Wednesday 9 August 2017

Mimi Nipo Sexy Sana na Nina Mvuto Sidanganyiki na Vichips Mayai – Lulu Diva.

Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amejimwagia sifa jinsi anavyoamini kuwa yeye ni mzuri.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa alitambua kuwa yeye ni mzuri kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi kitu ambacho  kilimfanya kutolaghaika na watu waliokuwa wakimsifia.


“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua,” amesema na kuongeza.

“Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.

Hitmaker huyo wa Usimwache kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Utamu.

Toa Maoni yako Hapa Chini:

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment