Saturday 19 August 2017

Mwamuzi Mechi ya Watani wa Jadi Simba na Yanga Huyu Hapa.

Mwamuzi bora wa msimu uliopita, Elly Sassi mwenye umri wa miaka 28 ndiye atakayechezesha mechi ya watani Yanga na Simba.

Simba na Yanga zinakutana Jumatano ijayo katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18 utakaoanza rasmi Agasti 26.
Sassi ambaye ndiye mwamuzi bora Ligi Kuu msimu ulioisha 2016/2017.

Mwamuzi huyu kijana, amekuwa akitabiriwa kufika mbali kutokana na ubora wa kazi yake huku pia akitajwa kuwa ni mmoja wa waamuzi wenye misimamo ya kufuata sheria na kanuni za mchezo wa soka na si mtu wa kuteteleka katika maamuzi yake jambo ambalo linamfanya kumudu michezo mingi mikubwa ya ndani na nje ya nchi.

Tayari kuelekea mchezo huo mgumu mno kwa pande zote mbili yaani Simba na Yanga vilabu hivyo vyote vimekimbia jiji na kwenda kujifisha kisiwani Zanzibar, Wakati Simba wakiwa kisiwani Unguja wenzao Yanga wao wako Kisiwa cha Pemba.




Toa Maoni yako Hapa Chini:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment