuwa mtoto huyo ni mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz ingawa wenyewe wanazikanusha, sasa leo mama mzazi na dada wa Diamond wamefunguka.

Wakiongea kwenye na Soudy Brown kwenye U HEARD ya XXXL ya Clouds FM baada ya kuendelea kusambaa kwa taarifa hizo nao walifunguka.


Hamisa rafiki yangu siyo wifi yangu lazima niwe na furaha kwa sababu kajifungua salama. Wewe ulikuwa unataka nifanyeje? Hizo habari za Diamond mimi sizijui. Niulize mambo yangu. –  Esma.

“Wewe unanitafuta nini Soudy? Naumwa kifua. Watoto wote ni wajukuu zangu hata wewe mtoto wako ukizaa mjukuu wangu. Wewe mwenyewe mwanangu, mtoto ukizaa mjukuu wangu. Wewe ni shushushu mbona hujafika Hospitali kumuona? Walioniona nimeenda Hospital waambie wakuhadithie vizuri. Mimi namuombea maisha mema alee mtoto wake vizuri kwa amani na furaha.” – Mama Diamond


Toa Maoni yako Hapa Chini:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment